Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 34,311
- 54,900
Unapafahamu Tabora kwa Masempele wewe?Kwa Ally Maktubu?Kwa Chizi Mpumunti?Kilabu cha Gondwe?Okay.Tuhamie Rau Madukani Unapafahamu kwa Mwagongo Iringa wewe?Kwa Mwamoto Uyole?Hebu acha utani.Unapafahamu Makanyagio kwenye "mabanzi" kwa Chuwa au Nelkon?Acha utani wewe.Unaufahamu ulanzi wa Mtwivila na mapera ya Ikonongo?🙏😂😂😂😂Be easy!Nakutania tu!Duh! Mbeya naifahamu sana, in and out. Nilisoma Iyunga Sekondari, kuna wakati nilikuwa mtaalam mshauri wa kampuni moja ya kigeni ambayo ilikuwa Mbeya kabla ya mkoa kigawanywa. Hakuna mwaka ambao sijawahi.kufika Mbeya.
Naifahamu Dar kikamilifu sana, nimeishi ma bado nina makazi Dar.
Naifahamu sana Mwanza, nimeishi na nina makazi pia.
Naifahamu sana Arusha, nimeishi na nina makazi Arusha.
Dodoma, Tanga, Tabora, Iringa, Morogoro, Mtwara nazitembelea mara kwa mara.
Ukubwa wa jiji la Mbeya unayazidi kwa kiasi gani majiji kama Arusha, Dodoma, au Tanga?
Unajua ukubwa wa Mwanza na uwingi wa watu wa Mwanza?
Population:
Dar es Salaam 7,405,000
Mwanza city 1,245,000
Mbeya City 620,000
Arusha city 519,000
Tanga City 245,000
Dodoma city 324,347
Kwa statistics hizi, kama kigezo ni population pekee, Mbeya kama itakuwa na majimbo 2, Mwanza itatakiwa kuwa na majimbo mangapi? Dar itatakiwa kuwa na majimbo mangapi?