Tamko la Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislam Tanzania

Status
Not open for further replies.
Naomba mtu anifafanulie ni kwa vipi Uanzishwaji na uendeshwaji wa Mahakama za Kadhi unashabihiana kimuundo na kisheria na MoU katika baadhi ya hospital zilizo chini ya jumuia za kikristo nchini
 
Hospitali zinahudumia watu wote pamoja na wasio na dini.

Mahakama ya kadhi itahudumia waislam peke yake alafu mnataka kodi ya serikali(wakristo,waislam,wasio na dini,waabudu dini za bibi zao) pesa yao itumike kuwahudumie nyie waislam peke yenu. Huo ni utaahira.

Labda uniambie hizo hospitali huhudumia wakristo peke yake.
Hospital za misheni zinatoa huduma ya kulipia sio bure,ile ni biashara,na biashara haibagui mteja,as long as ana pesa ya kulipia huduma,kwanini serikali igharamike kuziendesha?
 
kwani mahakama zilizopo hazikidhi mahitaji yenu nyie ndugu zetu waislamu?????? na ni kwa kiwango gani hazikidhi hizo haja zenu????


Pia, hamuoni kama mtaleta unyanyasaji na ubaguzi katika nchi yetu????
 
Sis wakristo hatujakataa mahakama ya kadh. Ila anzishen ninyi wenyew waislam na muiendeshe ninyi wenyewe. Kwa nini mnatak serikali iingilie mambo yenu? Huku mkijua kuwa serikali haina din?

Vp na mapesa munayopewa na serikali kwA ajili ya kuendesha taasisi na mahospitali yenu? Apo serikali inayo dini?
 
Mahakama ya Kadhi haina mdhara kwa jamii ya Kitanzania. Kenya na Uganda wanayo na mambo yanakwenda swadakta tu.

Viongozi wetu wa dini wangetangiza uhalisia na uungwana badala ya Hulka na Assumptions.

Mh.Pinda alikuwa na nia njema kabisa juu ya mchakato huu. Lakini wachache tu ndio wanataka kufanya yakwao.

Watanzania wataikumbuka dhamira nzuri ya PINDA. Na tunapaswa kukumbuka kuwa, at the end of the time, hakuna mwenye uwezo wakuzuia matashi halisi ya Imani(ref.Kadhi's Court). Ni mahakama isiyo na shida kijamii.

Tuwe waungwana tu ktk hili.

nchi haina dini ila wananchi wake wanadini
 
kama kifo kingekuwa kinakatiwa rufaa, walah laadhim mimi ningeongoza ujumbe wa kwenda kwa Mungu ili amfufue Mwalimu Nyerere.

tunamhitaji Mwalimu (au wa aina yake) sasa kuliko wakati mwingine wowote. hivi vilivyopo kwenye madaraka sasa hivi vyote ni vitoto-vitoto tu. kwenye kucheka vinalia, kwenye kulia vinacheka.
 
Kama hauna uelewa juu ya hili bora utulie tu .....Mahaskofu wenyewe nikama nani nchini kujibu hoja za wengine.?
Tutaigawana nchi hii ka Sudan.
 
Naomba mtu anifafanulie ni kwa vipi Uanzishwaji na uendeshwaji wa Mahakama za Kadhi unashabihiana kimuundo na kisheria na MoU katika baadhi ya hospital zilizo chini ya jumuia za kikristo nchini
Ni kwasababu MOU si kwa ajili ya taasisi za imani moja tu.
 
Swala limepelekwa mahakamani na Mch.Mtikila..hivyo basi bunge halina uwezo tena wa kuupitisha huu muswaada.Tupo mahala pabaya..kila mmoja wetu kwa imani yake tumuombe MWENYEZIMUNGU atuvushe hapa.Tuache mzaha ktk jambo hili la imani.

Someone should have oppened a case against the Church to stop it to medle and interfere in Katiba process.
 
Profesa Lipumba aliunga mkono tamko la Maaskofu wa UKAWA,sasa aunge mkono na tamko hili la Masheikh ili akamilishe unafiki wake wa kuwafurahisha wanandoa wake Chadema

Kama kuna Maaskofu wa UKAWA vile vile wapo wa CCM. Ni nani hao? Ni Askofu mganga njaa MTETEMELA?
 
Kama unajua kutafakari uwezi kusema ivyo kwaiyo ccm itaongoza kwa sababu ya wana nchi? Au kwa sababu ya waislam tafakari kabla ya kuandika

Mkuu CCM inajua vyema kuzichanga karata........ fikiria zaidi hizi movie utaelewa tu, maaskofu wametoa tamko, pengo ka neutralize na ku confuse , waislam walijibu tamko, bakwata itakuja na lake, kisha watu wanupako na lao.....kisha serikali ita conclude.....na time inayoyoma bila kujadili mambo muhimu kuelekea oct 2015.
 
kwani mahakama zilizopo hazikidhi mahitaji yenu nyie ndugu zetu waislamu?????? na ni kwa kiwango gani hazikidhi hizo haja zenu????


Pia, hamuoni kama mtaleta unyanyasaji na ubaguzi katika nchi yetu????
Hazikithi,huko mahakama kuna sheria za kiislamu kuhusu mirathi na ndoa.

unakuta hakimu matayo ndo anahukumu mambo ya mirathi kwa sheria za kiislamu,haiji.
 
Hospital inahudumia wananchi kwa malipo,yet serikali ilipe wafanyakazi mshahara.

mahakama ya kadhi inahudumia waislamu ambao pia ni wananchi bure,kipi cha ajabu serikali ikilipa gharama za kuendesha?.
je mapato ya hospitali za misheni yanakwenda serikalini ama mifukoni mwa maaskofu?

Acha upuuzi, hebu nenda kwenye hizo hospitali kama hujakuta madokta waislam, ajira katika hizo hospitali hazibagui dini wala kabila kama ambavyo hakuna ubaguzi wa dini au kabila katika kuhudumia wagonjwa, je katika mahakama za kadhi itawezekana kupata kadhi mkristo ili kushughulikia matatizo ya waislam!!??
 
hili tamko tulilitegemea sasa ni mwendo wa matamko
Hili ligi kwa msaada na uratibu wa Jakaya Mrisho Kikwete.
Mradi wameliweka susla Mahakama ya Kadhi kama ajenda ya kisiasa, kwaheri umoja wa Watanzania.
 
Profesa Lipumba aliunga mkono tamko la Maaskofu wa UKAWA,sasa aunge mkono na tamko hili la Masheikh ili akamilishe unafiki wake wa kuwafurahisha wanandoa wake Chadema

Acha unafki wa kisho.. kama huitak serekal ya ccm kwann iliwaahid waislama? Mnafanya watu ni wajinga cku kikinuka ndo mnatafuta wachaw ni nani kumbe ni serekal hii dhaifu inaahid kitu ngumu kutekelexa


Jamani sijui hamuelewi.....HATUITAKI HYO MAHAKAMA. Anzisheni na muiendeshe wenyewe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom