Tamko la CCJ dhidi ya Kauli za Tendwa juu ya Usajili wa kudumu

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,996
Chama cha Jamii ambacho kimenuiwa kunyimwa usajili wa kudumu na Serikali inayodaiwa kuwa ni ya kidemokrasia ya Rais Jakaya Kikwete leo kimetoa majibu yasiyo na utata ya kwanini uamuzi huo ambao umekuwa ukifanyika kama njama kati ya serikali na uongozi wa juu CCM ni uamuzi wa kiwoga, usio na demokrasia na wenye lengu la kukipigisha magoti chama hicho kusalimu amri na kutupilia mbali wazo lake la kutaka kushiriki Uchaguzi Mkuu.

Unaweza kukaa pembeni kusubiri kitu kifanyike au unaweza kushiriki kufanya kitu. Ukitaka kushiriki tuma ujumbe huu:
"Tunakusihi ufanikishe usajili wa kudumu kwa CCJ mapema iwezekanavyo ili kiweze kushiriki uchaguzi mkuu. Asante". Tuma kwenda namba zifuatazo: 754 304772
Habari ndiyo hiyo...

Kutoka Daily News:

CHAMA cha Jamii (CCJ) has given seven days to the Registrar of Political Parties, Mr John Tendwa, to work on their demands otherwise they will go to court.

The party is demanding that the registrar's office state the amount of money needed for verification of the party's status and declare whether the party will get permanent registration or not.


CCJ spokesperson, Mr Fred Mpendazoe said in Dar es Salaam today that the party has already contributed for verification costs.


"If by any means there is no budget for verification of the CCJ then the registrar has to tell us how much is needed for sending officers in 10 regions so that we can make contribution among the members," he stressed.


Mr Mpendazoe, however, said that the funds contributed would be loaned to the government, adding that he is optimistic that the government will pay back.


"I hope we'll get our money back in the next budget. The government has to tell us as soon as possible so that we can start contributing," he explained.


Mr Mpendazoe added: "The registrar's office has to withdraw its statement (of not giving the party full registration) before the press and give the party permanent registration so that it can prepare for the coming general elections."


Contacted for comment today, the registrar said he had just arrived from a journey and therefore would comment when he is back to office next week.


The Minister in the Prime Minister's Office, Policy, Coordination and Parliamentary Affairs, Mr Phillip Marmo, also failed to comment as he was in his constituency (Mbulu).
 

Attachments

  • CCJ-PressRelease.pdf
    73.1 KB · Views: 224
Muda huu nimepata uthibitisho kuwa uongozi wa CCJ ukiwa na tamko kali unaelekea Ofisi za Maelezo ili hatimaye kutoa majibu yake kwa Msajili wa vyama vya siasa. Katika majibu hayo yenye kurasa nne ambayo nimeheshimiwa kuona CCJ inatundika ushahidi wa kimazingira wa jinsi gani uongozi wa juu wa CCM ndio wamefanya uamuzi wa kuzuia CCJ isipate usajili wa kudumu ili isiweze kushiriki uchaguzi mkuu.

Habari ndiyo hiyo...
Thanks, tunasubiria.
 
ccj bana hawaishi visingizio
MS ni vizuri tukayasubiri "majibu hayo yenye kurasa nne yenye ushahidi wa kimazingira wa jinsi gani uongozi wa juu wa CCM ndio wamefanya uamuzi wa kuzuia CCJ isipate usajili wa kudumu ili isiweze kushiriki uchaguzi mkuu"- ndipo tuendelee kujadili.
 
Matamko matamko sijui ni ya nini, sisi tunataka kuona ni njisi gani mnaweza kutumia njia zilizopo kuweza kupata usajiri hata kama tendwa hataki kweli! hapo ndipo tunaweza kujua malengo yenu ambayo kwa sasa kidogo ni mashakani.
 
Lakini tuwe wa kweli jamani, CCJ inaweza kuwa tishio kwa CCM? Siamini
Kutoamini ni mzingi mzuri wa imani imara, hivyo CCJ itakujenga kiimani ili uiamini na kuishuhudia ilivyo tishio kwa CCM ndio maana majibu yenye kurasa nne ya ushahidi wa kimazingira wa jinsi gani uongozi wa juu wa CCM ndio wamefanya uamuzi wa kuzuia CCJ isipate usajili wa kudumu ili isiweze kushiriki uchaguzi mkuu, yatakujia hapa hapa.

Mimi sibanduki posti hii, nasubiria kwa hamu.
 
Its an hour now, bado wapo njiani?
Kesho nae tendwa ataitisha press conference kuwajibu and life goes on.
 
Muda huu nimepata uthibitisho kuwa uongozi wa CCJ ukiwa na tamko kali unaelekea Ofisi za Maelezo ili hatimaye kutoa majibu yake kwa Msajili wa vyama vya siasa. Katika majibu hayo yenye kurasa nne ambayo nimeheshimiwa kuona CCJ inatundika ushahidi wa kimazingira wa jinsi gani uongozi wa juu wa CCM ndio wamefanya uamuzi wa kuzuia CCJ isipate usajili wa kudumu ili isiweze kushiriki uchaguzi mkuu.

Habari ndiyo hiyo...
Mkuu utatuwekea japo facts huo ushahidi wa kimazingira pindi wakimaliza kuongea na wanahabari tafadhali
 
Lakini tukubali tukatae CCM na serikali yake ndiyo wauaji wa demokrasia hapa nchini. Wanakibeza wakati wanafanya mpango mkakati. Kuibuka kwa CCJ na kuimega CCM kutokana na makundi ya uhasama waliyoyatengeneza wao wenyewe ni dalili tosha za kuihujumu CCJ. Hakika CCM hawatataka kuona chama chochote kinasimama na kuwa tishio maana madhambi yao ni mengi. Wameanza kulishana sumu, kuchomana visu nk. Hivi tunawaamini kwa nini hawa. Nakubaliana na mtoa mada. Tusubiri hiyo taarifa.
 
Kwa Miaka 15 Vyama vya Upinzania vimeshindwa Kuishinikiza Serikali, sasa tungojee inawezekana lengo mojawapo la CCJ ni kuuonesha uma wa Upinzani kwamba Serikali inashinikizika ( Sijui ni kiswahili sanifu ama)
 
Unajua wadau tuende mbele Turudi nyuma
>> Kwanza CCM ndo wauaji wa Demokrasia Nchini
>> Pili CCJ sii shabikii ila kwa kweli ni Tishio Kwa CCM maana wanajua ikipewa tu rungu wengi watakihama chama tawala!
>> Tatu mimi nawaambia CCJ wakaze Buti hata kama uchaguzi utazuiwa na mahakama
>> Nne, Kwani Kazi ya Msajili ni nini? Hebu nisaidieni wadau

Maleriasugu Hivi bado tu hubadiliki na kauli zako?
 
Pasco na MMKJ nafurahi kuona mnavyojitahidi kuwafanya watu waone Ccj ni mkombozi, ni kama vile namona Pasco alivyokaa akisubiria hilo tamko. Jamani tumeona na kusikia matamko mangapi we need physical action now na si blaa blaa, leo Ccj wakimaliza tamko lao kesho Tendwa anatoa tamko lake keshokutwa Ccj watakuja na tamko kali maradufu baadaye Tendwa atawapuuza na sinema itakuwa imefika tamati. Mwisho Ccj kwa kujitetea watasema mnaona wasingenishika shati ningemgaragaza, ngumi za utotoni hizo.
 
CCJ leo wamefanya kweli. Press Conference imefanyika na imeshamalizika. Kweli wametoa tanko la kurasa 4 na maelezo ya ziada ya "Hadithi ya Mhalifu na Mfalme".
Taarifa ninayo ila kwa vile Mwanakijiji ametumiwa soft copy, ni vizuri akiiweka, mimi nitawaambia hiki kilichomo kwenye hilo tamko.
 
Ukurasa wa Kwanza.
Wamezungumzia utangulizi na usajili wa muda ulikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kitendo cha Msajili kukataa kufanya uhakiki wa wanachama wa CCJ kupitia vyombo vya habari kabla hata ya kuangalia maombi yao. CCJ wamesema huu ni "HUU NI UNYIMAJI WA HAKI".
 
Ukurasa wa Pili.
Wamezungumzia uwezo wa Msajili kuwa Hana uwezo wa kukataa kusajili kiholela.
Wamenukuu Ibara ya 10 ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya 1992, inayotamka kuwepo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambapo Ibara ya 8(5) inamlazimisha Msajili lazima atoe usajili wa kudumu kwa kila chama cha siasa kilichotimiza masharti ya usajili na kuaninisha vizuizi vinavyoweza kupelekea chama kunyimwa usajili wa kudumu, lakini kipengele cha ofisi ya Msajili kukosa bajeti hakipo kwenye vizuizi, hivyo siyo kizuizi, hayo ni matatizo ya ofisi yake.

Pia wameshutumu tamko la Msajili ati ana shughuli nyingine, wamesisitiza kazi kuu ya Msajili ni kusajili, mengine yote yatafuata.
 
Ukurasa wa Kwanza.
Wamezungumzia utangulizi na usajili wa muda ulikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kitendo cha Msajili kukataa kufanya uhakiki wa wanachama wa CCJ kupitia vyombo vya habari kabla hata ya kuangalia maombi yao. CCJ wamesema huu ni "HUU NI UNYIMAJI WA HAKI".

Tupe kwanza hiyo softikopi tusome halafu ndio tujadiliane. Adhawaisi utakuwa ni mjadala wa upande mmoja.
 
Back
Top Bottom