Tamthilia ya Huba haiendani na jina lake. Kinachoendelea ni upotoshaji na uhuni

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
TAMTHILIA YA HUBA HAIENDANI NA JINA LAKE. KINACHOENDELEA NI UPOTOSHAJI NA UHUNI TUU.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Wanafilamu wengi walikuwa wakilalamika hakuna wawekezaji katika tasnia ya filamu ndio maana kazi zinazotoka ni mbofumbofu. Miaka ya hivi karibuni kumetokea mabadiliko kidogo yenye matumaini katika tasnia hii baada ya dunia kuhama kutoka analojia kwenda dijitali. Uwepo wa Dstv na makampuni mengine umekuwa kichocheo cha ukuaji wa tasnia ya uigizaji hapa nchi.

Wawekezaji haitakuwa kisingizio tena. Watanzania walitarajia kuona kazi nzuri zenye kupendeza, zenye kusisimua, utunzi wenye ubunifu wa kipekee, tamthilia zenye mipangilio ya visa, matukio na maneno ya kisanaa yenye kuleta akili mpya ndani ya jamii.
Lakini Taikon ninasikitika kuwa bado kuna ombwe kubwa katika Filamu zetu.

Ukiangalia uigizaji wa wasanii wetu hauna tofauti na ule uliokuwa unafanyika sekondari. Yaani ni kama watoto wadogo hivi ambao wanaigiza Kibabababa na kimamamama.

Ninaamini Waigizaji hawana makosa kwa sababu muigizaji anaigiza kulingana na mtunzi na muongozaji atavyotaka filamu ichezwe. Tatizo kubwa la Tasnia ya filamu hapa nchini ipo kwa Watunzi na waongozaji wa filamu.
Uwezo wa Watunzi upo chini sana. Mtunzi ndiye chanzo cha Filamu. Yeye ndiye anayeandaa kisa, matukio, wahusika, mandhari nzuri.k.
Muongozaji wa filamu ambaye pia anaweza kuwa mtunzi yeye kazi yake ni kuwa katika ulimwengu halisi na kuchagua wahusika na mandhari halisi inayoendana na simulizi ya mtunzi hata kama ni ya kubuni. Muongozaji wa filamu lazima amuelewe mtunzi alikuwa anapicha gani kichwani mwake katika stori yake. Ndio maana inashauriwa kama mtunzi yupo ni bora muongozaji wa filamu amshirikishe ili filamu itoke kama ilivyokusudiwa.

Tuachane na mambo hayo. Turudi kwenye mada.

1. Filamu za Bongo zinatatizo la misconceptions.
Nafikiri hii inatokana na watanzania wengi pia kuwa na tatizo hili.
Wabongo wengi tunatatizo la misconceptions katika baadhi ya ishu. Mfano wabongo wengi wanashindwa kutofautisha kati ya heshima na Woga.
Sio ajabu ukamsikia mtu akisema ukiwa na pesa unaheshimika wakati heshima inatokana na matendo yenye heshima, maadili mema. Badala ya kusema ukiwa na pesa unaogopeka.

Upendo Vs Tamaa.
Watanzania wengi wanashindwa kutofautisha kati ya upendo na tamaa. Na hiki ndicho kinachojitokeza kwenye filamu ya huna.
Huba kwa lugha nyingine huitwa upendo "mapenzi ya dhati" ambapo pakiwa na huba automatically hakuwezi kuwa usaliti.

Lakini ukitazama kwenye tamthilia ya huba kuna hiyo misconception ya kuchanganya huba na tamaa.
Mtunzi anafikiria kila mapenzi ni HUBA. Wakati mapenzi yasiyo ya dhati huitwa tamaa. Na mapenzi ya kweli ndio huitwa HUBA.

Ukifuatilia kinachoendelea kwenye tamthilia hiyo utagundua kinachoendelea ni umalaya, uhuni na tamaa mbaya. Na wala hakuna kitu kinachoitwa Huba kama jina la tamthilia lilivyo.

Umalaya, uchafu, na uasherati uliovuka mipaka ndicho kinachoendelea humo ambapo ni kinyume cha Huba. Kuchukuliana Mabwana, kuchukuliana Wake.
Mara Mama anatoka na Kijana wake wakiume.
Mara Baba "JB" anatoka na Mke wa Mkwe wake "Tima" yaani uchafu uchafu tuu. Filamu inanuka uchafu tuu. Hakuna huba hata sehemu moja.

2. Kuwajibika kisheria hakuna.
Mtu kafanya uhalifu kwa mfano kaua au kateka. Mtunzi hajaandaa kisa cha namna ya kushughulikia wahalifu katika simulizi yake.
Jambo hilo limejitokeza pia katika tamthilia ya wimbi. Tukio la utekaji limetokea, hiyo ni jinai ni lazima mtunzi angeandaa wahusika wengine wa kisheria kama polisi wakifuatilia tukio hilo.
Haya huku kwenye tamthilia ya Huba, Mke wa JB aliuawa, lakini ufuatiliaji wake hauridhishi ni kama kesi imetekelezwa hewani.

Angalau Pazia walijitahidi kwenye kipengele hiki.
Mnashindwa na Wakenya kama kwenye Semina, Kovu, n.k.
Mtunzi lazima ukishatunga kisa cha uhalifu lazima jicho lako na kalamu yako iwe kali mno kuhakikisha unaandaa tukio jingine mbele kumuadhibu mhalifu na kuleta madhara makubwa yatokanayo na huo uhalifu ili jamii ijifunze kuwa uhalifu sio mzuri. Watu waogope.

Lakini ninyi mnafundisha Watu umalaya, kudanga, kufanya uasherati. Yaani mawazo kama watoto wanaobalehe Balehe hivi muda wote kuwaza mapenzi tena katika namna nyepesi kabisa.

Ati huyu kamtongozo huyu kisha Kalala naye, kisha kumfuata tena Dadaake Kalala naye, mara Kalala na mama yake.
Mara mkwe na mkwe wanalalana tena. Mpaka unajiuliza hivi haya mambo yanafanywa na watu wenye akili timamu kweli.
Tena bila aibu yapo live nchi nzima Watu waone kuwa Watanzania ni wajinga kwa kiwango hiki.

Badilikeni bhana!

3. Ubunifu katika Visa hakuna.
Ubunifu wa migogoro hakuna hata unajiuliza hivi tamthilia maana yake nini. Yaani unakuta kipande kizima kinaenda Watu wanajizungusha zungusha tuu.

Alafu kuna ile kasumba mbaya ya kudhani kupiga piga kelele na kutupiana maneno makali ati ndio migogoro. Embu acheni hizo.

Kwa mfano kwenye filamu ya Huba mgogoro ambao ungevutia zaidi ni ule wa kuchunguza nani aliyemuua mke wa JB?
Mhusika mmoja anafuatilia kuhakikisha muuaji anapatikana mhusika mwingine anakazana kuficha.
Upande mwingine mgogoro mwingine wa kuchunguza mali za JB zinatokana na nini na sio iishie tuu kwenye mambo ya kishirikina, kusadikika ambayo hayana uhalisia.

Haya athari za baba na mama kuachana lazima mgogoro mwingine ungezuka kwa kuonyesha jinsi watoto wanavyopata tabu, na lazima watoto wapewe kipande wacheze.

Kwa vile jina la tamthilia ni HUBA, lazima kuna wahusika wawili ambao wangekuwa wanapendana sana kiasi kwamba nguvu ya mapenzi ingeonekana.
Wengine wanajaribu kuyasukasuka hayo mahusiano na kuyateteresha lakini wahusika hao ( love birds) wanapitia hizo changamoto lakini wanashinda majaribu.
Hivyo ndivyo mambo yanavyoenda.

Sasa ushasema Huba alafu muda huohuo unaonyesha nguvu ya Pesa kwamba pesa inaweza kuvunja Huba. Hii haipo hivyo. Labda kama huba yenye maana ya kudanga hapo sawa.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Bongo muviiii
1702059224873.jpg
 
Yan bongo hamna kisa tofaut na mape z ,
Loloita -tofaut na kiss cha lolita visa vingine ni upuuzi tu , yan huyu kalala na huyu na huyu utafikiri hamna visa tofauti n mapenzi.
Kama utamruhusu mwanao aangalie kaza moyo - akija kuwa panyaroad au malaya usiseme kajifunzia wapi ww ndo umemfundisha
 
Visa havina muunganiko, kijana kaiba boda boda, ambayo aliyeibiwa ni mtumishi nae mtumishi katembea na mke wa mtu, yule mke wa mtu ana tatizo la ugumba,kaenda kwa mganga akabakwa, polisi wakafatilia kabla hawajamkamata mganga wakakutana na ishu ya mauaji mengine ya mtoto wa mwanakijiji wakaachana na ishu ya mke wa mtu kubakwa , wakadili na mauaji, askari mwingine akatokea akawageuka katika hyo kesi kwa kuwa anajuana na wauaji na alishakula nao njama , inaendaaa inaendaaa mpaka inachosha hata kuangalia
NB:comment yangu haiusiani na tamthilia ya HUBA wala JUA KALI
 
Visa havina muunganiko, kijana kaiba boda boda, ambayo aliyeibiwa ni mtumishi nae mtumishi katembea na mke wa mtu, yule mke wa mtu ana tatizo la ugumba,kaenda kwa mganga akabakwa, polisi wakafatilia kabla hawajamkamata mganga wakakutana na ishu ya mauaji mengine ya mtoto wa mwanakijiji wakaachana na ishu ya mke wa mtu kubakwa , wakadili na mauaji, askari mwingine akatokea akawageuka katika hyo kesi kwa kuwa anajuana na wauaji na alishakula nao njama , inaendaaa inaendaaa mpaka inachosha hata kuangalia
NB:comment yangu haiusiani na tamthilia ya HUBA wala JUA KALI

Yàni ni kama mtunzi amechanganyikiwa
 
Yan bongo hamna kisa tofaut na mape z ,
Loloita -tofaut na kiss cha lolita visa vingine ni upuuzi tu , yan huyu kalala na huyu na huyu utafikiri hamna visa tofauti n mapenzi.
Kama utamruhusu mwanao aangalie kaza moyo - akija kuwa panyaroad au malaya usiseme kajifunzia wapi ww ndo umemfundisha

Alafu wanajificha kwenye kichaka kuwa soko ndio linataka hivyo wakati uwezo wao ndio umeishia hapo
 
Yani siku hz kuangalia tamthilia za kibongo ni ujinga kabisa..tamthili nzuri ambayo ilikua ina mafunzo ilikua ya KOMBOLELA na kidogo zahanati ya kijiji...ila zingine ni ujinga jinga tuu...kama hyo ya mtaa wa kaza moyo ni ushenzi mtupu..matusi yamejaa mle,uvutaji bangi,magenge ya kihuni..sijui kwakweli inafundisha nini...
Bora kuangalia documentaries
 
Back
Top Bottom