Taka zinazomwagwa Baharini

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Ndugu zangu

Jioni hii rafiki yangu mmoja amenitumia Barua pepe akilalamika kuhusu Maji machafu yanayopita Kwenye mabomba makubwa chini ya ardhi kwenda kumwagwa baharini , rafiki yangu huyu analalamika kwamba zile taka huwa hazimwagiwi dawa ili kuuwa wadudu kabla ya kumwangwa baharini kama ilivyo maeneo mengine ya nchi nyingi .

Mbaya zaidi ni kitendo cha mmoja wa viongozi alietakiwa kwenda kuangalia eneo hilo kushindwa kushusha miguu yake kutokana na usalama wake alikaa Kwenye gari yake akapewa taarifa akiwa ndani ya gari kisha akaondoka zake

Sasa mimi siko Kwenye masuala ya mifumo ya maji taka na sina taarifa nyingi kuhusu maeneo hayo ila siku za karibuni niliona picha Kwenye gazeti moja la Kiswahili mafundi wa kichina wakitengeneza mabomba ya maji machafu kwenda baharini sijui huu mradi umefikia wapi .

Tukiacha hayo kusema za ukweli eneo la feri kwa mfano ambalo watu wengi wanaogelea pamoja na kigamboni kama kweli taka zile zinatupwa bila kuuliwa vijidudu ni hatari kubwa sana kwa afya za watu wanaotumia habari hiyo
 
Back
Top Bottom