Usishindwe Kufurahia Maisha yako kwa sababu ya historia au mambo yako ya nyuma

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Taikon kama Mchunguzi huru, na ambaye ninajihusisha na watu wote, nilikuja kugundua kuwa moja ya mambo yanayowafanya Watu wengi kushindwa kufurahia maisha yao ni pamoja na kuendekeza PAST na BACKGROUND zao.

Basi hivi leo, ikiwa wewe ni mmoja wa Watu wa aina hiyo. Mimi Taikon Master ninaujumbe wako.

Past na background yako inaweza isiwe nzuri. Yawezakuwa umetoka katika familia maskini sana. Yaani sana.

Yawezekana umetoka katika familia isiyo na elimu.

Yawezekana unatoka katika familia isiyo na maadili.

Yawezekana umefanya makosa mengi na makubwa.

Yawezekana!

Yawezekana umesoma shule za Kayumba. Yawezekana.

Huenda mambo hayo yanakufanya usijiamini. Na kama hujiamini automatically huwezi kuyafurahia maisha yako.

Sasa Nisikilize! Nasema nisikilize kijana. Tena kwa umakini.

Huhitaji kutoka familia au ukoo bora ili maisha yako yawe na furaha. Hauhitaji hicho.

Huhitaji kusoma shule bora, za vipaji, z gharama ili uwe na furaha maishani.

Huhitaji kutoka katika familia yenye maadili sana ili uwe na maisha yenye furaha.

Huhitaji kuwa mkamilifu ndio uwe na maisha ya furaha.

Huhitaji kuwa Handsome boy au Cute ndio ufurahie maisha

Sizungumzi kama motivation speaker hapa. Nazungumza kama Mtibeli kukufanya uwe kama mimi au zaidi yangu.

Wakati nasoma, nikiwa nimetoka kijijini kwetu Makanya, nimeenda Advance, kuna ile umekutana na wanafunzi wametoka shule kubwa na seminari. Basi kuna ile wanajiona wao ndio wao na wanawapa maneno ya shombo na dharau wenzangu na miye.

Wapo waliojiona duni na kushindwa kufurahia maisha ya Advance Kwa sababu ya Wapuuzi wachache. Lakini haikuwa hivyo kwangu.

Niliapa kwamba, kamwe Past na background zangu hazitanifanya niwe duni mbele ya yeyote yule.
Mademu wakali niliwachukulia, na katika waliofaulu kwa kiwango cha juu kwenye top 5 nilikuwepo.

Yaani niache kupiga Pisikali kisa nimetoka Makanya(kijijini) na kuwaachia waliotoka sijui majiji makubwa. Thubutu labda sio Mimi. Au ati kisa sina nguo nzuri kama wao, au simu nzuri kama wao. Labda sio mimi.

Unajua kuna ile vijana wenzako, washindani wako wananguo nzuri, wana smartphone, alafu wewe huna lolote.

Nakumbuka nilikuwa na tisheti mbili tuu. Moja ilikuwa Tshet ya Liverpool na nyingine ilikuwa Flana nyeusi.

Lakini hayo hayakunizuia kufuata ninachokitaka. Sikuwa duni mbele ya yeyote. Na ndio maana pale shuleni nilikuwa miongoni kwa wanafunzi tunaopiga Pisikali na washindani wangu niliwakalisha.

Hii ni kwaajili ya vijana wadogo mliopo shule.

Jikubali ili ujitambue.
Kamwe usiukatae ukweli/uhalisia.

Jua ulipotoka lakini ulipotoka(Past na BACKGROUND) isiwe ndio muongozo wako.

Unapokwenda (ndoto na future zako) ndio iwe muongozo wako.

Usipange mambo kwa mihemko bila kuangalia uhalisia.

Elewa binadamu ni kiumbe mbinafsi na ambaye mara nyingi hataki umzidi.

Mtu yeyote ambaye anatumia Past yako kuhukumu present yako(wakati uliopo wako au wakati ujao wako) huyo ni adui yako.

Mfano mtu anakuambia, wewe kila siku biashara inakushinda, yaani wewe hakuna biashara utafanya ukafanikiwa.

Au wewe mapenzi yalishakushinda, ni bora ujiachie.

Kamwe kwenye maisha yako usikubali kuwa mtu wa kushindwa. Usikubali adui zako wawe katika sikio lako.

Yeyote ambaye umempa access ya sikio lako umempa nguvu ya kuamua future yako kwa kiasi kikubwa.

Hautakuwa nafuraha kwa kutaka kuwafurahisha waliokuona wewe ni mtu wa kushindwa. Huwezi kufurahi kwa kuwafurahisha adui zako. Yaani kufanya kile adui zako wanachokitaka.

Adui ni mtu yeyote ambaye hataki ufanye kinachokufurahisha wewe hata kama sio uhalifu au dhambi.

Mfano, kuna Watu wanapenda ku-post Wenza wao kwenye mitandao.

Hicho kinawapa furaha. Pia wapo Watu wanaopenda maisha ya mitandao hicho ndio kinawapa furaha. Lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu ati kima fulani hawataki wafanye hivyo. Wakati jambo hilo sio dhambi wala sio uhalifu. Hilo ni kosa.

Usiwe mtu wa kujali mawazo na maoni ya Watu wengine. Huko ni kuwapa Watu umuhimu ambao hawana kwenye maisha yako.
Yaani kile kitendo cha kuwaza nikifanya hivi Watu watanionaje tayari wewe ni miongoni mwao Watu wasio na furaha Duniani.

Kuwapa Watu umuhimu hasa wale ambao wewe hawaoni umuhimu wako huko ni kujitesa tuu.

Ukifanya jambo lolote zingatia haya;
1. Unalipenda kwa dhati? Hii itakupa furaha.

2. Je ni kosa kisheria? Hii itakupa ulinzi na usalama.

3. Matokeo yake kwako yatakuwa yapi? Hii itakupa assurance.

4. Je litaathiri Watu wako wa muhimu kama Mkeo, watoto na wazazi? Hii itazidisha furaha yako.

Maana furaha inakua zaidi pale wahusika wako wa muhimu wakifurahia.

Elewa kuwa wewe ni mtu bora. Na upo kwaajili ya kupata vitu bora.

Usijidharau.

Uache kuishi Vizuri kisa Past na background yako ambayo mara nyingi adui zako wanapenda sana kuitumia kukunyanyasa na kukandamiza. Usikubali.

Ilishatokea ilishatokea. Lakini kamwe haitajirudia.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ni ukweli mtupu...
Binafsi Toka nianze kuish leo kila siku ..
Maisha yangu yamebdlika kwa kiasi kikubwa
 
Ujumbe mswanu
 
Back
Top Bottom