Taifa Stars vs Morroco October 9 2010

Status
Not open for further replies.
drogba na ramirez(wa chelsea) walishatufunga,sijui chamakh nae atakuwa na hasira za kushindwa kuwafunga chelsea j2 iliyopita atamaliza hasira zake bongo
Huyo usimuwazie maana kuna wengine wamefika hapa wakachemka,kumbuka hii si friend match halafu na sisi tunae Nizar,Ngasa,Henry ambao nao wanawahofia pia na unaijua defence yetu hasa tunapokutana na timu kama hizi nyumbani.
 
Jama kitu kinaonyeshwa SUPER SPORT 3 kuanzia saa 9:30 jioni, wadau na wapenzi wa mpira habari ndio hiooooooooo.
 
Washambuliaji ni Danny Mrwanda (DT Long An-Vietnam), Mohammed Banka (Simba), Mrisho Ngasa na John Bocco (Azam).

Hii safu ya washambuliaji iimarishwe siku zijazo. Poulsen amfuatilie Machupa huko aliko. Yuko kwenye form nzuri sana ..
 
MAHUDHURIO hafifu ya mashabiki katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa baina ya Taifa Stars na Brazil uliofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Juni mwaka huu yameleta mageuzi mapya kwenye masuala ya viingilio hapa nchini.

Mchezo huo wa Juni uliohudhuriwa na mashabiki kiduchu tofauti na wengi walivyodhania Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilipanga kiingilio cha juu Sh 200,000 na cha chini ni Sh 30,000.

Kwa kawaida michezo mingi inayofanyika kwenye uwanja huo, kiingilio cha juu huwa ni Sh 50,000 wakati kile cha chini huwa ni Sh 3,000 ama Sh 5,000, lakini wakati huo TFF ilisema kulingana na gharama kubwa za kuileta Brazil nchini ndio sababu waliweka viingilio vikubwa.

Jana TFF ilitangaza kuwa mchezo wa Jumamosi ijayo kati ya Taifa Stars na Morocco utakaofanyika kwenye uwanja huo kuwania kufuzu fainali za Afrika mwaka 2012 kiiingilio cha juu ni Sh 30,000 wakati cha chini ni Sh 5,000 na hiyo ni kutokana na fundisho walilopata kwenye mechi ya Stars na Brazil.

Mechi ya Stars na Brazil viingilio ilikuwa Jukwaa la Viti Maalum A (VIP A) Sh 200,000, VIP B Sh 150,000, VIP C Sh 100,000.

Jukwaa la Rangi ya Chungwa Mkabala na VIP Sh 80,000 na Jukwaa la Rangi ya Chungwa nyuma ya magoli shilingi 50,000 na Jukwaa la Rangi ya Bluu Mzunguko pamoja na Jukwaa la rangi ya kijani sehemu hizo ilikuwa Sh 30,000.

Kwa mazingira hayo mashabiki wa soka wenye vipato vya chini maarufu kama wenye uchungu na mpira walitakiwa kujikamua zaidi ili wafike uwanjani, lakini walikwama matokeo yake waliangalia kupitia televisheni zaidi, hivyo uwanja ukajaa wenye nacho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Rais wa TFF Leodegar Tenga alisema kitendo cha kupandisha kiingilio cha chini katika mechi ya Stars na Morocco kutoka Sh 5,000 hadi Sh 30,000 kiliwatenga wapenzi wengi wa soka na kuwa matokeo yake viti vingi vilibakia wazi.

Tenga alisema hali hiyo haitotokea tena katika michezo ijayo ya kimataifa na kuwa ana matumaini viingilio vilivyotangazwa jana vitakuwa nafuu kwa mashabiki.

Kwa upande wake Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage alitaja viingilio hivyo kuwa ni Sh 30,000, Sh 20,000, Sh 15,000, Sh 7,000 na Sh 5,000.

Alieleza kuwa Morocco inatarajiwa kuwasili kesho saa nne usiku na kuwa mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka Mauritius ambao ni Sochurn Raji, Botun Barkishna na Vally Vivian, wakati Kamishina atakuwa Mohammed Aziz kutoka Kenya.

Rekodi ya juu ya mapato yanayotokana na viingilio iliwekwa Septemba mwaka 2007 kwenye uwanja huo huo, wakati wa mchezo wa mwisho wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kati ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' na Msumbiji, ambapo kiasi cha Sh 605,020,000 kilipatikana kati ya Sh 644,530,000 zilizotarajiwa kupatikana.

Kulikuwa na upungufu wa Sh 39,510,000 uliotokana na viti 1,612 ambavyo tiketi zake zilidaiwa hazikuuzwa. Kiingilio kilikuwa Sh 50,000, Sh 40,000, Sh 30,000 Sh 20,000, Sh 10,000 na Sh 3,000.

Lakini rekodi hiyo ilivunjwa Juni katika mchezo wa Stars na Brazil ambapo kiasi cha Sh bilioni 1.6 kilipatikana.

Uwanja huo una uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 walioketi kulingana na takwimu zilizotolewa mwaka 2007 na aliyekuwa Mkurugenzi wa Michezo, Henry Ramadhan, siku chache kabla ya mchezo wa Taifa Stars na Msumbiji.

Kama mambo yangeenda kama TFF ilivyopanga kwenye mchezo wa Stars na Brazil ingevuna zaidi ya Sh bilioni 2.7, kwani kwa kiingilio cha Sh 200,000 kwa jukwaa kuu A (VIP), ambalo lina viti 748, zingepatikana Sh 149, 600,000.

Jukwaa B kiingilio cha Sh 150,000 na kuna viti 2,260 zingepatikana Sh 339,000,000, huku Jukwaa Kuu C kwa kiingilio cha Sh 100,000 na kuna viti 2,404 zingehifadhiwa Sh 240,400,000.

Jukwaa la rangi ya chungwa linaloangalia jukwaa kuu kwa kiingilio cha Sh 80,000 na kuna viti 6,460, kiasi cha Sh 516, 800,000 kingepatikana, huku majukwaa ya nyuma ya magoli, ambapo kiingilio ni Sh 50,000 na kuna viti 7, 300 zingepatikana Sh 365,000,000.

Jukwaa la bluu mzunguko lenye viti 18,364 kiingilio cha Sh 30,000 zingepatikana Sh 550,920,000, wakati jukwaa G ambalo lina viti 19,590 linalojulikana pia kama jukwaa la kijani, ambalo ndilo Watanzania walio wengi hujihifadhi hapo kwa kiingilio hicho cha Sh
30,000 basi zingevunwa Sh 587,700,000.

Kama zingeuzwa tiketi zote kiasi cha 2,749,420, 000 kingepatikana, ambapo kihesabu ni sawa na kusema Sh bilioni tatu.

Lakini kwa vile wangekuwepo watu wachache wangeingia bure kutokana na sababu mbalimbali, inawezekana labda kungekuwa na upungufu wa Sh milioni 200.
 
6.jpg


Jan Poulsen akiwaandaa wachezaji wake kwa ajili ya mpambano huo.

KOCHA wa Taifa Stars, Jan Poulsen, leo asubuhi alinaswa na paparazzi wetu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, akikiandaa kikosi chake na mpambano huo.




Wachezaji wa Stars wakijifua.





Nizar Khalfan (mwenye rasta) akimpeleka puta Haruna Shamte wakati wakijifua leo asubuhi.


Ni mazoezi ya kufa mtu.


 

TIMU ya taifa ya Morocco a.k.a Simba wa Milima ya Atlas, jana usiku iliwasili nchini kwa ajili ya kuivaa timu ya taifa, Taifa Stars, pata mipicha ya Simba hao walipowasili Uwanja wa Ndege Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA) wakati timu hiyo ikiwasili, CHAMAKH ndani ya nyumba... Hawa wwarabu lazima tuwanyuke 2-1

 
Msiende kumuangali Chamakh tu na kusahau chama lenu ohooo
 
mm wala siangalii maana nnajua waaarabu wana hasira baada ya kutaka kumjeruhi mwenzao

leo ni kipigo cha paka mwizi
 
hi dear brothers i am from Morocco
any one can give me a video or photos about the Moroccan and Tanzanian preparation for sunday game
thanks
 
It is now official the game will be live broadcasted on Supersport 3 channel, the match commentary will begin at 14:30 Central African time!
 
drogba na ramirez(wa chelsea) walishatufunga,sijui chamakh nae atakuwa na hasira za kushindwa kuwafunga chelsea j2 iliyopita atamaliza hasira zake bongo
Wachezaji wa kuwaangalia kwa jicho la tatu hapo (iwapo watacheza ) ni el Hamdaoui na huyo winga el Zhar, Chamakh hatishi kama haletewi mipira yake ya kichwa, footwork hana hivyo mipira ya chini anakuwa wa kawaida tu. Yousef Hadj naye sio mbaya na mbio zake..maana ikumbukwe wamoroko wanakwenda mbio kama kishada kwa sababu mbio is also their pride sport.
 
It is now official the game will be live broadcasted on Supersport 3 channel, the match commentary will begin at 14:30 Central African time!

SS BROADCAST DETAILS
Saturday: Tanzania vs Morocco, SS3 and SS9, 3pm (CAT).
Kwa hapa bongo ni saa 10 jioni (16h00)
 
Nataka nkanunue leo ijumaa tiket. Naomba orodha ya maeneo naweza pata tiket halali sio zilizochakachuliwa!
 

Nyota wa timu ya taifa ya soka, Taifa Stars, wanaojiandaa na mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika 2012 dhidi ya Morocco Jumamosi, wameahidi kuwashangaza wageni wao huku Mrisho Ngassa akiwataka Watanzania wasubiri raha.

Winga mwenye kasi, Mrisho Ngassa aliwataka Watanzania watarajie raha kwa sababu timu imejiandaa vyema, ingawa alionya kwamba mafanikio yatahitaji ushirikiano wa wachezaji katika kushambulia na kuzuia. Alisema kuwa ni vizuri kama mashabiki watajitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Taifa ili kuwapa sapoti ya ushangiliaji wakati wa mchezo huo.
Beki wa kati wa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro' alisema licha ya kwamba Morocco ina wachezaji wengi wanaocheza Ulaya, Stars haitaingia uwanjani kiunyonge.
"Tumeshapata uzoefu kwa kucheza na wachezaji wakubwa, unakumbuka walikuja Brazil, Ivory Coast, Cameroon na kadhalika, kwa hiyo Morocco hawatutishi," alisema Cannavaro.
Morocco inayoundwa na nyota kibao akiwemo Marouane Chamakh wa Arsenal na El Hamdoaui wa Ajax, ilitarajiwa kuwasili usiku wa kuamkia leo ikitokea Amsterdam, Uholanzi tayari kwa mechi yao hiyo ya pili ya Kundi D, itatakayoanza saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa.
Katika mchezo ya Stars ilitoka sare ya 1-1 ugenini kwa Algeria, wakati Morocco walilazimishwa sare ya 0-0 nyumbani kwao dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom