WA-UKENYENGE
JF-Expert Member
- Oct 1, 2011
- 2,918
- 1,233
Nimeshasema hapa kwamba Serikali hii imejaa mataahira na ushahidi wa hili jinsi mambo yalivyo hivi sasa shaghala baghala. Rais wa nchi hata kusimama mbele ya Umma wa Watanzania kuongelea kuhusu hili swala la posho kunamshinda!!!! Swala muhimu kama hili anaongea kupitia kurugenzi yake ya Mawasiliano!!!!! Pia mgomo wa madakatari unaoendelea zaidi ya wiki sasa Rais wa nchi hajatia neno!!!! Huku Watanzania wakiendelea kufa na wengine kukosa huduma muhimu kwa matibabu mbali mbali wanayoyahitaji.
Kungekuwa na watu wenye akili timamu katika Serikali hii iliyopoa madarakani basi yote haya yangekuwa yameshazungumziwa kwa kinaga ubaga na kusingekuwa na utata wowote ule lakini kutokana na kujaa mataahira ndani ya Serikali hii kitu ambacho kimesababisha ombwe kubwa sana la uongozi nchini haijulikani nini kinachoendelea kuhusiana na mgomo wa madaktari na pia ongezeko la posho ya Wabunge. Wamethubutu wameweza na sasa wanasonga mbele!!!! Walidhani Urais ni lelemama na kuchekacheka!!!! Mungu inusuru nchi yetu.
Unajua mkuu, mimi huwa nashangaa hawa viongozi wetu wamefikaje hapo walipo? Je huko wanakopita, watu huwa wanasahauje hizi dharau? Au ndo mambo ya milungula ya kampeni watu hujisahau na kuanza kujipendekeza kwao na hatimaye kuwapa kura au kuwasaidia kuiba kura? Sioni tena maana ya kuwa na kiongozi ndani ya jamii zetu wakati hawajali!! Lakini yana mwisho, tutafika sehemu tutaanza kujichangulia hata magari yao ay nyumba zao. This is too much!!