Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
- Thread starter
- #81
Usifikiri kwa vile hutuoni Ccj basi tunasubiri mtuletee mabadiliko NO we are fighting on the other side of the mountain hamtuoni, ina maana na nyie Ccj mlisubiri wengine wawaanzishie mfumo wa vyama vingi halafu nyie muende kuomba usajili Idara ya maelezo huku mmevaa tai kubwa mkisindikizwa kwa ulinzi wa polisi, jueni kuwa kuna wenzenu walipoteza maisha kuupigania mfumo huu ambao baada ya miaka 15 ndiyo mnajitokeza, kwa hiyo msividharau vyama vingine mvipe heshima stahili.
wrong; mfumo wa vyama haukuanzishwa na wengine ulianzishwa na wenyewe tena pasipo shinikizo lolote lile. As a matter of fact ni kwa hisani "yao" ndiyo vyama hivyo vingine vimekuwepo na ndio sababu hadi leo hii hawasumbuliwi na uwepo wa vyama hivyo vingine. Na zaidi ni kuwa CCJ ni matokeo ya watu ambao wameshiriki katika mapambano ya vyama vingi toka awali.
Hata hivyo usichukulie kuwa nadharau mchango wa vyama vingine vya upinzani kwani nitakuwa si mkweli wa historia na mkanaji wa hisani yao kwa taifa. Wamefanya mengi na mchango wao ni mkubwa tangu awali. Hata hivyo ninatambua kuwa kila zama ina mashujaa wake. Wao walikuwepo na sisi sasa tupo. Wengine walioko CCJ leo hii hata kuzaliwa walikuwa hawajazaliwa wakati vuguvugu la vyama vingi liliporudi tena.
So.. hizi ni zama zao!