Vinasaba vya panya kumsaidia Binadamu kuongeza umri wa kuishi

Eugen TZA

Member
Aug 7, 2023
61
98
Wanasayansi wamefanikiwa kuhamisha vinasaba (Gene) vinavyoweza kuongeza maisha (umri wa kuishi) kutoka kwa panya wasio na manyoya (Mole Rat) kwenda kwa panya wa kawaida hawa tunaowajua, Utafiti huo unasema baada ya panya hao kuwekewa vinasaba hivyo vimeboresha hali yao ya kiafya na kuongeza umri wao wa kuishi.

Imeelezwa kuwa vinasaba hivyo kutoka kwa panya aina ya Mole Rat vinasaidia kuzalisha Hyaluronic Acid ambayo inasaidia kulinda seli za mwili kuharibika, zikitengeneza ute unaosaidia kulinda seli na kusaidia kuponya kidonda kwa haraka, Baada ya panya hao kuhamishiwa vinasaba hivyo umri wao umeongezeka mara kumi zaidi kwa mujibu wa chuo kikuu cha Rochester.

Umri wa maisha ya panya wa kawaida ni miezi 12 hadi miaka miwili kwa panya wanaotuzwa vizuri, Wakati panya weupe wasio na manyoya (Mole Rat) wanaweza kuishi miaka 28 hadi 37 aina hii ya panya wanapatikana katika nchi za Afrika maeneo ya Kenya na Somalia ambapo vinasaba vyao kwa mujibu wa jarida la Nature vina uwezo wa kuongeza maisha kwa asilimia 5%

#PeaceOverInterest
 
Back
Top Bottom