DOKEZO TAKUKURU Nendeni Mikocheni Sekondari mkaone Walimu wanavyodai Rushwa Waziwazi Kwa Waliomaliza Form4

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,462
29,163
Kwema Wakuu,

Hapa mtaani nilipo kuna ka binti kamemaliza Form4 na majibu ndio yametoka siku chache zilizopita. Shule aliyomaliza inaitwa Mikocheni Sekondari, na ilipo ni njia ya Kawe (Old Bagamoyo Road) kituo kimoja kabla ya Clouds.

Sasa wanafunzi hawa waliomaliza form 4 ili wakabidhiwe Leaving Certificates zao basi inabidi wapite kwa walimu wao mbalimbali na idara mbalimbali pia kusainisha "Clearance Forms", zikishasainiwa pote ndipo wapewe Leaving Certificate.

Walimu kwa kujua kua Wanafunzi wanazihitaji hizo Clearance Certificates wana mchezo wa kuwadai Chochote wanafunzi hao kisha ndio wawasainie. Wanaita hela ya soda lakini imekua ni lazima na mwanafunzi ukiweka ngumu kutoa chochote kitu basi husainiwi.

Iliwahi kutokea hapo kabla kua Wanafunzi kadhaa huchangishana, kuandika majina yao na kukusanya form kisha mmoja huzipeleka kwa mwalimu husika kusaini.

Hata kama ndio motisha lakini isiwe lazima basi, kama mwanafunzi kweli humdai basi ni wajibu wako kumsainia form yake bila kudai chochote kitu.

Watu mnaopokea mishahara Mnajidhalilisha kumkomalia mwanafunzi ambae hana kazi yoyote akupe wewe hela ya soda wakati ni wajibu wako.
 
Wewe unaoushahidi?

Au umesimuliwa na mtoto wako ambaye pengine alitaka pesa ya matumizi yake binafsi ila akasingizia Waalimu wanataka Rushwa ndo apewe leaving certificate?

Usipende kuchafua taasisi pasipo na ushahidi.

Kumaliza shule mwanao isiwe kigezo Cha kuwadharirisha Waalimu.

Walimu wamekufundishia mtoto wako miaka minne halafu Leo unakuja kuwazushia maneno ya kuwadharirisha kiasi hiki?
 
Story kama hizi hazi ingii akilini
Kwa kawaida Mwalimu hawezi kudai mwanafunzi rushwa eti ampe leaving certificate ya kidato cha nne?
Isije kuwa wanafunzi wanadaiwa kutokana na uharibifu mbalimbali walifaonya shuleni au upotevu wa vitabu/vifaa vya shule ambapo ni utaratibu wa kawaida
 
Fanya kwenda pale jumatatu ukaulize. Ukifika tafuta hao Form 4 waliomaliza uwaulize.

Labda iwe wewe ni kati ya walimu hao.
 
Amemaliza form four au form six maana waliomaliza sikuchache zilizopita n F6 form 4 wamemaliza mwaka Jana waliopo watamaliza mwez wa kumi mwaka huu

Sasa huyo aliyemaliza siku Chache amemaliza mtihan wa baraza lipi?
Rudia kusoma tena, maandishi bado yapo.
Sijasema waliomaliza siku chache zilizopita.
 
Story kama hizi hazi ingii akilini
Kwa kawaida Mwalimu hawezi kudai mwanafunzi rushwa eti ampe leaving certificate ya kidato cha nne?
Isije kuwa wanafunzi wanadaiwa kutokana na uharibifu mbalimbali walifaonya shuleni au upotevu wa vitabu/vifaa vya shule ambapo ni utaratibu wa kawaida
Rudia tena kusoma, maandishi bado yapo. Sijasema wanatoa Rushwa ili wapewe Living Certificates.
 
Story kama hizi hazi ingii akilini
Kwa kawaida Mwalimu hawezi kudai mwanafunzi rushwa eti ampe leaving certificate ya kidato cha nne?
Isije kuwa wanafunzi wanadaiwa kutokana na uharibifu mbalimbali walifaonya shuleni au upotevu wa vitabu/vifaa vya shule ambapo ni utaratibu wa kawaida
Mwanangu na yeye mhanga, kapoteza vitabu 2 hivyo leaving yake wameizuia. Ananidai mimi sasa elfu 40 za vitabu vya library. Walau yeye kasema ukweli wake
 
Njaaa itatuaa aise

Ova
Walimu nao wameona wajilipe Kwa namna hyo eti hivi ni haki kweli, imagine nchi Ina wafanyakazi wa Takukuru lkn hawafanyi chochote. Ivi ni lini umeskia Takukuru wamekamata mtu Kwa Rushwa ivi karibuni
 
Olasitti Sec School kule Arusha nao rushwa ya hivi imewanoga sana mpaka kutowatambua wazazi ...wao wanataka mwanafunzi Tu afuate Cheti na wamkamue
 
Waambie hao Takukuru waanze kwanza na askari wetu wa usalama barabarani. Maana kila siku wanachukua rushwa mchana kweupe kutoka kwa madereva wa magari! Na bado hawachukuliwi hatua zozote zile za kisheria!!
Home Boy... Juzi nimeliona Hilo police wa Tz wana hatari sana
Rushwa kama chai kila basi kubwa .
Utaona konda anashuka na kutoa 10k kila sehemu.
 
Story kama hizi hazi ingii akilini
Kwa kawaida Mwalimu hawezi kudai mwanafunzi rushwa eti ampe leaving certificate ya kidato cha nne?
Isije kuwa wanafunzi wanadaiwa kutokana na uharibifu mbalimbali walifaonya shuleni au upotevu wa vitabu/vifaa vya shule ambapo ni utaratibu wa kawaida
Wee...kaka walimu tuache tu!!tuna mambo meusi Sanaa..anachosema Wala sibishi maana nnawajua walimu wenzangu na inafanyika sanaa hyo michezo watoto wakija kuchukua leaving wanaambiwa watowe hata 2000 ya soda
Wala sio uongo brooo...
Ila Sasa kaja kutushtaki jf jamani kaahhh
 
Back
Top Bottom