Taifa Stars chini ya TFF yaunga mkono Kampeni ya 'Piga Mpira Usipige Mwanamke'

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ chini ya uongozi wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) wanaunga mkono Kampeni ya PIGA MPIRA SIO MWANAMKE.

Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali THAMANI WOMEN TANZANIA

(thamani.tz) inaendesha kampeni hiyo ya kupaaza sauti dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na vilabu tofauti vya Mpira wa miguu kama Simba SC,Singida Fountain Gate na Azam FC.

Mwanzilishi wa THAMANI, Nafue Nyange akihojiwa juu ya Kampeni ya PIGA MPIRA SIO MWANAMKE amesema “Jana tumemaliza siku 16 za Harakati dhidi ya ukatili kwa Wanawake na Watoto wa kike. Mbali na hizi siku 16 ukatili kwa makundi haya mawili ni janga la kila siku.”

“Hivyo, ni jukumu la kila Mwananchi kila siku kupinga na kukataa ukatili wa kijinsia. Maendeleo ya Taifa letu yanachangiwa kwa asilimia kubwa sana na Wanawake na Watoto, ndio ambao tunawategemea kuwa viongozi na wajenzi wa Taifa letu kesho.

“Ni wazi kwamba Ukatili kwa makundi haya mawili yanaturudisha nyuma sasa na vilevile baadaye. Ni muhimu sana Wanaume na vijana wa kiume wahusishwe katika shughuli mbalimbali za kutokomeza ukatili wa kijinsia.

“Ni muhimu kuwakumbusha kuwa wao ni part of the solution not the problem.”
 
Wanyakyusa tulikuwa tunasema koma amisi mwana ubukeghe kusukulu,kabla ya hapo walikuwa wanasema koma amisi bana bendeghe kitali yaani kunywa pombe watoto waende shule kabla yapo walikuwa wanasema kunywa pombe watoto watembee uchu Now they are very advance and creative it is a society of critical thinkers
 
Nadhani kutokana na issues ambazo zinaligharimu taifa kipindi hiki ni Upigaji wa Pesa za UMMA..., wangesema Serikali Piga Kazi Usipige Kodi za Wananchi
 
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ chini ya uongozi wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) wanaunga mkono Kampeni ya PIGA MPIRA SIO MWANAMKE.

Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali THAMANI WOMEN TANZANIA

(thamani.tz) inaendesha kampeni hiyo ya kupaaza sauti dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na vilabu tofauti vya Mpira wa miguu kama Simba SC,Singida Fountain Gate na Azam FC.

Mwanzilishi wa THAMANI, Nafue Nyange akihojiwa juu ya Kampeni ya PIGA MPIRA SIO MWANAMKE amesema “Jana tumemaliza siku 16 za Harakati dhidi ya ukatili kwa Wanawake na Watoto wa kike. Mbali na hizi siku 16 ukatili kwa makundi haya mawili ni janga la kila siku.”

“Hivyo, ni jukumu la kila Mwananchi kila siku kupinga na kukataa ukatili wa kijinsia. Maendeleo ya Taifa letu yanachangiwa kwa asilimia kubwa sana na Wanawake na Watoto, ndio ambao tunawategemea kuwa viongozi na wajenzi wa Taifa letu kesho.

“Ni wazi kwamba Ukatili kwa makundi haya mawili yanaturudisha nyuma sasa na vilevile baadaye. Ni muhimu sana Wanaume na vijana wa kiume wahusishwe katika shughuli mbalimbali za kutokomeza ukatili wa kijinsia.

“Ni muhimu kuwakumbusha kuwa wao ni part of the solution not the problem.”
Sawa...
Ila hela ya watoto mbona ina figisu?!
Kunani?!
Yale yale ya kina Malinzi nk nk?!
 
Back
Top Bottom