Takwimu: Umri wa Mtanzania kuishi umeongezeka kutoka Wastani wa miaka 44 hadi 65

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Akizungumza katika mkutano maalum uliohusisha pia Wakuu wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, leo Agosti 31, 2023, Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa amesema mchakato wa Sensa uliopita umekuwa na mafanikio makubwa na haijawahi kutokea kuwa na ushirikiano wa juu kama uliioneshwa na watendaji.

Ameongeza kuwa Nchi nyingi zinakuja Tanzania kujifunza juu ya mchakato wa Sensa ulivyofanyika.

Amesema “Umri wa Mtanzania kuishi umeendelea kuongezeka, wale waliokuwepo katika Sensa ya Mwaka 1978 umri wa Mtanzania kuishi ilikuwa miaka 44, wakati huo vifo vya kina mama Wajawazito, kwa sasa umri wa Mtanzania kuishi umefika miaka 65.

“Watanzania wanaendelea kuishi zaidi kwa kuwa na wastani wa miaka 69 wakati kwa Wanaume ni wastani wa miaka 62.

“Wanawake wanaishi miaka mingi zaidi kutokana na sababu kadhaa ikiwemo za kibaiolojia.”

Ameongeza kuwa kiwango cha elimu kimeongezeka, watu wanaojua kusoma na kuandika imefikia zaidi ya Asilimia 80, upande wa Bara ni zaidi ya Asilimia 90.

Naye, Kamisaa wa Sensa ya watu na makazi, Anne Makinda akizungumza katika mkutano huo amesema “Awamu ya kwanza ilikuw akufanya uchechemuzi, ya pili kuhesabiwa na ya tatu ni kupeleka elimu ya matokeo ya Sensa kwa wahusika.

“Bado tunawategemea ninyi (wakuu wa mikoa) kuchukua haya ya juu mkayapeleka kwa Wananchi.”
 
Back
Top Bottom