Tamko la CCJ dhidi ya Kauli za Tendwa juu ya Usajili wa kudumu

Usifikiri kwa vile hutuoni Ccj basi tunasubiri mtuletee mabadiliko NO we are fighting on the other side of the mountain hamtuoni, ina maana na nyie Ccj mlisubiri wengine wawaanzishie mfumo wa vyama vingi halafu nyie muende kuomba usajili Idara ya maelezo huku mmevaa tai kubwa mkisindikizwa kwa ulinzi wa polisi, jueni kuwa kuna wenzenu walipoteza maisha kuupigania mfumo huu ambao baada ya miaka 15 ndiyo mnajitokeza, kwa hiyo msividharau vyama vingine mvipe heshima stahili.

wrong; mfumo wa vyama haukuanzishwa na wengine ulianzishwa na wenyewe tena pasipo shinikizo lolote lile. As a matter of fact ni kwa hisani "yao" ndiyo vyama hivyo vingine vimekuwepo na ndio sababu hadi leo hii hawasumbuliwi na uwepo wa vyama hivyo vingine. Na zaidi ni kuwa CCJ ni matokeo ya watu ambao wameshiriki katika mapambano ya vyama vingi toka awali.

Hata hivyo usichukulie kuwa nadharau mchango wa vyama vingine vya upinzani kwani nitakuwa si mkweli wa historia na mkanaji wa hisani yao kwa taifa. Wamefanya mengi na mchango wao ni mkubwa tangu awali. Hata hivyo ninatambua kuwa kila zama ina mashujaa wake. Wao walikuwepo na sisi sasa tupo. Wengine walioko CCJ leo hii hata kuzaliwa walikuwa hawajazaliwa wakati vuguvugu la vyama vingi liliporudi tena.

So.. hizi ni zama zao!
 
Nimeipenda CCJ kwani imeweza kuifanya serikali ya CCM kuonyesha woga na sasa inaanza kujiumbua na kujikuta iko uchi hadharani. Kitendo cha Msajili cha kushindwa kutimiza wajibu wake kama ilivyoainishwa kwenye katiba kinatoa maswali mengi kuliko majibu. Hivi sasa ni wazi kuwa Tendwa kama alivyo Jaji Makame ni wakereketwa wa CCM na kama kawaida yao ya ulafi wako pale kuhakikisha huu utawala wa kifisadi hauondoki madarakani kwani wananufaika nao. Kwa bahati mbaya wameshindwa kwenda na wakati na kutambua kuwa huwezi kudanganya watu wote wakati wote - sana sana utajikuta unajidanganya mwenyewe kama Tendwa anavyojidanganya sasa. Tofauti na mbinu za vyama vilivyotangulia ambavyo vimejizatiti zaidi katika kukata matawi ya huo mbuyu (CCM) kwa dhana ya kuuangamiza, CCJ wameelekeza zaidi nguvu zao katika kukata mizizi ya huo huo mbuyu (CCM). Pamoja na vyama vingine kuendelea kuivua nguo serikali ya CCM, CCJ inataka kuhakikisha wenyewe wanazivua nguo zao kama anavyoanza kufanya Msajili Tendwa kama zezeta vile - patamu hapo.
Mimi nimeshampelekea text message, wewe hapo ulipo unasubiri nini ?
 
Mpaka leo bado tu hajatengeneza huo msingi wa maandamano wakati muda umekwisha,leo ni tarehe 26 Mei sasa kama mko slow kiasi hicho maana yake hata mkipata usajili mtakuwa mmeshachelewa kujiandaa na uchaguzi mkuu kwa hali hii mlipaswa kuwa very fast ili mkimbizane na muda..Mtajipanga saa ngapi ili mshiriki uchaguzi Mkuu kama hata usajili wenyewe mnautafuta kwa mapozi hivyo..Sheria mpya ya uchaguzi inawataka kukusanya fedha pamoja na vifaa vyote vitakavyotumika wakati wa uchaguzi si chini ya siku 90 nyie bado mnajikongoja tu..Inakula kwenu!by the time mnapata usajili hamuwezi tena kushiriki uchaguzi kwa kuwa mmeshindwa kumeet matwaka ya sheria ya gharama za uchaguzi..Itakuwa imekula kwenu.

kama imewachukua miaka zaidi ya 15 kushindwa kuja na msingi wa maandamano yoyote ya maana utaishangaa CCJ ambayo hata usajili wa kudumu haina?
 
GS

Hawa jamaa nafikiri timing yao ni mbovu lini wataenda kwa wananchi, kama suala ni kushiriki uchaguzi kwa gharama yeyote nafikiri wana mis point, wangekuwa na busara wangesubiri wasajili baada ya uchaguzi watu wangewaelewa vinginevyo tuchukulie ni uroho wa madaraka au wanatafuta huruma ya wananchi au wanataka kuanzisha shari.

vile vilivyopo sasa navyo havina uroho wa madaraka, havitaki huruma ya wananchi kila wanaposimama majukwaani "kuishtaki" serikali kwa wananchi? au ndio waoga wa kutaka shari kwa sababu wanaamini katika falsafa hewa ya "umoja, amani, na mshikamano" na mafisadi?
 
Mpaka leo bado tu hajatengeneza huo msingi wa maandamano wakati muda umekwisha,leo ni tarehe 26 Mei sasa kama mko slow kiasi hicho maana yake hata mkipata usajili mtakuwa mmeshachelewa kujiandaa na uchaguzi mkuu kwa hali hii mlipaswa kuwa very fast ili mkimbizane na muda..Mtajipanga saa ngapi ili mshiriki uchaguzi Mkuu kama hata usajili wenyewe mnautafuta kwa mapozi hivyo..Sheria mpya ya uchaguzi inawataka kukusanya fedha pamoja na vifaa vyote vitakavyotumika wakati wa uchaguzi si chini ya siku 90 nyie bado mnajikongoja tu..Inakula kwenu!by the time mnapata usajili hamuwezi tena kushiriki uchaguzi kwa kuwa mmeshindwa kumeet matwaka ya sheria ya gharama za uchaguzi..Itakuwa imekula kwenu.

tatizo nikuwa nyinyi mnaikumbatia hiyo sheria wakati mimi siikumbatii wala kuitambua. Ni sheria mbovu na dhamira yangu hainitumi kuipa heshima yoyote. Ni miongoni mwa sheria ambazo CCJ itazifuta the first seven days as I know. Nyinyi Chadema naona mmekubali iwepo na hamjafanya lolote kuipinga zaidi ya kutoa hotuba ya kwanini ni sheria mbovu - jambo ambalo wengine pia wamelifanya.
 
Nimeipenda CCJ kwani imeweza kuifanya serikali ya CCM kuonyesha woga na sasa inaanza kujiumbua na kujikuta iko uchi hadharani. Kitendo cha Msajili cha kushindwa kutimiza wajibu wake kama ilivyoainishwa kwenye katiba kinatoa maswali mengi kuliko majibu. Hivi sasa ni wazi kuwa Tendwa kama alivyo Jaji Makame ni wakereketwa wa CCM na kama kawaida yao ya ulafi wako pale kuhakikisha huu utawala wa kifisadi hauondoki madarakani kwani wananufaika nao. Kwa bahati mbaya wameshindwa kwenda na wakati na kutambua kuwa huwezi kudanganya watu wote wakati wote - sana sana utajikuta unajidanganya mwenyewe kama Tendwa anavyojidanganya sasa. Tofauti na mbinu za vyama vilivyotangulia ambavyo vimejizatiti zaidi katika kukata matawi ya huo mbuyu (CCM) kwa dhana ya kuuangamiza, CCJ wameelekeza zaidi nguvu zao katika kukata mizizi ya huo huo mbuyu (CCM). Pamoja na vyama vingine kuendelea kuivua nguo serikali ya CCM, CCJ inataka kuhakikisha wenyewe wanazivua nguo zao kama anavyoanza kufanya Msajili Tendwa kama zezeta vile - patamu hapo.
Mimi nimeshampelekea text message, wewe hapo ulipo unasubiri nini ?

Natumaini wana demokrasia wetu kina GS na Luteni watakuwa tayari na wenyewe wametuma ujumbe huo..
 
Hili tamko limeenda shule, short, detailed and comprehensive. Go CCJ, wasipotoa usajili tunasimamisha uchaguzi.
 
Wewe ni mzandiki, mzushi na muongo, acha kabisa kuniwekea maneno yako ebo!, nioneshe wapi nimeandika "CCm sasa wamekomaa?". We vipi wewe!!!
Hofstede

Taratibu huna haja ya kutumia maneno kama hayo, pitia post yako hii hapa chini kwenye red utueleze ulikuwa na maana gani, hiyo kama si kukomaa kwa CCM ni nini, Respect

Sipendi malumbano ila kwa hili ngoja nikupe maelezo

1. 1995: CCM ilikuwa changa katika siasa za vyama vingi hivyo basi mbinu chafu kama za kuiba kura na kuvuruga uchaguzi walikuwa hawajajiweka sawa, ..............................................................................................

Sasa leo hii 2010 CCM wana uwezo wa kufanya watakavyo kuanzia kuiba kura na hata kuamrisha watendaji wao waliowaweka kutotangaza mpinzani kashinda mpaka wampe baraka Je kwa nini WANAOGOPA KUIPATIA CCJ USAJILI WA KUDUMU?
 
Hofstede

Taratibu huna haja ya kutumia maneno kama hayo, pitia post yako hii hapa chini kwenye red utueleze ulikuwa na maana gani, hiyo kama si kukomaa kwa CCM ni nini, Respect

Mkuu Luteni;
Maneno kama hayo huwa nayatumia tu pale mtu anaponiwekea maneno yake kwangu, mbona kwenye hiyo quote ya red sijaona sehemu niliyosema "CCm imekomaa?". Ninapenda sana kujadili hoja, pia mtu ani quote kwa nilichoandika/sema ila sipendi kujadili nilichozushiwa. kwa hiyo wewe unastahili kuitwa na mimi "maneno kama hayo" kwa kuwa umewadanganya wasomaji kuwa mimi nimeandika nisichokuwa nimeandika na pia umenizushia kuwa nimesema ambacho sijaandika.

Mkuu sasa tujadili hoja za CCJ kwa ukweli bila kuzushiana. Vinginevyo uni quote na andika unalotaka nitakujibu kwa hoja tu, na sitatumia "maneno kama hayo"
 
kama imewachukua miaka zaidi ya 15 kushindwa kuja na msingi wa maandamano yoyote ya maana utaishangaa CCJ ambayo hata usajili wa kudumu haina?

Hapo ndio napo pataka..Hoja yangu ni kuwa mnajimegea kwamba CCJ itafanya yale ambayo vyama vya upinzani vimeshindwa kufanya kwa miaka 15 lakini kumbe hata CCJ yenyewe inapita mule mule tena bora haya ya vyama vingine..To be honest sijaona jipya kabisa,MUNGU anisamehe kama nakosea...Ukiwa nje ni rahisi sana kuona kama wengine hawafanyi kitu wamekaa,tu ndio maana wahenga walisema ukitaka kufaidi uhondo wa ngoma
ni lazima uingie ucheze.Eti siku saba kwa Tendwa vinginevyo mahakamani..yale yale tu ambayo hata vyama vingine tumefanya.Hivi CCJ inadhani Tendwa anaogopa mahakama au kesi?kwanini atakayeshitakiwa na yeye au ofisi yake?naamini Tendwa wala hatabadilisha msimamo wake tena anasubiri kwa hamu hizo siku saba zifike ili muende mahakamani..Steps ni zile zile labda mlichotuzidi ni staili ya kujitambulisha kwa jamii basi zaidi ya hapo,hakuna jipya...
 
hahaha adui yako akijua yote unayotaka kufanya basi hufai kupigana...
 
Natumaini wana demokrasia wetu kina GS na Luteni watakuwa tayari na wenyewe wametuma ujumbe huo..

Sorry kwani huu ujumbe unaenda kwa Tendwa au kwa nani?kama ni kwake hivi unafikri atazisoma kweli meseji zetu?au zinaenda kwa nani ili aharakishe usajili huu?Niko tayari kutuma lakini mpaka nipate majibu ya kuridhisha..Hata sms 50 naweza kutuma pia ila mniconvince kwanza!!!
 
wewe tuma.. na ndiyo zinakwenda kwa Tendwa... jamani ndiyo ushiriki wa wananchi. Wenzenu hapa kijijini we do this all the time, tena kwa email halafu huwa tunapeleka hadi mabarua kwenye maofisi ya wabunge ili watusikilize... ni kuonesha kuwa wananchi wanajali..
 
na vipi kuhusu privacy za watu wanaotuma ujumbe huo kumbukeni namba sasa hivi zimesajiliwa zilizo nyingi msijitafutie mambo mengine wananchi
 
tatizo nikuwa nyinyi mnaikumbatia hiyo sheria wakati mimi siikumbatii wala kuitambua. Ni sheria mbovu na dhamira yangu hainitumi kuipa heshima yoyote. Ni miongoni mwa sheria ambazo CCJ itazifuta the first seven days as I know. Nyinyi Chadema naona mmekubali iwepo na hamjafanya lolote kuipinga zaidi ya kutoa hotuba ya kwanini ni sheria mbovu - jambo ambalo wengine pia wamelifanya.

Tumepiga kelele sana kama wewe hujaona basi..kwa kuwa wao ndiom wameshika kisu kwenye mpini nasi tunajitosa hivyo hivyo hata tukikataa sasa haitatusaidia kitu badala yake sisi ndio tutakaoharibikiwa..hata sisi tukipewa uwezo wa kufuta sheria mbalimbali hata hiyo itakuwa miongoni mwao..hatujaikumbatia hata kidogo,tutakumbatiaje sheria zinazotuumiza?hivi hili linawezekana Mwanakijiji,umezungumza kwa kutafakari au?
 
na vipi kuhusu privacy za watu wanaotuma ujumbe huo kumbukeni namba sasa hivi zimesajiliwa zilizo nyingi msijitafutie mambo mengine wananchi

privacy ya vitu gani kwani ni siri; mimi nimetuma na kusaini kwa jina langu halisi siyo la mwanakijiji.
 
wewe tuma.. na ndiyo zinakwenda kwa Tendwa... jamani ndiyo ushiriki wa wananchi. Wenzenu hapa kijijini we do this all the time, tena kwa email halafu huwa tunapeleka hadi mabarua kwenye maofisi ya wabunge ili watusikilize... ni kuonesha kuwa wananchi wanajali..
Binafsi sijaelewa tukituma hizo text kwa Tendwa halafu what is next naje asipozifungua na kuzisoma itakuwa imetusaidia nini, nipe shule kabla sijaamua kutuma coz this in new strategy inawezekana ndiyo mbinu mpya za Ccj unazosema.
 
asipozifungua zitajaa kwenye simu yake siyo? au zinafutika; au atakuwa na kazi ya kuzifungua lakini atakuwa ameshasoma chache.. huu unaitwa usumbufu wa kisiasa; kumfanya ideal na hilo swala. As a matter of fact nzuri zaidi ni ya kumpigia simu na kumpa ujumbe huo.
 
Habari Leo

CHAMA cha Jamii (CCJ) kimesema kitamkopesha Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa begin_of_the_skype_highlighting end_of_the_skype_highlighting fedha za kuwapa maofisa wake 10 wafanye uhakiki wa wanachama wa chama hicho mikoani ili kipate usajili wa kudumu. CCJ imemtaka Tendwa aseme anahitaji shilingi ngapi kwa ajili ya kazi hiyo.

Chama hicho kimesema,wanachama wake watachanga fedha na wataikopesha ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na zitarudishwa na riba.

Msemaji wa CCJ, Fred Mpendazoe begin_of_the_skype_highlighting end_of_the_skype_highlighting, amesema, chama hicho kinampa Tendwa wiki moja atoe ufafanuzi kwa nini hana fedha za kuwatuma maofisa wake kufanya uhakiki wakati kwa mwaka huu hakuna chama kilichofanyiwa uhakiki au hakukuwa na bajeti ya suala hilo.

"Tunaomba msajili atuambie bajeti ya kupeleka maafisa wake 10 ni kiasi gani na sisi na wanachama wetu tutachanga fedha ambazo tutaikopesha serikali ili kuwatuma maafisa wake na baadaye zitarudishwa na riba juu" amesema Mpendazoe.

CCJ pia imemtaka Tendwa aeleze ameshindwaje kukisajili chama hicho kwa madai ya kuwa na kazi nyingine wakati msingi wa ofisi yake ni usajili wa vyama vya siasa na nyingine ni za ziada.

Mpendazoe amesema, shughuli nyingine za ofisi hiyo hazipaswi kuingiliana kwa namna yeyote ile na majukumu yake makuu ya kusajili vyama vya siasa.

Mpendazoe ameyasema hayo akiwa na Mwenyekiti wa CCJ , Richard Kiyabo na Katibu wa chama hicho, Renatus Mukabhi.

Viongozi hao wa CCJ wamedai kuwa,endapo hawatapata maelezo ya kuridhisha wataenda mahakamani ili wapate haki.

"Kuna kila dalili ambazo zinaonesha msajili anatumika kwa kiasi fulani katika kukwamisha chama hiki cha jamii kisipate usajili wa kudumu kwani siyo rahisi akawa hana bajeti ya kusajili chama wakati ndio msingi wa ofisi yake" amesema Mpendazoe.

Amesema,CCJ kimekamilisha matakwa ya msajili na kwenda kuomba usajili wa kudumu, msajili alitakiwa kuanza kuhakiki wanachama ili akatae au akubali maombi yao lakini si kukataa hadharani kupitia vyombo vya habari hata kabla ya kujaribu kuangalia maombi yao jambo ambalo ni kinyume na haki.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom