Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,057
Tanzania ni nchi pekee ambayo vioja haviishi, na vioja hivyo zaidi huletwa na watu wanaoijiita viongozi au Wasomi.
Tanzania ndiyo nchi ambayo unaweza kupata mawazo ya kijinga zaidi kwa mtu anayeitwa doctor au profesa, ya kijinga kuliko unayoweza kuyapata kwa aliyeishia darasa la saba.
Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo sheria, kanuni na hata baadhi ya nafasi hutengenezwa ili mtu fulani apate cheo, siyo kwamba kuna mahitaji. Yaani jimbo linatengenezwa ili tu mtu fulani awe mbunge, siyo kwamba kulikuwa na uhitaji wa kuwa na jimbo la uchaguzi la nyongeza.
Mmesikia huko Mbeya, imekuja huko Dar, na tutaendelea kusikia.
Eti Mbeya igawanywe iwe na majimbo mawili ya uchaguzi kwa sababu idadi ya watu imeongezeka! Upuuzi mkubwa. Hivi ni wapi ambako watu hawaongezeki? Kama kuongezeka kwa watu ndiyo kigezo pekee cha kupngeza idadi ya wabunge, basi itabidi tuongeze na idadi ya MARAIS kwa sababu idadi ya watanzania imeongezeka sana. Kama eneo la jimbo limebakia lile lile, uhalali wa kuongeza jimbo jingine unatoka wapi?
Watanzania tunaongezeka kila siku, ina maana kila mwaka tutakaokuwa na uchaguzi tutakuwa runaongeza idadi ya majimbo ya uchaguzi?
Uongeze idadi ya wabunge kwa sababu idadi ya wananchi imeongezeka, kwani hao wabunge ni madaktari kiasi cha kusema wanazidiwa na idadi ya wagonjwa wa kuwahudumia? Au tuseme hao wabunge ni walimu wa kusema kuwa wamezidiwa na ongezeka la wanafunzi katika darasa?
Kama hatuna akili, tunashindwa hata kutazamia? Hizi nchi ambazo miaka nenda rudi idadi ya majimbo yao ni yale yale, wenyewe hawaongezeki?
Wananchi wanahitaji:
1) Ongezeko la hospitali, madaktari na wauguzi linaloendana na ongezeko la idadi ya watu, siyo ongezeko la wabunge au mawaziri.
2) Ongezeko la shule na walimu, linaloendana na ongezeko la idadi ya watoto, siyo ongezeko la wabunge au mawaziri.
3) Ongezeko la miundombinu ya usafiri na usafirishaji linaloendana na ongezeko la idadi ya watu na vyombo vya usafiri, siyo ongezeko la wabunge au mawaziri.
4) Ongezeko kubwa la uwekezaji litakaloleta ongezeko kubwa la ajira linaloendana na ongezeko kubwa la idadi ya watu, siyo ongezeko la wabunge au mawaziri.
5) Ongezeko kubwa la wazalishaji na walipa kodi watakaoongeza mapato ya Serikali, siyo ongezeko la wabunge. Tunahitaji ongezeko la wazalishaji, siyo matumbo na midomo ya walaji. Wabumge ni walaji, siyo wazalishaji.
Katika mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, iwekwe pia sheria inayozuia kuongeza majimbo, isipokuwa kwa sababu ya pekee na ya wazi kama vile Serikali kama itafuta baadhi ya hifadhi kubwa za Taifa na kuzifanya kuwa maeneo ya makazi na shughuli za kiuchumi. Hiyo itazuia wanasiasa hadaa, ambao badala ya kusema kuwa ushindani wa kuupata ubunge jimboni kwake umekuwa mkubwa, anawahadaa watu eti ni kwa sababu idadi ya watu imekuwa kubwa.
Kama idadi ya watu ndiyo kigezo pekee cha kupngeza idadi ya viongozi na wawakilishi, basi pia toa pendekezo la kuwa na ongezeko la idadi ya Marais, Mawaziri Wakuu, Mawaziri na Wakuu wa Mikoa, maana hao pia wanastahili kuhudumia ongezeko hilo la watu.