TAKUKURU leo kupasua jipu kwa waandishi wa habari

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Dr.Hosea anategemewa leo kupasua jipu. Amesema maneno mengi yamesemwa kuhusu uchaguzi wa ccm kwamba ulitawaliwa kwa rushwa lakini hadi sasa hivi hamna aliye fikisha malalamiko takukuru. Sasa leo ameamua kupasua jipu. Hadi sasa haijafahamika ni jipu gani litapasuka leo. Ni hayo tu. mia
 
figganigga Dr. Hosea anatakiwa akabidhi mafaili ya watuhumiwa wa rushwa na ubadhilifu wa mali za umma kwa DPP ili wapelekwe mahakamani na siyo waandishi wa habari.
 
Last edited by a moderator:
... Amesema maneno mengi yamesemwa kuhusu uchaguzi wa ccm kwamba ulitawaliwa kwa rushwa lakini hadi sasa hivi hamna aliye fikisha malalamiko takukuru. Sasa leo ameamua kupasua jipu....
Anataka kumjibu bosi wake?

..Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amesema anakerwa na jinsi vitendo vya rushwa vinavyozidi kushamiri nchini na kutoa wito kwa Watanzania wote kushiriki kwa pamoja kuwafichua na kuwataja hadharani wale wote wanaojihusisha na tabia hiyo.
Alisema anachukizwa kuona vitendo vya rushwa vikizidi kushamiri, huku jamii ikikaa kimya bila kukemea kwa kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo ambavyo vinachangia kwa kiasi kikubwa kuwanyima haki Watanzania walio wanyonge.
 
Hizo ni mbinu za kummaliza Sumaye kisiasa, inasikitisha sana pale TAKUKURU inapotumika kisiasa. Wote tunaiona rushwa ilivyo waziwazi, lakini hawa watu huwa wanakuja na mbinu za kuwaokoa wabadhilifu waziwazi. Kwasasa hatuna imani tena na chombo hiki, ni bora taarifa itoke magazeti ya udaku kuliko kwenye hiki chombo chao cha kujilinda.
 
Take it from me. Hakuna jipu wa mtoto wa jipu atakayepasuliwa leo.! Hosea uwezo aliopewa ni wa kushulikia kasi za dagaa na si kambare. Hata sintopoteza muda wangu kumwangalia kibogoyo huyu
 
Hatakuja na jipya zaidi atawasafisha tu kwa kusema hakukuwa na rushwa katika uchaguzi.
 
Hakuna jipya hapo..waandishi wataenda kwa kuwa kuna MPUNGA tu ila hata story ya front page haitakuwepo.ila atakalotoa leo itakuwa story kubwa kwa vibaraka Habari Leo na Uhuru hapo kesho
 
Dr.Hosea anategemewa leo kupasua jipu. Amesema maneno mengi yamesemwa kuhusu uchaguzi wa ccm kwamba ulitawaliwa kwa rushwa lakini hadi sasa hivi hamna aliye fikisha malalamiko takukuru. Sasa leo ameamua kupasua jipu. Hadi sasa haijafahamika ni jipu gani litapasuka leo. Ni hayo tu. mia

Waandishi wa habari watakaokwend kumsikiliza watakuwa wamekosa kazi ya kufanya kwa ctarajii mapya kutoka hiyo taasisi, wakienda TBC 1, Uhuru, mzalendo hao ni sawa.
 
Jipu la nini au litasaidia kitu gani?Nae auze sura kwenye vyombo vya habari tu hana la msingi.
 
PCCB aise wanachekesha, badala ya kupambana na rushwa wao ndo wala rushwa. Cha ajabu maafisa wake siku hizi wanajifanya maafisa usalama wa taifa eti wakifanya kazi kwa kificho, lo! Wanawatisha watu mitaani na maofisini eti wasipowapa chochote wataitisha file ebooo! Hosea angalia vijana wako na uwafundishe mipaka ya kazi zao bwana. Kazi yao ni kupambana na rushwa tu, period! PCCB si CID wala TISS member.
 
Watu wamehonga mpaka vitumbua hosea unataka kusema nini?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Haya ni matumizi mabaya ya kodi zetu! TAKUKURU haina ubavu wa kuwadhalilisha waajiri wao!
 
Waandishi wa habari watakaokwend kumsikiliza watakuwa wamekosa kazi ya kufanya kwa ctarajii mapya kutoka hiyo taasisi, wakienda TBC 1, Uhuru, mzalendo hao ni sawa.
hawa nao si waandishi au
 
Back
Top Bottom