Tambwe hiza na madiwani wa Arusha!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Wanajamvi kumekuwepo na taarifa ya kukanganya toka kwa tambwe Hiza!

Na John Daniel

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimedai kuna taarifa za uongo zinazosambazwa kuhusu idadi ya madiwani wake katika Manispaa ya Arusha na kueleza kuwa chenyewe ndicho kinachoongoza kwa kuwa na jumla ya madiwani 16 wakiwemo
wabunge watatu.

Chama hicho pia kimesisitiza kuwa kama kingeshindwa kisingeweza kugombania kiti hicho cha umeya kwa kuwa sera na ilani za uchaguzi zitakazotekelezwa na kiongozi huyo bado ni za CCM na si vinginevyo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumulumba, Dar es Salaam jana, Naibu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda, Bw. Tambwe Hiza alisema ni aibu kwa watu wanaojiita viongozi kudaganya wananchi kuhusu idadi ya madiwani bila kuona aibu.

"Kuna taarifa za uwongo zinazoenezwa kwamba CCM imepora umeya Arusha, ukweli ni kwamba CCM ndio ina madiwani wengi kuliko CHADEMA, tuna madiwani 10 wa kuchaguliwa, watatu wa viti maalumu na wabunge watatu, jumla 16.

CHADEMA wana madiwani wanane wa kuchaguliwa, viti maalum watatu, wabunge wawili wa viti maalum na mbunge moja wa kuchaguliwa jumla 14, jamani hapo nani ana madiwani wengi?" alihoji Bw. Tambwe na kuongeza:

"Kwanza CCM hatuwezi kugombani umeya wa Arusha maana sera na ilani ya uchaguzi inayotekelezwa ni ya CCM, asilimia 90 ya fedha za maendeleo za halmashauri zote ikiwemo Arusha zinatoka serikali kuu ya CCM, sasa hata meya akitoka chama gani atatekeleza mipango ya ilani ya CCM, lakini kilichopo Arusha ni ukweli kwamba tulishinda umeya," alisisitiza Bw. Tambwe.

Alisema anasikitishwa na CHADEMA kuhoji uhalali wa Mbunge wake wa viti maalumu, Bi. Mary Chatanda, kuwa mmoja wa wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo wakati sheria ziko wazi kuhusu eneo gani mbunge wa viti maalumu atawakilisha.

"Tarehe 10.12.2010 CHADEMA wenyewe walimwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa serikali kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu wajumbe wa halmashauri kisheria na katika majibu yake kupitia barua yenye kumbukumbu na. JC-A.130-74 ya 16.12.2010 aliwapa ufafanuzi kuwa ni maamuzi ya chama husika kuamua mbunge wake wa viti maalumu atawajibika halmashauri ipi.

"Na hii waliuliza baada ya wao CHADEMA kuamua wabunge wake wawili, Bi. Grace Kiwelu na Bi. Lucy Owenya wawakilishe Halmashauri ya Hai na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo kuwakatalia, lakini baada ya ufafanuzi huo wale wabunge waliruhusiwa, sasa wanachohoji ni nini kama si kupotosha tu wananchi kwa makusudi ili wajitafutie umaarufu bure," alisema Bw. Tambwe.

Alisema kwa mujibu wa sura ya 287 ya kifungu cha 35 1 D wabunge wa viti maalumu wanatokana na idadi ya kura za chama husika, lakini ni wapi wafanye kazi zao ni uamuzi wa mamlaka husika ya chama kilichowateua na kutoa mfano kuwa kwa upande wa CHADEMA kazi hiyo hufanywa na Kamati Kuu.

"Sisi tunasema kama CHADEMA wanadai kuna ukiukwaji wa sheria waende mahakamani badala ya kuchanganya watu, mbona wanadai wameshindwa kuhoji ushindi wa rais eti sheria inawazuia kwenda mahakamani, ndio maana wanataka katiba mpya mbona hili la meya wanaruhusiwa kwenda mahakamani lakini hawaendi kama wana haki," alihoji.

Alikana CCM kutaka kufanya mazungumzo yoyote na CHADEMA kuhusu suala hilo na kusisitiza kuwa chama chake kiko sahihi, hivyo hakina sababu wala nia ya mazungumzo.

Cahanzo GAZETI HURU LA KILA SIKU:: CCM: Tuna madiwani 16 Arusha
 
Back
Top Bottom