Tamko la serikali kuhusu mgomo wa madktari

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
najua wengi wetu tunatamani kusikia tamko la serikali kuhusu mgomo wa madaktari.haieleweki kama serikali imewatimua madaktari waliogoma au la.haieleweki kama mgomo umekwisha au la.hatuelewi nini kinaendelea,je serikali imefanikiwa kudhibiti hali mbaya ya huduma kwenye mahospitali yaliyoko kwenye mgomo au la.pinda alisema tuvumilie sasa tunavumilia mpaka lini?mponda alisema yuko tayari kwa mazungumzo je madaktari wamekutana naye?ana makinda alisema tutarajie taarifa kutoka serikalini je tutasubiri mpaka lini?watanzania wanaendelea kufa au kuumia kwa kukosa huduma stahiki je tusubirie mpaka lini?tunawezaje kulazimisha tamko la serikali litoke ?je swala la mgomo wa madaktari sio kipaumbele kwa wabunge wetu?nahitaji tamko la serikali kama mwananchi niliyeathirika na mgomo huu.hatuwezi na kamwe tusikubali swala hili liende bila watu kuwajibika.mbunge wangu nifikishie ujumbe huu bungeni!wanajf na wananchi tushinikize kutolewa kwa tamko la serikali lenye muelekeo wa kuhitimisha mgogoro huu.
 
Ilikuwa mapema sana kwa serikali kutumia silaha kali na ya mwisho ya kutishia kufukuza kazi madkatari jumapili.
Matokeo yake ni total shutdown ya hospitali kama Muhimbili na MOI
 
jamani yaani hatuli tukashiba; madaktari madaktari, hatuogi tukatakata: mgomo mgomo, hatupigi stori tukacheka; pinda pinda. mbona serikali ilishatoa tamko lake siku ya Jumapili kuwa daktari ambaye ataendelea na mgomo ifikapo jumatatu (jana) ajihesabu kuwa hana kazi. tamko gani tena linatakiwa?
 
Ilikuwa mapema sana kwa serikali kutumia silaha kali na ya mwisho ya kutishia kufukuza kazi madkatari jumapili.
Matokeo yake ni total shutdown ya hospitali kama Muhimbili na MOI

naamini pinda alipotoshwa,tamko lile liliandaliwa na wizara ya afya.sio mbaya akijirudi na kutoa tamko lake halisi.na pia ni muhimu kuwawajibisha waliompotosha ambao ndio chanzo cha mgomo huu.
 
Wabunge wa upinzani kesho wambane bi mkora hii issue iwe discussed bungeni na akikataa wote watoke nje ya bunge na kuanza kuandaa maandamano ya wananchi kupinga ukimya wa serikali juu ya mauaji yanayoendelea!
 
Pia,
Tusitegemee tamko lolote kutoka kwa Pinda kuwa litakuwa hitimisho la mgogoro baina ya madaktari na serkali.
Rekodi yake ni safi. Hajawahi kusovu chochote tangu awe PM.
Hili tu keshalikoroga!
 
Ntafurahi kuskia tamko la serikali litakalohitimisha kwa Kumtimua Blandina Nyoni!
 
jamani yaani hatuli tukashiba; madaktari madaktari, hatuogi tukatakata: mgomo mgomo, hatupigi stori tukacheka; pinda pinda. mbona serikali ilishatoa tamko lake siku ya Jumapili kuwa daktari ambaye ataendelea na mgomo ifikapo jumatatu (jana) ajihesabu kuwa hana kazi. tamko gani tena linatakiwa?
mkuu,huwezi kula kwa raha wakati watu wanataabika na kufa.kama madaktari wale wamejifukuzisha kazi basi tusikie mbadala wa madaktari hao na sio wanajeshi 15 ambao hawajatosheleza mahitaji.wewe hutaki kusikia tathmini ya athari za mgomo?hutaki kusikia waliosababisha mgomo wamewajibika vipi?tuwe serious kidogo hata kama hatujazoea,hii sio richmond wala dowans!people are suffering!
 
Wabunge wa upinzani kesho wambane bi mkora hii issue iwe discussed bungeni na akikataa wote watoke nje ya bunge na kuanza kuandaa maandamano ya wananchi kupinga ukimya wa serikali juu ya mauaji yanayoendelea!
nakubaliana na wewe,kama tulitoka bungeni kupinga matokeo ya urais na muswada mbaya wa katiba sioni kwa nini tusidemonstrate kupinga wagonjwa kutaabika au kufa.
 
naamini pinda alipotoshwa,tamko lile liliandaliwa na wizara ya afya.sio mbaya akijirudi na kutoa tamko lake halisi.na pia ni muhimu kuwawajibisha waliompotosha ambao ndio chanzo cha mgomo huu.
Acha unafiki bana,
Kupotoshwa? My underwear!
Mgogoro umedumu zaidi ya wiki tatu tangu madaktari interns walipoacha kazi kudai malipo yao.
Attempts zimefanyika nyingi za kuwasiliana na waziri mkuu na chama cha madaktari (MAT).
Hadi MAT wakaenda ofisini kwake na kagoma kuongea nao akawasakizia na secretari wake.
Mgomo ukaitishwa rasmi na ukadumu siku sita hali akijua madaktari wanamtaka wamalize mgogoro.
Ana vyombo vya usalama vinampelekea taarifa hata kama viongozi wa wizara ya afya wangem-disinform.
Alikuwa akijua yote na kuamua jinsi tulivoona.
Tusimtetee kuwa kapotoshwa.
Mkapa kakaa ikulu miaka 10 hatujawahi kusikia kapotoshwa.
kila leo JK kapotoshwa, Pinda kapotoshwa!
ehe! Potoshapotosha syndrome!
 
I dont expect anything good from this country espeially from my lazy crazy government, The PM is on top bt infinite times he did so many blunders in his carrier. He is totally failure figure in the gava.
 
kwa style hii ya kushushuana unaweza kuta PINDA kaulizwa nani alikwambia utoe hilo Tamko?? eheee?
 
mbona kamati ya madaktari inayoratibu mgomo huu intoa taarifa mara kwa mara?iweje serikali ikae kimya?wabunge kama kweli mnawakilisha wananchi na kama kweli sis tuliwachagua basi hakuna budi kuwakilisha mawazo yetu.
MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI CHA LEO
Kutokana Na Serikali Kuendelea Kuwa Kimya Kuhusu Madai Yetu, Kamati Imeazimia Yafuatayo
1. Kuendelea Na Msimamo Uleule, Na Kukaza Kamba Zaidi (Ombi Tunaomba Tupeane Moyo Na Kushikana Mikono Hata Kuinua Wale Waliodondoka)
2. Kwa Sasa Juhudi Zote Za Kutafuta Suluhisho La Mgogoro Huu Na Jitihada Zote Zinaelekezwa Ofisi Ya Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, Ili Kuweza Kutatua Haraka Nasi Kuweza Kurudi Kutoa Huduma Yetu Muhimu Kwa Wananchi.
3. Utaratibu Wa Kuonana Unaandaliwa Tujiandae Pale Tutapofahamishwa.
... 4. Kuendelea na utaratibu wa kukutana wachache wachache pale inapobidi.
Mwisho Kamati Inatoa Shukrani Kwa Wapambanaji Wote Na Tuendelee Kushikamana. Pongezi Kwa Hospitali Zote Zilizosimama Mpaka Sasa Hivi (Mnh, Amana, Tmk*, Mwananyamala, Kcmc, Bmc, Mbeya, Ifakara, Morogoro*, Bombo*)
Shukrani za pekee ziende kwa madaktari bingwa wa hospitali ya Muhimbili kwa kuonyesha njia kwa maazimio yao (kukubali madai yetu kuwa ni ya msingi, Majibu ya Mhe. Waziri Mkuu hayakujitosheleza kujibu hoja licha ya kujaa vitisho, kuendelea na huduma za dharura tu na kuipa serikali masaa 48 kuumaliza mgogoro huu, na way forward waliyoamua ni kuunda kamati itayowasilisha maoni na maazimio yao kwa Mhe. Rais.
N.B: Licha ya kuishukuru kamati inaangalia uwezekano wa kuonana nayo ili kuweka sawa baadhi ya maazimio yao, tunatarajia ushirikiano wao.
Pia shukrani kwa Residents wa KCMC kwa kujiunga na kuongeza nguvu.
TAARIFA;
Leo saa 12.30 jioni kutakuwa na kipindi cha majadiliano cha BBC ambacho Mada itakuwa ni kuhusu migomo ya watumishi wa Afya, itaongozwa na Waziri Hamsini na waalikwa ni Dr. Namala Mkopi (Tz), Mwakilishi wa Wizara (?) (Tz) na Mwenyekiti wa KMPDWU (Kenya). Mnakaribishwa kusikiliza na kuchangia.
Tunashukuru kwa Ushiriakiano wa kila mmoja wenu.
Imeandaliwa na Kamati ya Jumuiya ya Madaktari.
 
unaota ndoto ya tamko la nini..... ili muanze kulinanga si bora lisitoke tu tuendelee kubishana bila majibu
 
kwa style hii ya kushushuana unaweza kuta PINDA kaulizwa nani alikwambia utoe hilo Tamko?? eheee?
Kwani hawajaanza?
Tayari Mkurugenzi wa Muhimbili keshatupiwa zigo kuwa ndo chanzo cha yote kwa kitendo cha kuwaandikia barua intern doctors kuwarejesha wizarani.
Haijulikani ilikuwa ni initiative yake au maelekezo!
 
jamani yaani hatuli tukashiba; madaktari madaktari, hatuogi tukatakata: mgomo mgomo, hatupigi stori tukacheka; pinda pinda. mbona serikali ilishatoa tamko lake siku ya Jumapili kuwa daktari ambaye ataendelea na mgomo ifikapo jumatatu (jana) ajihesabu kuwa hana kazi. tamko gani tena linatakiwa?

Ushibe mara ngapi?! Mbona mtumbo umekuvimba kama furushi kinyesi.
 
Mbona mimi sielewi? ni tamko gani tena linalotakiwa? kinachoendelea sasa ni kupokea majina ya madaktari ambao hadi sasa bado wako kwenye mgomo na orodha ikikamilika ni kuwatimua kwa majina.... hadi wakamilishe mikoa yote itachukua muda kidogo!
 
Back
Top Bottom