Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 736
Haya tena weekend ijayo kutakuwa na mtanange kati yetu na Morroco pale National Stadium na hii itakuwa mechi ya pili ya kimashindano ya kocha Poulsen baada ya ile ya sare ya 1-1 dhidi ya Algeria and I hope tutaondoka na point (s) kama tukikaza msuli...
TIMU ya Taifa ya Morocco inatarajiwa kuwasili nchini Oktoba 8, mwaka huu tayari kwa mchezo wa awali wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2012 dhidi ya Taifa Stars.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kwenye mtandao wa Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF), kikosi hicho kitatua nchini kikiwa na wachezaji 22 akiwemo Marouane Chamakh wa Arsenal ya England ambao watacheza dhidi ya Taifa Stars Oktoba 9, mwaka huu.
Wachezaji wanaotarajiwa kuwasili nchini siku hiyo ni makipa Karim Fegrouch (Wydad Casablanca), Nader Lamyaghri (Wydad Casablanca) na Ahmed Mouhamadina wa Olympique Khouribga.
Wengine ni mabeki Mehdi Benatia (Udinese), Adil Karrouchy (Difaa El Jadida), Fettah Boukhris (FUS Rabat), Morad Ainy (Raja Casablanca), Rachid Soulaimani (Raja Casablanca), Michael Chrétian Basser (AS Nancy), Chakib Benzoukane (Sofia) na Hicham Mahdoufi wa Raja Casablanca.
Viungo ni Adil Hermach (RC Lens), Mohamed Berabeh (Al Dhafra), Issam Erraki (Al Wahda), M'bark Boussoufa (Anderlecht), Karim Al Ahmadi (Feynoord Rotterdam) na Nabil El Zhar wa Liverpool.
Washambuliaji ni Mounir El Hamdaoui (Ajax Amsterdam), Chamakh, Youssef El-Arabi (Caen), Adil Taarabt (Queens Park Rangers) na Youssef Hadji wa AS Nancy.
Kocha wa timu hiyo, Mfaransa Dominique Cuperly amejigamba kuwa atahakikisha anaibuka na ushindi katika mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.