Takwimu kamili za Matokeo ya Udiwani katika kat zilizofanya Uchaguzi J.pili Tar 16.06.2013

Du Bois ideas

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
427
82
Kwenu wana great thinkers,

Kwanza, kabla ya yote nipende kutoa pole kwa chama Cha Demokrasia na Maendeleo kwa kupoteza wanachama wao na wengine wengi kujeruhiwa katika Bomu lilitokea Soweto Arusha katika kufunga kampeni zao za udiwani katika mji huo, tukio ambalo lilikuwa na watu wengi sana. Kutoka na hilo nawapa Pole sana wanachadema wote walipo popote pale ulimwenguni.

Pili, mimi ningependa tufanye tathmini ya kina katika matokea kule kulikofanyika uchaguzi ili tuone chama gani kinashuka na kipi kinapanda katika medali zake za Kisiasa kati ya Chadema na CCM. Kwa babu kuna post simekuwa zikija hapa zinasema CCM imeshinda viti vingi zaidi vy udiwani katika kat zilizofanya uchaguzi. Maswali amabyo ningependa tupate Takwimu ni haya

1. Jumla ya kata zilikuwa 22 ukitoa kata 4 za Arusha
2. CDM imeshinda ngapi? Na kati za hizo ngapi zilikuwa za CDM hapo awali na ngapi zilikuwa za CCM?
3. CCm Imeshinda kata ngapi Jumla? na kati ya hizo ngapi zilikuwa za CCM na ngapi za CDM?
4. Katika kat zote hizo 2 ukijumlisha CCm imepata kura ngapi na CDM ngapi kwa Ujumla?

Natumaini maswali haya yanaweze kutupa picha kamili kama kweli CCM imeendelea kuwa chama chenye mvuto kwa Watanzania au CDM ndo chama kinachopendwa sasa na watanzania. Mimi paka sasa sina takwimu za matokeo katika kata zote hizo 22

Asante
 
Kutumia ujambazi na wizi wa kura ndio mvoto wa ccm?...huu ni ujinga ndugu yang ulioandika, wananchi tunafikiria siasa za ccm zinapofikia watu kufa kwa mabomu na risasi,wanavokatwa mapanga,kuumizwa na kulazwa hospitali wewe unaleta uzezeta hapa? USHINDI GANI HUU WEWE UNAOUSEMEA? KUUMIZA WATANZANIA WENZETU? KUUWA? Haina hata maana, wewe au mkeo angekufa ungeleta ujinga huu hapa?...
 
Duh mdau umeteka attention yakusoma ujumbe wako kumbe na wew ni ngojangoja. Haya maswal kimsing yakichambuliwa tutajua waz kama ni nani anayeshuka, nani anapanda au nani amesimama palepale(stagnant point)
 
Hivi Rais anayaona haya, atakama NI chama cha upinzani, lakin katika hili Rais anaangaliwa kama kiongozi wa nchi, je kwa mtindo huu kuna chaguzi huru kweli?
 
Prince Tumbo,

ukiangalia katika post yangu kwanza nimeanza na kutoa Pole kwa wahanga wa tukio hili ni kweli kitendo kama hiki hakivumiliki kabisa hata mimi nakipinga kwa 100% lakini jambo lilinifanya kuomba taarifa hizi ni baada ya watu kuanza kupost hapa CCM imeshinda viti vingi vya uchaguzi. Swali la kujiuliza ni kweli wameshinda viti vingi kama wanavyosema takwimu itakuwa msema kweli, mwenye takwimu atupe hapa ili tujua hizi post zima ukweli au ni longolongo?


Kutumia ujambazi na wizi wa kura ndio mvoto wa ccm?...huu ni ujinga ndugu yang ulioandika, wananchi tunafikiria siasa za ccm zinapofikia watu kufa kwa mabomu na risasi,wanavokatwa mapanga,kuumizwa na kulazwa hospitali wewe unaleta uzezeta hapa? USHINDI GANI HUU WEWE UNAOUSEMEA? KUUMIZA WATANZANIA WENZETU? KUUWA? Haina hata maana, wewe au mkeo angekufa ungeleta ujinga huu hapa?...
 
Back
Top Bottom