Tamko la Kamati Kuu ya CCM; Muda waongezwa kujivua gamba

Hapa sasa ndo kifo cha magamba make Nape ajiandae kujibu maswali magumu juu ya mapacha wa3,huyu Vasco kweli ni 'changanya za kwako',sasa balaza la mawazili ni ccm tupu walipokaa wakaona mafuta ya taa yapande bei,leo kwenye cc anawaongoza wenzie waseme mafuta ya taa yashushwe bei,sasa sijuhi huku alimwogopa nani kubadilika hivi ama anaonesha uzuzu wa cabinet yake kwamba hawakumshauri rais wao?

a contradicting decision,na ndo maana hata mawaziri wake hawamwelewi kwa maana anakaa nao wanaelewana hivi alafu akienda huku anaongea vinginevyo,kumbe yeye ndo chanzo namba1 cha serikali yake kupwaya hivi na hata kama ni hujuma yeye ndo anajihumu,maamuzi ya hivi nayakumbuka kama ile ishu ya bomoabomoa pale Ubungo,uzinduzi hoteli pale Arusha n.k

Nalazimika kukiri kwamba kwa stairi hii si ajabu hii nchi yetu ikawa imeuzwa kiasi ambacho hatujajua na tukija kujua tutakuja kujuta na tutalia sana!
 
jana nimechelewa kulala kwa sababu ya upuuzi huu? let them findw another way 2 convice me.
 
"Aidha Kamati Kuu imejadili masuala mengine kama; migogoro ya ardhi, tatizo la bei ya pamba, tatizo la uuzaji wa mahindi, migogoro migodini, masuala yanayohusu kero za Muungano na kuagiza Serikali kuyashughulikia kwani yanatatulika"

wametoa maamuzi gani kuhusiana na waziri mkuu mizengo Pinda kujihusisha na migogoro ya ardhi na haswa suala la ekari zaidi ya laki tatu kule mpanda Agrosol ? kuna haja ya kuwatazama hawa jamaa wanaongea kama vile wanaagiza serikali inayotawaliwa na CDM na sio wao , huwa hawajui kinachoendelea?
 
Wadau mimi nakuja na off point, hivi Dodoma kuna baridi hivyo!. Nape kavaa shati, sweta na koti juu wakati anatoa taarifa ya kikao cha CC.
 
Mimi siwaelewi hawa jamaa wanapolalamika kana kwamba wao ni chama cha upinzani

ila malalamiko haya yanalipa nguvu suala la kutenganisha kofia ya mwenyekiti wa chama na rais vinginevyo inakuwa ngumu sana mwenyekiti kusimamia matakwa mawili yanayopingana kwa vile yeye pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri wanaopitisha miswada yote likiwemo la kupanda bei mafuta ya taa.

Lowassa for chairman.
 
NI HAPA HAPA. Wadau walisema hatoki hata mmoja sass RA Katoka mmeanza mara ooh hamuwawezi mara pooh wamekwama,,,lipi Jena KWENU? Mnakuwa Kama hula mnapata perio....ikifika LAZIMA kuziba ikiisha eehee
 
halaf nape hiyo midomo mbona myeusi sana?...unakula ganja nini mkuu?....

tamko lenyewe dizaain kama la ki-ganja ganja
 
Naomba comments za watu wafuatao;
1. Nnauye jr
2. Faiza Foxy
3. Jenifa
4. Mzee wa hoja
5. W. J. Malecela
6. Omr
7. Mr Mak
8. Muhadhir
9. Rejao
10. Nduka

Ahsanteni sana...
 
sasa ajiite nani na yeye kazi yake ndo kueneza huo ukilaza wa chama chake? unamuonea mtoto wa watu,lol

yaani pamoja na kuamuru simu za wajumbe wa CC kuzimwa ndiyo mnakuja na hii "soft statement" ? kweli magamba vilaza. Halafu unajiita katibu mwenezi, duuuh!
 
chama chenu kwa kusikitika! hawa wajumbe wa nec wengi wao si wabunge? na wanaunga mkono hoja kila siku? masikitiko sana yanaweza kuleta msongo wa mawazo,tafuteni suluhisho basi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
5. Kamati Kuu inasikitishwa na tatizo la umeme nchini kwani athari zake kwa uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja ni kubwa. Hivyo basi imeitaka Serikali kutumia muda iliyopewa wa kurekebisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kuja na mpango wa dharura wa kunusuru hali hii na kisha kulimaliza kabisa tatizo la umeme nchini.
Nape M. Nnauye (MNEC)
KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI
DODOMA
1/8/2011
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imemaliza kikao chake cha siku moja usiku wa tarehe 31/07/2011 mjini Dodoma chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeamua yafuatayo;

1. Imefanya uteuzi wa makatibu ishirini na saba (27) kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika wilaya hizo. (majina na wilaya zao yameambatanishwa). Pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu imetengua uteuzi wa Makatibu wa Wilaya watatu (3) katika kuboresha ufanisi wa kazi katika wilaya hizo.(majina na wilaya zao yameambatanishwa).


2. Kamati Kuu imepokea na kuridhia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuwakilisha Mkoa wa Tabora, Ndugu Rostam Aziz. Aidha imempongeza kwa uamuzi huo uliozingatia maslahi mapana ya chama chake.

3. Kamati Kuu imepokea pia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Ndugu Rostam Aziz na kuagiza chama kupanga ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga itakayozingatia ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya uteuzi wa mgombea.
Aidha Kamati Kuu imeagiza shughuli zote za kampeni kutafanywa na CCM Mkoa, Wilaya na ngazi zote za chama wilayani Igunga. CCM Taifa watashiriki kuongeza nguvu. Chama kinatoa wito kwa wana CCM, wapenzi na wakereketwa wa chama chetu kushiriki kwa pamoja kuhakikisha jimbo linabaki kwa CCM.

4. Kamati Kuu haijaridhishwa na kiwango cha bei ya mafuta ya taa nchini kwa kuwa ndio nishati inayotumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini. Aidha Kamati Kuu haikuridhishwa na maelezo ya kupandishwa kwa bei ya mafuta hayo kwa kisingizo cha kuzuia uchakachuaji wa mafuta mengine. Hivyo basi, Kamati Kuu imeiagiza Serikali kutafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa na kuvitaka vyombo vya Serikali vinavyohusika na usimamiaji wa ubora wa mafuta, vihakikishe vinatimiza wajibu wake kuzuia kabisa mtindo wa uchakachuaji wa mafuta nchini na si kupandisha bei ya mafuta ya taa kama suluhisho.

5. Kamati Kuu inasikitishwa na tatizo la umeme nchini kwani athari zake kwa uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja ni kubwa. Hivyo basi imeitaka Serikali kutumia muda iliyopewa wa kurekebisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kuja na mpango wa dharura wa kunusuru hali hii na kisha kulimaliza kabisa tatizo la umeme nchini.

6. Aidha Kamati Kuu imejadili masuala mengine kama; migogoro ya ardhi, tatizo la bei ya pamba, tatizo la uuzaji wa mahindi, migogoro migodini, masuala yanayohusu kero za Muungano na kuagiza Serikali kuyashughulikia kwani yanatatulika.

7. Kamati Kuu imeipongeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kazi nzuri ya kutekeleza maamuzi ya NEC na kuitaka iongeze kasi katika utekelezaji huo, ili kuhakikisha mageuzi yaliyokusudiwa yanatekelezwa kwa wakati. Aidha imejadili na kupitisha miundo mipya ya Idara ya Itikadi na Uenezi na Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

8. Kuhusu suala la maadili ndani ya Chama, Chama kinaendelea kusimamia maadili, na kuwataka wale waliotakiwa kujipima na kuwajibika watumie muda huo, kujipima na kuwajibika kwa masilahi mapana ya chama.
Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inatarajiwa kukutana wakati wowote mwezi Septemba, ambapo pamoja na mambo mengine itatathimini utekelezaji wa maamuzi yake. Imetolewa na:-


Nape M. Nnauye (MNEC)

KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI
DODOMA
1/8/2011
9. kadhalika kamati inasikitishwa na ulegelege wa mwenyekiti wa chama, na kuwa inatafakari kufanya maamuzi magumu juu yake..
10. endeleza hapo
 
Magamba alikuwa rostam sasa chama kiko shwari na hakuna tena siasa za kuvuana magamba big up ccm mnatisha el na ec wako gaadooo imaraaa el atakaposhinda uchaguzi 2015 atamteua ec kuwa pm
 
Hakuna jipya!!hawa jamaa wamepoteza mwelekeo.gamba la lowasa si mchezo kulivua manake si la nyoka ni la mamba.
 
CCM is feable enough not to take any firm ACTION!!

Yes ...Feable and very weak to cause anymeangiful CHANGER to this nation ...

Kumbukeni Mfano wa Babu na Kinyonga ...the only way out!!

Gamba gamba ...Lilipi?
 
Loh yamekuwa hayo, ama kweli Magamba si chama kile enzi zile, ikiwa wanaweza kuwa mstari wa mbele kuwakolimba walio safi kivipi wanashindwa kuwakolimba EL na AC "Lo..kazi ni kwako!
<br />
<br />


Mzimu wa korimba unakikorimba chama cha magamba sasa.
 
NI HAPA HAPA. Wadau walisema hatoki hata mmoja sass RA Katoka mmeanza mara ooh hamuwawezi mara pooh wamekwama,,,lipi Jena KWENU? Mnakuwa Kama hula mnapata perio....ikifika LAZIMA kuziba ikiisha eehee
<br />
<br />

Hayo mambo yakujivua gamba lenu bila kurudisha mali zilizoibiwa haitakaa ikubalike machoni mwa watanzania hata kama na mwenyekiti akivua gamba.

Kimsingi hakuna kitakachoweza kuifanya ccm iishi tena zaidi ya miaka 4 ijayo. Naamini watanzania wengi tunaomba ccm ife mapema iwezekanavyo.
 
Hivi mnataka alama gani mjue CCM imekufa tayari?

Kama walikutana na kutumia fedha nyingi wengine kutoka Zanzibar na kujadili na kuazimia hayo mambo mepesi ambayo rais au hata waziri Mkuu au katibu wa Chama ange weza kuyatolea maamuzi na ufafanuzi akiwa pale Magogoni au Lumumba, mnasubiri nini kuizika CCM? Haipo tena ni woga wetu tu! labda tunaogopa vyombo vya dola lakini chama cha siasa hamna hapo tena hapo.

Kumbe ndio maana Ben che Mkapa hakwenda, hata hicho kikao kimeifisadi CCM.
 
NAJUTA KUIFAHAMU HII 'CCM FOTOKOPI' NA MAAGIZO YA KINAFIKI NCHINI

Hakika ni vioja kuona mkono mmoja wa Jakaya Kikwete akiwa ni rais wa nchi (wa ki-aina) ikipandishia mwananchi gharama ya maisha katika kila idara ya maisha ikiwa ni pamoja na nishati ya mfuta ya taa.

Bajeti za wizara zote zinapoandaliwa huwa ni wa kuzingatia zaidi dhamira na dira ya rais kwa watu wake hata kabla haijapelekwa bungeni. Kwa lugha nyingine rais ndiye mkuu wa kutengeneza bajeti ya serikali hivyo kugeuka kuipinga kwa namna yoyote ni unafiki na kupotezea muda Wanzania.

Na kwa upande mwingine inatia kinyaa kuona mkono mwingine wa pili wa mtu huyo huyo na serikali yake, eti kwa sababu tu sasa kavaa kofia ya CCM kusahau alichokifanya akiwa na kofia ya serikali, ukionekana kutoa machozi ya mamba KUMHURUMIA mlazwahoi wa Tanzania eti kwamba bora alale njaa lakini akawashe japo ka-kibatari kutazama nyo nyuso za wanawe yalivyokunyamana kutokana na kero za njaa mwana malegezo ambayo CCM haikuona umuhimu wowote wa kuijadili.

Jamani hii hali hasa ndio 'Masterpiece Case' ya UNAFIKI inayoelezea kwa nini tumefikia hapa tulipo kama taifa; kufanya mzaha mtupu kwa maisha ya watu; jambo ambalo linatusukuma kuanza kujiuliza ya kwamba hiyo ORODHA NDEFU YA MAAGIZO HEWA ya CCM yaliotolewa leo kwani ni AKINA NA NANI HAO (wakiwamo Chenge, Karamagi, Lowassa na akina Abdalla Zombe) NDIO WALIOKWEPO KWENYE KIKAO HICHO HUSIKA na historia ya uadilifu unawaweka wapi hasa mbele ya macho ya Watanzania????????

Nakumbuka mara kadha Mwalimu Nyerere alikua na kawaida ya kwenda mbali kidogo katika mambo mengi kiutendaji kama kiongozi wa nchi kutazama ujumbe unaotolewa na vile vile kumtazama usoni hasa MTOA UJUMBE mwenyewe ili apate kuona kama maneno matamu yaliopakwa siagi, maziwa na asali kiasi hicho kweli yanaendana na mtu mwenyewe jinsi tunavyomfahamu uadilifu wake????? Jama Watanzania kabla ya kumeza haya maneno matupu yenye kufikiria tena huyu mdudu 'MPANGO WA DHARURA WA KUREKEBISHA UMEME NCHINI' (dirisha kuu la ufisadi kama zile za Richmond) ni sharti watu tukajiulize kwamba maamuzi hayo yalitolewa watu gani wenye sifa zipi machoni mwa jamii.

Ama kweli Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ilikua ni enzi zile za akina mzee Chrisant Mzindakaya na vikao vikiongozwa na Mzee mwenyewe wa UADILIFU kote dunia, Mwalimu JK Nyerere. Na kweli wakisema kitu na wananchi sote tunasikiliza na kutumainia.

Sasa hivi kumebakia ngonjera na mazingaombwe tu kwenye vikao vya CCM vilivyopata kuheshimika huko nyuma na mwishoni kututokea puani kule kuamini kwingi viongozi wasio waadilifu kwa kila kitu; hebu sasa ngoja tu uje usikie fedha za uchaguzi wa 2015 zitakavyoanza kusakwa bila aibu kwa kasfa nyinginezo nzito zaidi kuliko za Richmond eti kwa kupitia tu kichochoro hicho cha 'UMEME WA DHARURA' uliosemwa na CCM huko Dodoma.

Tangu nisikie neno 'UMEME WA DHARURA' kwenye taarifa hii ya CCM mwenzenu najikuta nikitamani kuhamashisha Watanzania wote Wakulima vijijini kwa wafanyakazi mijini sote twende tukashike doria kwenye ule utaratibu wetu tuliojizoelea wa SUNGUSUNGU ya Mrema pale Benki Kuu yetu ya Taifa ili akina Rostam Aziz wengine wasije wakaanza tena kututenda jinsi ambavyo walivyotugeuza sisi walipakodi kuwa ni mazezeta.

Nasema kwa maagizo hayo yaliotolewa na watuhumiwa wetu wale wale CCM kwa kashfa kibao za UFISADI ambazo bado hazijapatiwa jawabu lolote nchini, ni vema kila mlipakodi akalikazia macho mfuko wetu wa pamoja taifa pale hazina kwa kuwa ni dhahiri mpango mwingine wa wizi ndio huo umeanza upya tena Dodoma.

Mtu ukiwahi kuumwa na nyoka, kitendo tu cha majani kuonekana kutetemeshwa ovyo ni sababu tosha ya KURUKA NA KUKANYAGANA ovyo.

 
Back
Top Bottom