Taifa lilipotekwa Nyara, Usalama wa Taifa walikuwa wapi?

MMK,
Mtalii alikutuhumu hapa kwamba unajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya kwenye ile thread ya Mtanzania aliyeuwawa UK, nilikuomba utoe tamko kuhusu tuhuma hizo lakini hadi leo umekaa kimya, I think we should all practise what we are preaching here.

NB:UGAIDI and not UGHAIDI- Apart from that, a very good article I must say, congratulations!I wish I could write like you.

kwanini usimuulize huyo jamaa akuambie ushahidi alionao kwamba nahusika na madawa ya kulevya? jibu gani la kwangu litakuridhisha litakufanya uniamini nitakachokuambia? Na mimi nikikutuhumu kuwa unajihusisha na kusafirisha watoto wa kike kwa Umalaya Thailand, utanithibitishia vipi kuwa huhusiki?
 
kwanini usimuulize huyo jamaa akuambie ushahidi alionao kwamba nahusika na madawa ya kulevya? jibu gani la kwangu litakuridhisha litakufanya uniamini nitakachokuambia? Na mimi nikikutuhumu kuwa unajihusisha na kusafirisha watoto wa kike kwa Umalaya Thailand, utanithibitishia vipi kuwa huhusiki?

Duh kumbe kuna mambo humu!yah ngoja tuendelee kuona maana it takes one to know one like it takes a thief to catch a thief ,Ok back to the topic which is cheif consideration ,tukiitazama Act ya 1996 kama inavyosomeka hapo chini;
Tunaona kuwa TISS ina protocol ilizowekewa katika kutoa taarifa zake za shughuli zake kwa authority iliyoko chuu yake ambapo ni pamoja na rais moja kwa moja.Hivyo kufanyia kazi taarifa hizo inakuwa ni juu ya malaka hizo husika ingawa kiongozi TISS ana haki ya kujiuzulu akiona mambo ya msingi aliyo ripoti hayachukuliwi hatua.Hivyo basi nionavyo mimi na ndio maoni yangu siku zote ni kuwa bila utawala bora hakuna iliatakalo endelea ktk taifa hili ,utatimiza wajibu wako kama Director wa TISS ila watawala watakwambia hewara taarifa zimefika ukizidi kuhoji na wewe unaandikiwa check yako kupoozwa ,ukigoma unatemwa chapchup,au unatengenezewa kibano nadhani mnakumbuka aliyefanananishwa jambazi na kumiminiwa risasi akiwa safari kwenye gari yake.


CHECK ATTACHMENT TO READ THE TISS 1996 ACT
 
Hii makala ni Nzito sana na huo ndio ukweli tuna safari ndefu kuelekea kwenye maendeleo.

Hivi nikumbushe labda nimekosea, USALAMA wa TAIFA si ni WAZEE na VIJANA wakereketwa wa CCM? Kuna Mtu anaweza kutokuwa ktk kundi hili awe usalama?

Kazi zao pamoja na kuainishwa zinaenda tofauti na masirahi ya chama?

Tutegemee nini kutoka kwao?

Zamani ilikuwa ni vigumu kujua watu wa USALAMA siku hizi kila unayemjua ukichungulia unamuona amekaa nyuma ya Bendera ya kijani. Huwa najiuliza, Je tuwabadilishe jina? Je wale wataifa ni lini watakuwepo?

Usalama haujakaa kusaidia taifa, umekaa kuasidia kundi la watu fulani, sasa ktk kama kundi linalohujumu nchi lina baraka za chama na hilo kundi ndo limeteka nchi basi inabidi usalama wakae upande wa wateka nyara. Inawezekana Mkulu wa Polisi ameliona hili na ndilo bomu linalohujumu nchi yetu

Kama wanafanya kazi kulikoni mabilioni yateketee/yatoweke? Halafu waliyoyatorosha bahadhi wana ulakini na uraia wao. Usalama walikuwa na uhakika gani kama haikuwa ni ugaidi?, mbona walikaa kimya mpaka raia wema walipo ingilia kati?
 
kwanini usimuulize huyo jamaa akuambie ushahidi alionao kwamba nahusika na madawa ya kulevya? jibu gani la kwangu litakuridhisha litakufanya uniamini nitakachokuambia? Na mimi nikikutuhumu kuwa unajihusisha na kusafirisha watoto wa kike kwa Umalaya Thailand, utanithibitishia vipi kuwa huhusiki?

Tuhuma utupiwe wewe halafu shughuli ya kutafuta ushahidi inipate mimi? Kwani mi polisi au hakimu? Ulipaswa utoe tamko kuhusu hilo suala,hukuwa na haja ya kutoa ushahidi- kukanusha tu ingetosha. Ningefanya hivyohivyo kama ungenituhumu hapa kwa chochote.
 
MMK,
Mtalii alikutuhumu hapa kwamba unajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya kwenye ile thread ya Mtanzania aliyeuwawa UK, nilikuomba utoe tamko kuhusu tuhuma hizo lakini hadi leo umekaa kimya, I think we should all practise what we are preaching here.

NB:UGAIDI and not UGHAIDI- Apart from that, a very good article I must say, congratulations!I wish I could write like you.

kana-Ka-Nsungu bwana wewe unatamani alafu tena sijui....

Wewe naona unataka kuzaliwa na Nzungu nini(Tanzania imekushikushinda) maana ni kutamani tamani tu (joke)
 
Tuhuma utupiwe wewe halafu shughuli ya kutafuta ushahidi inipate mimi? Kwani mi polisi au hakimu? Ulipaswa utoe tamko kuhusu hilo suala,hukuwa na haja ya kutoa ushahidi- kukanusha tu ingetosha. Ningefanya hivyohivyo kama ungenituhumu hapa kwa chochote.

aliyetoa tuhuma muulize ushahidi
 
Mimi nadhani kazi ya usalama wa taifa ni jukumu la raia wote wa Tanzania.

Kile kitendo cha kuwaachia kazi hio watu wachache ndio huwafanya wajisahau na kunogewa na UFISADI. Watu wanaochaguliwa kufanya kazi hio wapo pale ka ajili ya "operations" ambayo inatokana na msaada wa raia wema.

Kazi hio inaonekana kama ndio "lifeline" kwa baadhi ya watu lakini hao wachache ambao siku hizi wanaingia kwa njai ya undugu hujiona kwamba wameula na kusahau wajibu wao wa taifa ambalo mpaka watu wanavusha mapesa pale DIA wao wanakuwa wanafikiria "trip" za nje na matanuzi mengine.

Lazima ieleweke kwamba jambo lolote la kulinda maslahi ya taifa ziku zote hushirikisha wananchi wote na linakuwa "intelligence led" na raia wema.
 
Makala hii imetoka kwenye gazeti la Tanzania Daima (hard copy) lakini kwenye mtandao haikuwekwa.

TAIFA LILIPOTEKWA NYARA, USALAMA WA TAIFA WALIKUWA WAPI?​
Na. M. M. Mwanakijiji

Nirudi kidogo kwenye suala la EPA na madai kuwa yawezekana Tanzania iko mikononi mwa maghaidi.

Uwezekano kuwa nchi yetu iko mikononi mwa maghaidi na kuwa vyombo vyetu vya usalama vinatambua hivyo, ni uwezekano ambao lazima umshtue Mtanzania yeyote yule kwani kama ni kweli, basi tunachopigania siyo hali yetu ya maisha ya kuwa huru na wenye kufanikiwa bali tunapigania uhai wetu kama Taifa.

Tunahiyaji macho ya kuona kinachotakiwa kuonwa! Na kuchukua hatua sahihi.. We are n bad shape..!..Hakika kama tukiendeleea kurembuliana hapa ..ni kweli hatuna Taifa..watch this also!! https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=13611
 
watakuwa wamelala kabisa hawa , au hawapo, au wapo kama sanamu, au nao mafisadi, au...au.

Tangu swali hili lilipoulizwa mpaka leo mafisadi wanatuzomea!
 
Kwa upeo wangu mdogo niliyo nayo naamini kwamba Usalama wa TAIFA hawafanyi kazi kama wanavyo takiwa .Hii ni kwasababu wengi walipewa kazi kwa kujuana hawajui kwanini wanafanya kazi hiyo ,hawana malengo ya kufanya kazi kwa ufanisi ,hawakotayari kufa kwa kuilinda TANZANIA ila wako tayari kulinda wenzao wanaoendeleza ufisadi.
Hawa jamaa hawako huru na matakwa ya kazi yao .Wanaishi kwa uoga na kuogopana badala ya kufanya kazi inayotakiwa.Sijui ni vigezo zipi zilizo waingiza au vilivyo wafanya wachague kazi hizo au wachaguliwe.Lakini naamini ni kufaamiana na waliomo pia mtindo wa kubebana ambao ndio umearibu mfumo mzima wa uongozi.
Watu wenye uchungu kulinda inchi hawapo ila kulinda mwenye nacho .
Lazima huu mfumo ubadilishwe ndipo utawala utabadilika na kufata kanuni na taratibu za kazi pia haki hapo ndipo itatendeka lakini kwa kuangalia ujamaa,Urafiki ,undugu,pia na ujirani.Taasisi hiyo itabakiwa kuwa na jina siyo faa.
Wengi wao elimu zao ni za kujidai na kujikweza kwamba wapo mle wanafanya kazi.
Tanzania bado tunatakiwa tufundishwe jinsi ya kuwa na uchungu na inchi yetu bila hivyo utasikia siku moja tunatawaliwa na mkenya au mkenya kapewa mkuu wa wilaya
 
Mhh! kaka naona kweli leo 'umefyatuka!' maana hayo makombora ya masafa ya mbali 'unayofyatua' si mchezo.....semax2 kaka kitoto cha anza tambaa....kesho kitatembea...who knows keshokutwa kita paa!!

Weldone MM.Mwanakijiji,Rev.Kishoka.
 
Sasa umeamua kuwafuata watu wa Usalama wa Taifa? Hawa hawaguswi na hawagusiki, walioliteka taifa siyo mafisadi wa EPA.. tumia akili kchwani...Nusura upatie...

asante.

Usalama wa Taifa hawaguswi??

Kwa nini Bosi wa zamani wa Usalama wa Taifa, Kombe walimuondoa Roho yake kama mbuzi mwitu??

Kam wao kweli hawawaguswi kwa nini wanahangaika sana na kugombea ubunge?? Bunge limejaa mishushu kila kona??

Huko usalama hakuna kitu na wala si mahali pa kujidai kwa nguvu zote kwamba ukiwa huko basi huguswi?
Usalama wa taifa wamejiingiza kwenye uharamia, wanahusika moja kwa moja na wizi wote mkubwa uliotokea Tanzania.
 
Idea nzima ya "taifa" imetungwa na hao "Usalama wa Taifa" -literati, intelligentsia na illuminati, ili kuweza kukufunga wewe vizuri huku ukifikiri kwamba una "taifa" huku wanakunyang'anya uhuru wako na kukutoza kodi wakati huo huo.

Huku unawashukuru.
 
Last edited:
Mkuu heshima kwa mbele,

Yaani uchambuzi huu umetulia, hongela mzee kwa uchambuzi makini
 
Kuwauliza usalama wa Taifa, PCCB, POLISI n.k ni sawa na kwamba wewe na wanao mpo ndani, unawaambia watoto lindeni mali za nyumba hii ali hali huwaambii nini ambacho wanakilinda.

Mara kwa mara baba na mama mnakuwa mnaingia na wageni ndani ya nyumba, watoto hawajui ni akina nani, na nini kinaendelea humo ndani, na watoto umewambia kuwa kuuliza nini kinaendelea ndani ni utovu wa nidhamu, mtoto umeamuliwa kufuata like utakachoamriwa tu.

Mara watoto wanapata taarifa kuwa ndani ya nyumba pesa zimeibiwa. Utajiuliza nani kaiba na hali muda wote wewe umekuwa ukilinda!!

Baba na mama hawataki kuongelea wizi uliotokea. Usalama wa Taifa, PCCB ni watoto wa baba. Baba amewawekea mipaka ya ulinzi na kazi zao. Upeo wao sidhani ni mkubwa kuweza kuchanganua yanayoendelea humo ndani. Usiri na vitisho vya baba vinawafanya watoto wawe wapole kama kondoo wa sadaka.

Baba amejiwekea kizuizi kwamba hawezi kushutumiwa na kushitakiwa kwa wizi, na alikubaliana na watoto wake, wangali hawajui baba anamipango gani.
Nani ategue kizuizi?? Wanaoweza kutegua ndio wale baadhi walikuwa mle ndani na baba.

Tanzania ipo kwenye koma. Sijui nani atainusuru na umauti unayoinyemelea. Nikiangalia nchi nyingine angalau zina sense kuwa wanahitaji kuamka, kuendeleza jamii na kutetea haki za wazawa wao, nahisi nakuwa mkimbizi nchini mwangu. Magaidi wameiteka nyara nchi, Gaidi ni nani? ni raisi na viongozi wenziwe ambao wamechukua pesa zote ndani ya nchi. Jamanii?? ni aibu sana.
 
Back
Top Bottom