Tamko la madaktari bingwa MNH, MUHAS na ORCI

hii move inaelekea kubaya sana usikivu wa serilkali upo wapi? mkuu wa nchi hajui aseme nini tulipoambiwa hafai tulishupaza shingo zetu

Mkuu wa nchi anatafuta hawezi kuwa na la kusema, maana move kama hizi huzisema kupitia wazee fulani fulani (akina Iddi Simba - yupo rumande, na wazee wengine hasa wa Dar wameisha mstukia Mkuu, nasikia yupo Dodoma labda anataka kuwatumia hao, ila bado mkuu anatafuta ni wazee wa mji gani na wa aina gani atawatumia kulihutubia taifa kupitia wao. Let's wait
 
vipi comrade hawezi kuwatumia wazee wa Mbeya maana ndiko anakotokea mwenyekiti wa madaktari mshauri aende mbeya Comrade
 
".....Na njia nyingine zote za uchangiaji pesa zimesitishwa na kupendekeza zitumike namba za mawakala zifuatazo Voda 31915 na Tigo 05416......"

hapo kwenye blue:

Nauliza pia natoa ushauri:
1. kama njia zote zimesitishwa na kupendekeza kutumia hizo namba za mawakala ( Voda 31915 na
Tigo 05416)
, kwanza nani kasitisha hizo njia za uchangishaji? serikali au nani?
2. Kama Serikali ndio imezuia hizo njia za awali, hivi hizi za mawakala haziwezi zuiwa pia?
3. Hawa mawakala tunaochangia sasa, ni reliable, siyo tunaweka then anagoma kuzitoa?
Ushauri: Kwanini tusipewe akaunti namba ya one of the Doctors, au hata akaunti ya MAT au jumuiya ya madakari tukaweka huko michango yetu direct? Doubt yangu, ni kuwa hapa Jamvini kila mtu anakuja na lake, so inawezekana hii source sio reliable (unless) kama wanaJF mnaweza prove kuwa hii source ipo ok, na hizo namba za mawakala ni sahihi.
Ila bado nahamasisha na kukubaliana kuwa michango iendelee kuchangisha ili dr. apate matibabu sahihi

Get well soon Dr. Ulimboka
 
Hii ndio kitu nisichokubaliana nacho kabisa!.. Sasa hawa madaktari wanapogoma ndio kusema Dr.Ulimboka kapigwa na wananchi kiasi kwamba wao ndio wachukue adhabu hii?

Halafu wanaombwa wananchi wale wale waliadhibiwa kuchangia tiba ya Ulimboka wakati wengine tuna wagonjwa wanaotaka huduma tu wapone lakini wanatufia mkononi kwa sababu ya mgomo huu..Nawaomba Madaktari iadhibuni serikali na sii wananchi walipa kodi ambao hawana makosa kabisa.

TUCTA wametoa kauli na wito kwamba swala hili litafikishwa ktk vyombo vya kimataifa, na hatuelewi mazungumzo baina ya serikali na shirikisho la madaktari limeenda vipi au wamekwama wapi..

Tunaona migomo hadi Bugando na Hospital za makanisa halafu tukisema mfumo mbaya na wapi penye mapungufu watu wanakuja juu kutetea kanisa ilihali vyombo hivi havifanyi kazi inavyohitajika.

Kazi kusubiri fedha za donors na misamaha wajirushe kwa sifa ya huduma ambayo haitusaidii wananchi ktk kupunguza gharama za Afya na sasa ndio hatutibiwi kabisaa wakati kodi zetu wanakula.

Kinachofanywa na madaktari hakina tofauti na UAMSHO, wao wanaona kila haki ya kuchoma makanisa au kugoma lakini wanashindwa kuidhibu serikali yenyewe. Kesho ukisikia Sheikh mkubwa wa UAMSHO kafanyiziwa, utawasikia Wazanzibar na Waislaam wakilaani Wakristu na serikali lakini hawapimi kitendo cha kuchoma makanisa yasiyohusika na mgogoro ndio unafiki ulipoanzia. Vitendo vyetu sisi wenyewe ktk kuwaadhibu wananchi ndivyo vinavyozidi kutugawa.

Sioni sababu ya madaktari kugoma pasipo kuwashirikisha wananchi, kulifanya swala hili ni lao wao wenyewe kwa kuwasulubu wananchi ii kuikomoa serikali.. Watu wanakufa jamani, muwe na huruma japo kidogo wakati tunaitafuta suluhu.

TUCTA wamesema watalipeleka swala hili ktk vyombo vya kimataifa, muda wote kwa nini wasihusishwe mapema tukatafuta suluhu badala ya kuwaadhibu wananchi?..
I used to think you are one of the great thinkers..lkn sasa naona udini unaanza kuathiri uwezo wako wa kufikiri.
 
Hukumu ya Dhambi ya taifa anadhibiwa kila mtu mwenye makosa na asiye na makosa.
Wananchi wengi wanaiunga mkono serikali ya CCM na hawana matatizo nayo

Iddi Amini alipoivamia Tanzania 1978 vita ilipoingia ndani ya Uganda hawakufa watumishi wa serikali yake walikufa wananchi wa Uganda.

Udhaifu wa serikali ya Kikwete wa kuendelea kuruhusu wizi na ubadhirifu mkubwa katika sekta zote serikali ndiyo asili ya mgomo huu. Sisi wananchi tumeshindwa kuibana serikali katika udhaifu wake, chochote kinacho tokea kwa sababu ya udhaifu wa serikali ni wazi kabisa wa kuumia ni sisi wananchi.

Ni kazi ya kila mwananchi kutumia haki yake ya uraia kuibana serikali dhaifu na hata ikibidi kuiondoa madarakani.
Kazi ya kulinda Uhuru wa nchi kwa asilimia 90 haina uhusiano na Jeshi wala bunduki, ina uhusiano na harakati za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kama sisi wananchi tnasubiri viongozi wa serikali dhaifu au juuia fulani ya kimataifa iwakoromee akina Kikwete huo utakuwa ni Udhaifu kuliko ule wa kikwete mwenyewe na nina uhakika wa 100% tutaendelea kula chungu ya ghadhabu ya utawala wa CCM mpaka kila mtu afikwe na kiama.

Hii ndio kitu nisichokubaliana nacho kabisa!.. Sasa hawa madaktari wanapogoma ndio kusema Dr.Ulimboka kapigwa na wananchi kiasi kwamba wao ndio wachukue adhabu hii?

Halafu wanaombwa wananchi wale wale waliadhibiwa kuchangia tiba ya Ulimboka wakati wengine tuna wagonjwa wanaotaka huduma tu wapone lakini wanatufia mkononi kwa sababu ya mgomo huu..Nawaomba Madaktari iadhibuni serikali na sii wananchi walipa kodi ambao hawana makosa kabisa.

TUCTA wametoa kauli na wito kwamba swala hili litafikishwa ktk vyombo vya kimataifa, na hatuelewi mazungumzo baina ya serikali na shirikisho la madaktari limeenda vipi au wamekwama wapi..

Tunaona migomo hadi Bugando na Hospital za makanisa halafu tukisema mfumo mbaya na wapi penye mapungufu watu wanakuja juu kutetea kanisa ilihali vyombo hivi havifanyi kazi inavyohitajika.

Kazi kusubiri fedha za donors na misamaha wajirushe kwa sifa ya huduma ambayo haitusaidii wananchi ktk kupunguza gharama za Afya na sasa ndio hatutibiwi kabisaa wakati kodi zetu wanakula.

Kinachofanywa na madaktari hakina tofauti na UAMSHO, wao wanaona kila haki ya kuchoma makanisa au kugoma lakini wanashindwa kuidhibu serikali yenyewe. Kesho ukisikia Sheikh mkubwa wa UAMSHO kafanyiziwa, utawasikia Wazanzibar na Waislaam wakilaani Wakristu na serikali lakini hawapimi kitendo cha kuchoma makanisa yasiyohusika na mgogoro ndio unafiki ulipoanzia. Vitendo vyetu sisi wenyewe ktk kuwaadhibu wananchi ndivyo vinavyozidi kutugawa.

Sioni sababu ya madaktari kugoma pasipo kuwashirikisha wananchi
, ( ina maana sisi wananchi hatuoni hali ilivyo mbaya pale muhimbili Amana na Mwananyamala mpaka tuletewe maombi ya kujiunga kwenye mgomo???)kulifanya swala hili ni lao wao wenyewe kwa kuwasulubu wananchi ii kuikomoa serikali.. Watu wanakufa jamani, muwe na huruma japo kidogo wakati tunaitafuta suluhu.

TUCTA wamesema watalipeleka swala hili ktk vyombo vya kimataifa, muda wote kwa nini wasihusishwe mapema tukatafuta suluhu badala ya kuwaadhibu wananchi?..
 
Kwakua mmeshika makali naona mmeamua kutuua watanzania kwa kosa la serikali,ni vyema mngetafuta namna ya kuibinya serikali ili iwasikie vinginevyo mlaaaniwe kwa roho zote za watanzania zinazo potea ambazo labda uhai wao usingetoka kama zingepata huduma yenu!
 
Hukumu ya Dhambi ya taifa anadhibiwa kila mtu mwenye makosa na asiye na makosa.
Wananchi wengi wanaiunga mkono serikali ya CCM na hawana matatizo nayo

Iddi Amini alipoivamia Tanzania 1978 vita ilipoingia ndani ya Uganda hawakufa watumishi wa serikali yake walikufa wananchi wa Uganda.

Udhaifu wa serikali ya Kikwete wa kuendelea kuruhusu wizi na ubadhirifu mkubwa katika sekta zote serikali ndiyo asili ya mgomo huu. Sisi wananchi tumeshindwa kuibana serikali katika udhaifu wake, chochote kinacho tokea kwa sababu ya udhaifu wa serikali ni wazi kabisa wa kuumia ni sisi wananchi.

Ni kazi ya kila mwananchi kutumia haki yake ya uraia kuibana serikali dhaifu na hata ikibidi kuiondoa madarakani.
Kazi ya kulinda Uhuru wa nchi kwa asilimia 90 haina uhusiano na Jeshi wala bunduki, ina uhusiano na harakati za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kama sisi wananchi tnasubiri viongozi wa serikali dhaifu au juuia fulani ya kimataifa iwakoromee akina Kikwete huo utakuwa ni Udhaifu kuliko ule wa kikwete mwenyewe na nina uhakika wa 100% tutaendelea kula chungu ya ghadhabu ya utawala wa CCM mpaka kila mtu afikwe na kiama.

Lakini hatahivyo ukiangalia kwa undani wakuadhibiwa pengine ni sawa, yani ya kwamba kama serikali inawadhibu madaktari basi nao madaktari wana wa adhibu waliowaweka madarakani yani wananchi.

Wenye makosa na wanaopaswa kuadhibiwa si wanasiasa bali wananchi ili wajifunze kuacha kupokea kitu kidogo na wafanye maamuzi sahihi
 
".....Na njia nyingine zote za uchangiaji pesa zimesitishwa na kupendekeza zitumike namba za mawakala zifuatazo Voda 31915 na Tigo 05416......"

hapo kwenye blue:
" Fishy". Hii ina harufu ya samaki....au...!
 
Wakuu sote tukubali kuwa daktari na mwalimu si mtu wa kuchezewa. Kwa mantiki hii serikali ilitakiwa ilione hilo na kukaa chini kupata muafaka. Ikumbukwe kuwa health workforce shortage ni critical Tanzania. Uwezo wa kukodi madaktari nje ni ndoto na kuwafuta ni usingizi na kifo kwa mtanzania ambaye hana uwezo wa kutibiwa private na nje ya nchi. Kama kweli wabunge wanapenda wapiga kura wangegomea vikao vya bunge. Au tuseme ni kwa kuwa
Wamo ktk huduma ya matibabu nje na piano kugoma ni kupoteza sitting allowance? so astonished!

ni critically
 
Nimepitapita kwenye michango mingi ya wadau nimeoana kuna baadhi yetu wanawalaumu madaktari kugoma kwa sababu wanasababisha vifo vya wananchi wasio na hatia. Kuna wengine wameenda mbele na kudai kwamba kama Madaktari wamegoma kwa nini hawajagoma kumtibu Kamanda Ulimboka?!

Hoja zote mbili ni kielelezo cha uwepo wa fikra za ujima (duni) miongoni mwetu. Niseme tu kwamba katika harakati za kutafuta haki na usawa swala la damu kumwagika, vifo na vilema ni vitu visivyokwepeka. Si jambo la ajabu ikiwa baadhi yetu watapoteza maisha au watapata vilema kwa ajili ya kuokoa maisha ya vizazi vyetu vijazo. Ni fikra dhaifu sana kusema Madaktari wasigome kwa sababu tutakufa sisi wananchi wa kawaida. Swali la kujiuliza wasipogoma hatutakufa? Je madawa yatakuwepo Hospitalini? Vitanda vitakuwepo? Au ni sifa Mgonjwa kufia mikononi mwa Daktari asiye na Panadol?

Hata hivyo, jambo muhimu tunalopaswa kukumbukwa ni kwamba wakati wa Vita ya Chief Mkwawa na Wajerumani wananchi wengi walikufa ambao hawakuwa na hatia. Nani anakataa kwamba vifo vyao ndiyo Uhuru na uhai wetu sisi leo? Kupoteza uhai wa sehemu ya kizazi cha sasa kwa ajili ya hifadhi ya Uhai wa Watoto na Wajukuu wetu ni jambo ambalo haliepukiki. Vinginevyo tukubali kwamba hatuelewi falsafa ya harakati na ukombozi.

TUMBIRI (PhD, University of Hull - UK),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Siwaungi mkono hata kidogo, mtatuua jamani. Daini maslahi yenu kwa njia nyingine not at the expense of we the poor!
 
Madaktari wanatakiwa wajitahidi sana kuwasilisha vilio vyao kwenye vyombo vya kimataifa mfano UN, Amnesty International, ICC n.k tena haraka, vinginevyo wataokotwa wengi kwenye msitu wa Mabwepande.

nao mbona wanaua wananchi maskini.
 
Hizo ndo hatua za wanaume, big up nawapongeza kwani inaweza kuwa chachu ya ukombozi wa nchi hii, damu ya dr ulimboka ni sawa ya jesus haitapotea bure, kwani naamini kuwa ukombozi halizi huja kwa kumwaga damu. Mungu akupe afya njema pamoja na juhudu za madaktari wenzako. Nashauri madaktari wote hata wasio maspecialist wagome pia kuunganisha nguvu,

Ni kweli tuko pamoja tuombe wananchi wachangie vya kutosha ili hili jukumu la matibabu lishughulikiwe na madaktari pekee kuliko kutegemea fedha kutoka sirikalini kwani wataenda kummalizia hukohuko. Hawa ni wauji.
 
Kiongozi, umeongea jambo la kugusa sana, hasa wakati huu ambao nchi iko ktk majaribu makubwa.Ni kweli kabisa kugoma kwa madaktari kunapelekea kupotea kwa uhai wa walio wengi, hili liko wazi na inauma sana. Lakini kwa upande mwingine turudi nyuma. Hata kabla hawajagoma, hali ilikwisha kuwa mbaya kitambo. kwa wale mlioko humu ndani ambao huwa mnapata muda walau wa kutembelea baadhi ya hospitali kuwajulia hali wagonjwa bila shaka mtalizungumzia hili KUTOKA MIOYONI MWENU bila kutia unafki wowote. Ni nani asiyejua kuwa hali ya afya ni mbaya hapa nchini? wapo wagonjwa wengi waliopoteza maisha yao kwa kukosa dawa za kuwatibu, wapo waliokufa kwa sababu ya kukosa vifaa maalum za kuwafanyia upasuaji. Ukienda mbali zaidi na kuangalia suala la nishati, je ni wagonjwa wangapi wamepoteza maisha kwa sababu ya kukosa oksijeni walizokuwa wakizipata kutoka mashine maalum za kutoa hewa ya oksijen. Mashine hizo huendeshwa na umeme wa grid ya taifa au jenereta lakini kwa kuwa nishati si ya kudumu, wengi wamepoteza maisha kwa namna hiyo.

Ni wangapi wenu waliwahi ugua wakaenda hospitali za serikali? kwa kuwa muungwana kabisa, ilikuchukuwa muda gani kupatiwa matibabu? kwa namna hii ni wangapi wanafia ktk foleni za kusubiri matibabu? Mimi binafsi niliwahi ugua nikaenda hospitali ya mwananyamala-kiukweli kwa foleni iliyokuwa siku ile ilinichukua masaa sita hadi kuja kupata matibabu.Ulishawahi kupita kwenye wodi za watoto na wazazi/akina mama. Naomba mlioko huku msiongelee ushabiki au hisia ila tujaribu kwenda kwenye uhalisia kabisa wa maisha na uangalie kama unaguswa na mateso wapatayo wagonjwa kwa kukosa hayo niliyotaja hapo juu. Je Mna habari kuwa wagonjwa wengi sana wanalala chini kwa kukosa vitanda? Wengi wanalundikwa chumba kimoja au wanalala kitandani wawili wawili-hii hupelekea kupata maambukizi zaidi-kama ulishawahi kuona na kuguswa na hili hutaongea kwa ushabiki wala hisia.

Singeshangaa kama tumekuwa hivi kwa kukosa utajiri na rasilimali za kutosha. Hakika Mungu ametupa kila kitu tunachokitaka kwa maisha lakini kwa wachache wengi wanateseka tena sana--Hadi lini? Kwa wale wanaosoma historia, hata akina Mkwawa walipingwa na watu wao wenyewe kwa kutaka kuleta mapinduzi lakini haohao na vizazi vyao hadi leo wanafurahia matunda na sadaka waliojitoa akina Mkwawa, Mandela nk. Mbaya zaidi, hakuna kiongozi wa serikali anayeugua na kutibiwa ktk hospitali hizi pengine hata na familia zao. kwa mawazo yako wewe uliye jamvini, unafikiri ni nani wa kuboresha hizi hospitali? ni sisi walalahoi tunaotibiwa humo au hao viongozi wanaokwenda tibiwa nje? Kama utajibu kuwa ni viongozi basi nawe utakuwa upande wao bila shaka. Sisi wananchi ndio MABOSI wa nchi hii na sisi TUMEWAAJIRI WAO. ni lazima wala sio ombi, serikali wakatekeleza yale ambayo wanapaswa kutekeleza kwa maslahi, neema, afya, usalama, na maendeleo ya nchi yetu.

Ni wazi kuwa tuliyemwajiri ametuangusha kwa muda mrefu na kutudhoofisha sana. Je kuna ubaya gani BOSI akitaka kumrekebisha aliyemwajiri ili mambo yaende sawa? Lakini cha ajabu kwa watanzania walio wengi ni kama vile serikali ndio bosi wetu la hasha, Hebu tuamke wadau na tuungane ktk kuweka mazingira ya kuinusuru nchi yetu na hali mbaya tuliyonayo...

NAUNGA MKONO MGOMO KWA NIA NJEMA YA KULETA MABADILIKO YA KWELI NA SI VINGINEVYO.
 
Siwaungi mkono hata kidogo, mtatuua jamani. Daini maslahi yenu kwa njia nyingine not at the expense of we the poor!

Wameshajaribu hizo njia nyingine kitambo na hakuna aliyewasikiliza, hebu tuambie hizo ulizonazo ni zipi mbali na kukaa mezani na serikali na kupewa ahadi hewa. Mimi nimesoma ktk sekondari ya bodi. kwa sifa nyingi ya shule hizi wanafunzi mara nyingi hupikiwa chakula kibovu, mimi binafsi yalishanikuta. Sikudanganyi kwa uzoefu mdogo sana nilionao, ukidai haki yako kwa kuwasilisha tu malalamiko alafu ukaendelea kukitumia kile ambacho unadai kifanyiwe marekebisho, ni vigumu kupata hiyo haki. Njia pekee ambayo ilikuwa inatusaidia kuleta mabadiliko ni kugomea kula hicho chakula na kwa njia hii tulikuwa tunafanikiwa, japo si rahisi kwani iligarimu wengine kufukuzwa au kupewa suspension nk. Kwa mawazo yangu nafikiri this rule applies almost in any system in the world regardless how big or small it is. Migomo na maandamano ndio njia nzuri na ya amani zaidi ya kudai haki. TUWAPE MADAKTARI SUPPORT KWA NIA YA KULETA MABADILIKO KATIKA SEKTA YA AFYA.
 
Back
Top Bottom