Tuache kupayuka,tusubiri kikao cha NEC.Kauli ya kujivua gamba ilikuwa ni usanii tu ndio maana sasa wanaikimbia kauli yao wenyewe. Lowassa na Chenge wamegoma kung'oka na hakuna mwenye ubavu wa kuthubutu kuwafukuza maana chama chote kimejaa mafisadi.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imemaliza kikao chake cha siku moja usiku wa tarehe 31/07/2011 mjini Dodoma chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
1. Imefanya uteuzi wa makatibu ishirini na saba (27) kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika wilaya hizo. (majina na wilaya zao yameambatanishwa). Pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu imetengua uteuzi wa Makatibu wa Wilaya watatu (3) katika kuboresha ufanisi wa kazi katika wilaya hizo.(majina na wilaya zao yameambatanishwa).
Maneno muhimu..."imepokea na kuridhia taarifa...", kwa maana kuwa hakuna mjadala wala tathmini. CC haikuagiza hilo lifanyike, kwa hiyo hakukuwa nachakufuatilia hapo.2. Kamati Kuu imepokea na kuridhia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuwakilisha Mkoa wa Tabora, Ndugu Rostam Aziz. Aidha imempongeza kwa uamuzi huo uliozingatia maslahi mapana ya chama chake.
Maneno muhimu..."imepokea taarifa...", kwa maana kuwa hakuna mjadala wala tathmini. Katibu Mkuu alikwisharidhia huu uamuzi wa Rostam na kumuarifu Spika kwa mujibu wa utaratibu. CC haikuagiza na wala hakuna mjadala.3. Kamati Kuu imepokea pia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Ndugu Rostam Aziz na kuagiza chama kupanga ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga itakayozingatia ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya uteuzi wa mgombea. Aidha Kamati Kuu imeagiza shughuli zote za kampeni kutafanywa na CCM Mkoa, Wilaya na ngazi zote za chama wilayani Igunga. CCM Taifa watashiriki kuongeza nguvu. Chama kinatoa wito kwa wana CCM, wapenzi na wakereketwa wa chama chetu kushiriki kwa pamoja kuhakikisha jimbo linabaki kwa CCM.
Haijaridhishwa? Kiwango gani ndiyo kinaridhisha? Mwenyekiti wa CC ndiye mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, na ndiye Rais (Mkuu wa Serikali). Kikwete anasimamia maamuzi ya CC kuagiza serikali ya Kikwete kuhusu kutekeleza uamuzi wa ........ (sijui uamuzi wa nani?). Mkanganyiko.4. Kamati Kuu haijaridhishwa na kiwango cha bei ya mafuta ya taa nchini kwa kuwa ndio nishati inayotumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini. Aidha Kamati Kuu haikuridhishwa na maelezo ya kupandishwa kwa bei ya mafuta hayo kwa kisingizo cha kuzuia uchakachuaji wa mafuta mengine. Hivyo basi, Kamati Kuu imeiagiza Serikali kutafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa na kuvitaka vyombo vya Serikali vinavyohusika na usimamiaji wa ubora wa mafuta, vihakikishe vinatimiza wajibu wake kuzuia kabisa mtindo wa uchakachuaji wa mafuta nchini na si kupandisha bei ya mafuta ya taa kama suluhisho.
Inasikitishwa? Kweli hili ndiyo neno sahihi waliona katika ujumbe huu? Na pia, Mwenyekiti wa CC ndiye mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, na ndiye Rais (Mkuu wa Serikali). Kikwete anasimamia maamuzi ya CC kuagiza serikali ya Kikwete kuhusu kutekeleza uamuzi wa ........ (sijui uamuzi wa nani?). Mkanganyiko mwingine.5. Kamati Kuu inasikitishwa na tatizo la umeme nchini kwani athari zake kwa uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja ni kubwa. Hivyo basi imeitaka Serikali kutumia muda iliyopewa wa kurekebisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kuja na mpango wa dharura wa kunusuru hali hii na kisha kulimaliza kabisa tatizo la umeme nchini.
Kwa lugha nyingine, kulikuwa na mazungumzo kama ya kijiweni. Hakuna agenda wala azimio mahsusi. Ni kila mmoja kusema liwalo na mwisho kukubaliana kuwa ndiyo iwe hivyo. Yanatatulika haya, tusipoteze muda kutatua au hata kuagiza yatatulike.6. Aidha Kamati Kuu imejadili masuala mengine kama; migogoro ya ardhi, tatizo la bei ya pamba, tatizo la uuzaji wa mahindi, migogoro migodini, masuala yanayohusu kero za Muungano na kuagiza Serikali kuyashughulikia kwani yanatatulika.
Labda mie sijaelewa hapa. Wanapongezwa kwa kazi nzuri ya kutekeleza maamuzi ya NEC, kuwataka waongeze kasi katika utekelezaji huo. Kwa hiyo wametekeleza (wapongezwe?) au hawajatekeleza (waongeze kasi?)?7. Kamati Kuu imeipongeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kazi nzuri ya kutekeleza maamuzi ya NEC na kuitaka iongeze kasi katika utekelezaji huo, ili kuhakikisha mageuzi yaliyokusudiwa yanatekelezwa kwa wakati. Aidha imejadili na kupitisha miundo mipya ya Idara ya Itikadi na Uenezi na Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Hapo sasa. Inawezekana wamejipima kwa siku 120 na wameamua kuwajibika kwa kubakia katika nafasi zao ndani ya chama na jamii, kwa masilahi mapana ya chama.....na yao pia. Je, CC mnasemaje? Taarifa wapeleke wapi?8. Kuhusu suala la maadili ndani ya Chama, Chama kinaendelea kusimamia maadili, na kuwataka wale waliotakiwa kujipima na kuwajibika watumie muda huo, kujipima na kuwajibika kwa masilahi mapana ya chama. Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inatarajiwa kukutana wakati wowote mwezi Septemba, ambapo pamoja na mambo mengine itatathimini utekelezaji wa maamuzi yake.
full kudata! nasikia na kale ka ugonjwa ka kisasa huwa kanaathiri uwezo wa kufikiria!4. Kamati Kuu haijaridhishwa na kiwango cha bei ya mafuta ya taa nchini kwa kuwa ndio nishati inayotumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini. Aidha Kamati Kuu haikuridhishwa na maelezo ya kupandishwakwa bei ya mafuta hayo kwa kisingizo cha kuzuia uchakachuaji wa mafuta mengine.
Hivyo basi, Kamati Kuu imeiagiza Serikali kutafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa na kuvitaka vyombo vya Serikali vinavyohusika na usimamiaji wa ubora wa mafuta, vihakikishe vinatimiza wajibu wake kuzuia kabisa mtindo wa uchakachuaji wa mafuta nchini na si kupandisha beiya mafuta ya taa kama suluhisho.
Kweli haya sasa ni maigizo, Mhe. amepitisha bajeti na kukubali bei ya mafuta ya taa ipande akiwa kama mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, then huku akiwa kama mwenyekiti wa CC anasema hapana bei ya afuta ya taa ishushe tena anaiamuru serikali hiyo hiyo anayoongoza yeye!!
Hapo naunga mikono na miguu 100%Yani kwenye kikao cha baraza la mawaziri wameamua mafuta ya pande bei, kwenye halmashauri ya magamba wanasema bei ishuke eti inamuumiza mtu wa chini, vikao vyote hvyo mwenyekiti mmoja. Hakika bora tz bora hata tungempa DOVUTWA tujue moja.