Mossad walikuwa wapi nchi inashambuliwa kwa style ile ile kwa mara ya pili? Unguli wao ni propaganda tu?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,224
12,729
Mwaka 1973 Israeli ilishambuliwa na Misri na Syria kwa kushtukizwa wakati wa majira ya sikukuu ya Yom Kippur. Misri walivuka mfereji wa Suez na kuingia Israel(Sinai). Wasyria nao wakaingia huko Golan.

Hali ilikuwa tete sana kwa Israel hadi jeshi likaamua kuwa liwaache Wasyria wafanye wanavyotaka wao wadeal na mwenye nguvu, Misri.

Ukiisoma ile vita, habari za kijasusi kuhusu vita kutoka Mossad na MI ziliwafikia wakubwa mapema. Lakini siasa zilifanya wawe wazito kuchukua maamuzi.

Kwenye Movie Golda(2023), Waziri mkuu wa wakati huo, Golda Meir anasikika akisema kuwa kumobilize jeshi wakati wa sikukuu za Yom Kippur ni kutaka kujiua kisiasa na kuwapa wapinzani cha kusema.

Kwenye demokrasia, maamuzi makubwa, hata yanayohusu usalama wa nchi hutanguliza kwanza maslahi ya kisiasa kisha ya nchi ndiyo yanafuata.

Idara za ujasusi za Israeli zilishutumiwa vikali sana baada ya vita ya Yom Kippur, lakini ni ngumu sana idara hizi kufanya kazi zake vizuri kwenye mazingira ya kidemokrasia.

Jana tena, kwenye msimu wa Yom Kippur, asubuhi ya sabato Israel imeshambuliwa na Hamas kwa style ile ile ya 1973. Miaka 50 ya kumbukumbu ya vitw ya Yom Kippur!!. Tena imeshambuliwa baada ya kutokea machafuko makubwa ya kugombania "siasa" ndani ya Israeli.

Si rahisi kwa chombo kama Mossad kutofahamu kuhusu shambulio lililotokea jana. Lakini ni wanasiasa ndiyo wanaofanyia kazi taarifa za kijasusi. Na wanasiasa wanafanya maamuzi kwa kutanguliza maslahi ya kisiasa mbele.

Maoni yangu: Siasa za kidemokrasia ni hatari kwa usalama wa nchi. Zinaweza kukwamisha hata kazi za taasisi bora kama Mossad.
 
Zipo sababu nyingi israel alijua kuhusu hili shambulio na kuacha litokee ili apate kuifuta gaza aichukue na kuingia vitani na iran, pia kisiasa kuwatuliza wananchi waliokuwa wanaandamana
Jamii ya kimataifa, hata US yenyewe haiwezi kubali gaza kufutwa. Unaongelea zaidi ya watu milioni 2.
 
Maono kuhusu dunia kutochukua hatua dhidi ya wanaofadhili magaidi

22 September 2023
UN HQ, New York

Hotuba mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA : Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu 2023.


View: https://m.youtube.com/watch?v=kNH85jgzJ0Y
Asante Mheshimiwa Rais!
Mabibi na mabwana, zaidi ya milenia tatu zilizopita, kiongozi wetu mkuu Musa, alihutubia watu wa Israeli walipokuwa karibu kuingia katika nchi ya ahadi. Alisema wangekuta milima yao miwili ikitazamana. Mlima Gerizimu, mahali ambapo baraka kubwa ingetangazwa, na Mlima Ebali, mahali pa laana kuu.


Musa alisema kwamba hatima ya watu ingeamuliwa na uchaguzi waliofanya kati ya baraka na laana. Chaguo lile la enzi ya Musa, limekuwa likijirudia enzi na enzi, si kwa watu wa Israeli pekee. Lakini kwa wanadamu wote. Tunakabiliwa na chaguo kama hilo leo. Chaguo letu litaamua ikiwa tunafurahia baraka za amani ya kihistoria, ya mafanikio na matumaini yasiyo na mipaka, au tutapata laana ya vita vya kutisha vya ugaidi na kukata tamaa.

Nilipozungumza mara ya mwisho kwenye jukwaa hili hili la UNGA miaka mitano iliyopita, nilionya kuhusu madhalimu wa Tehran. Wamekuwa ni laana, laana kwa watu wao wenyewe, kwa eneo letu, kwa ulimwengu mzima. Lakini wakati huo, nilizungumza pia kuhusu baraka kubwa ambayo ningeweza kuona kwenye upeo wa macho.

Hivi ndivyo nilivyosema. Nanukuu: "Tishio la kawaida la Iran limeifanya Israeli na nchi nyingi za Kiarabu kuwa karibu zaidi kuliko hapo awali katika urafiki ambao sijawahi kuuona maishani mwangu."

Nilisema: “Siku ingefika hivi karibuni ambapo Israeli ingeweza kupanua amani nje ya Misri na Yordani hadi kwa majirani wengine Waarabu.” Mwisho wa kunukuu.

Sasa, katika mikutano isiyohesabika na viongozi wa dunia, nilitoa hoja kwamba Israeli na mataifa ya Kiarabu yalishiriki maslahi mengi ya pamoja, na kwamba niliamini kwamba maslahi haya mengi ya pamoja yangeweza kuwezesha mafanikio ya amani pana katika eneo letu la Mashariki ya Kati

Makofi

Asante (kwa makofi) . Naam, mnapongeza sasa kwa makofi . Lakini wakati huo, wengi walipuuzia matumaini yangu kudhani kuwa ni ndoto za kufikirika. Kukata tamaa kwenu kulitokana na robo karne ya nia kuwepo kupatika amani , na ikashindikana. Na kwa nini amani ilifeli? Kwa kulikuwepo nia njema? Kwa nini siku zote walikutana na kushindwa? Kwa sababu yaliegemezwa kwenye wazo moja la kwamba tusipohitimisha kwanza makubaliano ya amani na Wapalestina, hakuna nchi nyingine ya Kiarabu ambayo ingerekebisha uhusiano wake na Israeli.



Kwa muda mrefu nimetafuta kufanya amani na Wapalestina. Lakini pia ninaamini kwamba hatupaswi kuwapa Wapalestina kura ya turufu ya veto juu ya mikataba mipya ya amani na mataifa ya Kiarabu. Wapalestina wanaweza kufaidika sana na amani pana zaidi. Wanapaswa kuwa sehemu ya mchakato huo, lakini hawapaswi kuwa na kura ya turufu ya veto juu ya mchakato huo.


Na pia ninaamini kwamba kufanya amani na mataifa mengi ya Kiarabu kungeongeza matarajio ya kufanya amani kati ya Israeli na Wapalestina. Tazama, Wapalestina ni 2% tu ya ulimwengu wa Kiarabu. Maadamu wanaamini kwamba 90% nyingine itabaki katika hali ya vita na Israeli, umati huo mkubwa, ulimwengu huo mkubwa wa Kiarabu unaweza hatimaye kutumika kuharibu taifa la Wayahudi.

Kwa hiyo Wapalestina watakapoona kwamba sehemu kubwa ya ulimwengu wa Kiarabu imejipatanisha na dola ya Kiyahudi, wao pia, watakuwa na uwezekano mkubwa wa kuachana na dhana ya kuiangamiza Israel, na hatimaye kuikumbatia njia ya amani ya kweli.



Sasa, kwa miaka mingi, mtazamo wangu wa amani ulikataliwa na wale walioitwa wataalamu. Naam, walikuwa na makosa. Chini ya mtazamo wao, hatukuunda mkataba mmoja wa amani kwa robo karne. Walakini, mnamo 2020, chini ya njia ambayo nilitetea, tulijaribu kitu tofauti. Na kwa muda mfupi, tulipata mafanikio ya kushangaza. Tuliafiki mikataba minne ya amani - tukifanya kazi na Marekani, Israel ilitengeneza mikataba minne ya amani, katika muda wa miezi minne, na nchi nne za Kiarabu - Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na Morocco.

Makubaliano ya Abraham Accord yalikuwa msingi wa historia. Na leo, sote tunaona baraka za mapatano hayo. Biashara na uwekezaji na washirika wetu wapya wa amani inashamiri. Mataifa yetu yanashirikiana katika nyanja za biashara, nishati, maji, kilimo, madawa, mabadiliko ya hali ya hewa, na nyanja zingine nyingi. Takriban Waisraeli milioni moja wametembelea Umoja wa Falme za Kiarabu UAE katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Kila siku, Waisraeli wanaokoa muda na pesa kwa kufanya jambo ambalo hawakuweza kufanya kwa miaka 70 - wanaruka juu ya Rasi ya Arabia bila vikwazo hadi maeneo ya Ghuba, India, Mashariki ya Mbali na Australia.

Mikataba ya Abraham Accord ilileta badiliko jingine kubwa. Iliwaleta Waarabu na Wayahudi karibu zaidi. Tunaiona katika harusi za mara kwa mara za Kiyahudi huko Dubai, katika kuwekwa wakfu kwa shule ya Torati katika sinagogi huko Bahran. Katika wageni wakimiminika kwenye Jumba la Makumbusho la Uyahudi wa Morocco na Casablanca. Tunaiona katika masomo ambayo yanatolewa kwa wanafunzi wa Kiarabu kuhusu historia ya Maangamizi makubwa ya holocaust yaliyofanywa wakati wa Ujerumani ya Hitler katika mitaala ya shule za UAE.


Hakuna shaka. Makubaliano ya Abraham Accord yalitangaza mapambazuko ya enzi mpya ya amani.

Lakini ninaamini kwamba tuko kwenye kilele cha mafanikio makubwa zaidi - amani ya kihistoria kati ya Israel na Saudi Arabia. Amani kama hiyo itasaidia sana kumaliza mzozo wa Waarabu wa Israeli. Itahimiza mataifa mengine ya Kiarabu kurekebisha uhusiano wao na Israeli. Itaongeza matarajio ya amani na Wapalestina. Itahimiza mapatano mapana kati ya Uyahudi na Uislamu, kati ya Jerusalemu na Makka, kati ya uzao wa Isaka na uzao wa Ishmaeli. Hizi zote ni baraka kubwa sana.

Wiki mbili zilizopita, tuliona baraka nyingine zikiibuka. Katika mkutano wa G20, Rais Biden Waziri Mkuu Modi na viongozi wa Ulaya na Waarabu walitangaza mipango ya ukanda maalum wa ushoroba ambao utaunganisha rasi (Peninsula) ya Arabia na Israeli. Itaunganisha India na Ulaya na njia za meli baharini, mitandao ya reli, mabomba ya nishati, nyaya za mawasiliano fiber optic.


Ushoroba maalum (corridor) katika ukanda huu utawezesha kuondoa vituo vya ukaguzi vya baharini, barabarani, ktk reli na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya bidhaa, mawasiliano na nishati kwa zaidi ya watu bilioni 2.

Ni mabadiliko gani ya kihistoria zaidi ya haya kwa nchi yangu. Unaona, ardhi ya Israeli iko katika njia panda kati ya Afrika, Asia na Ulaya. Na kwa karne nyingi, nchi yangu ilivamiwa mara kwa mara na falme geni za mbali katika kampeni zao za uporaji na kutawala nchi za mbali. Lakini leo, tunapobomoa kuta za uadui, Israeli inaweza kuwa daraja la amani na ustawi wa kiuchumi na biashara kati ya mabara haya.


Amani kati ya Israel na Saudi Arabia itaunda Mashariki ya Kati mpya.

Ili kuelewa ukubwa wa mageuzi ambayo tunatafuta kuendeleza, ngoja nikuonyeshe ramani ya Mashariki ya Kati mnamo 1948, mwaka ambao Israeli ilianzishwa. Hapa kuna Israeli mnamo 1948. Ni kanchi kadogo, kilichotengwa, iliyozungukwa na ulimwengu wa Kiarabu wenye uadui.

Katika miaka yetu saba ya kwanza, tulifanya amani na Misri na Jordan. Na kisha mnamo 2020, tulifanya mapatano ya Abraham Accord - amani na nchi zingine nne za Kiarabu. Sasa angalia nini kinatokea tunapofanya amani kati ya Saudi Arabia na Israel. Mashariki ya Kati nzima inabadilika. Tunabomoa kuta za uadui. Tunaleta uwezekano wa ustawi na amani katika eneo hili lote. Lakini pia tunafanya jambo lingine.


Unajua, miaka michache iliyopita, nilisimama hapa na kalamu kuweka alama nyekundu katika ukanda wa Mashariki ya Kati kuonyesha laana, laana kuu, laana ya Iran ya nyuklia. Lakini leo, sasa, ninaleta alama hii kuonyesha baraka kuu, baraka ya Mashariki ya Kati mpya, kati ya Israeli, Saudi Arabia na majirani zetu wengine.

Hatutaondoa tu vikwazo kati ya Israel na majirani zetu, tutajenga ukanda mpya wa amani na ustawi unaounganisha Asia, kupitia UAE, Saudi Arabia, Jordan, Israel, hadi Ulaya. Haya ni mabadiliko ya chanya, mabadiliko makubwa. Alama nyingine ya historia.


Sasa, wakati ukanda wa amani Mashariki ya Kati upanuka, ninaamini kwamba njia ya kweli kuelekea amani ya kweli na majirani zetu wa Palestina inaweza hatimaye kupatikana. Lakini kuna tahadhari izingatiwe. Inapaswa kusemwa hapa, kwa uwazi na nguvu. Amani inaweza kupatikana tu ikiwa umebebwa na ukweli. Haiwezi kutegemea propaganda za uwongo. Haiwezi kuegemezwa kwenye chuki za kusambaza kashfa zisizo na mwisho kwa watu wa Kiyahudi.

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas lazima akome kueneza propaganda na njama za kutisha dhidi ya Wayahudi katika Taifa la Kiyahudi. Narudia, nasisitiza , hivi karibuni Mahmoud Abbas alisema kwamba mtawala imla Hitler wa Ujerumani hakuwa anachuki za kuwasakama wayahudi (antisemite) - huwezi kufanya kampeni hizi . Lakini alifanya hivyo. Alisema hivyo.


Na Utawala wa Palestina lazima uache kuwatukuza magaidi, waache sera yake ya kihuni ya kuwafadhili kwa kulipa pesa kwa magaidi wa Kipalestina, kwa ajili ya mauaji ya Wayahudi. Haya yote ni ya kuchukiza, lazima njama hizi zikome ili amani itawale

Na chuki na propaganda hasi dhidi ya Wayahudi lazima zikataliwe popote zinapoonekana, iwe upande wa kushoto au wa kulia, iwe katika kumbi za vyuo vikuu au katika kumbi za Umoja wa Mataifa. Ili Amani idumu, Wapalestina lazima waache kutema chuki kwa Wayahudi, hatimaye wajipatanishe na taifa la Kiyahudi. Kwa hilo simaanishi tu kuwepo kwa taifa la Kiyahudi, bali kwa haki ya watu wa Kiyahudi kuwa na haki ya kiasili kuwepo katika nchi yao ya kihistoria - ardhi ya Israeli.


Na niwaambie, watu wa Israeli wanatamani amani kama hii. Natamani amani kama hii. Wakati nikiwa mwanajeshi kijana, zaidi ya nusu karne iliyopita, askari wenzangu na mimi katika vikosi maalum vya Israeli tulikabili hatari za kufa katika nyakati nyingi kwenye medani nyingi za vita, kutoka kwenye maji ya uvuguvugu ya Mfereji wa Suez, hadi miteremko iliyoganda theluji ya Mlima Hermoni, kutoka nyuma ya Mlima Hermoni. Mto Jordan hadi lami za njia za kuruka ndege uwanja wa ndege wa Beirut Lebanon.

Uzoefu niliopata nikiwa askari mstari wa mbele vitani na mambo mengine njliyoyaona kwa macho yalinifundisha gharama ya vita. Askari mwenzangu aliuawa mita chache karibu yangu na mwingine alikufa mikononi mwangu. Nilimzika kaka yangu mkubwa. Wale wenzangu ambao binafsi wamewahi teseka katika laana ya vita wanaweza kuthamini vyema baraka za amani.


Sasa, kuna vikwazo vingi kwenye njia ya amani. Kuna vikwazo vingi, kwa njia ya makubaliano ya Abraham Accord ya amani ambayo nimeeleza hivi punde. Lakini nimejitolea kufanya kila niwezalo ili kushinda vikwazo hivi, kutengeneza mustakabali bora wa Israeli, na watu wetu wote, watu wote katika eneo letu.

Siku mbili zilizopita, nilijadili maono haya ya amani na Rais Joe Biden. Tunashiriki matumaini sawa kwa kile kinachoweza kupatikana. Na ninathamini sana kujitolea kwake kuchangamkia fursa hii ya kihistoria. Marekani ni mdau muhimu sana katika juhudi hizi. Na kama vile tulivyofanikisha Makubaliano ya Abraham, na uongozi wa Rais Trump, naamini tunaweza kupata amani na Saudi Arabia, na uongozi wa Rais Biden.

Kwa kufanya kazi pamoja na uongozi wa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa ufalme wa Saudia , tunaweza kuunda mustakabali wa baraka kubwa kwa watu wetu wote.


Sasa, mwajua, mabibi na mabwana, mwajua, kuna nzi katika mafuta haya safi. Kwa sababu uwe na uhakika, mahafidhina wakereketwa wanaotawala Iran watafanya kila wawezalo kuzuia amani hii ya kihistoria. Iran inaendelea kutumia mabilioni ya fedha kuwapa washirika wake wa ugaidi. Inaendelea kupanua hema zake za ugaidi katika Mashariki ya Kati, Ulaya, Asia, Amerika Kusini, hata Amerika Kaskazini.

Walijaribu hata kumuua waziri wa mambo ya nje wa Amerika. Walijaribu hata kumuua mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani. Hii inakuambia yote unayohitaji kujua kuhusu nia ya mauaji ya Iran, na asili ya mauaji ya Iran.


Iran inaendelea kutishia njia za meli za kimataifa baharini , kuwashikilia raia wa kigeni kwa ajili ya kuwakomboa kwa dau la fedha na kujihusisha na kuficha mipango ya kuwa na silaha za nyuklia. Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, mgambo wake wauaji wameua mamia na kuwatia mbaroni maelfu ya raia jasiri wa Iran.


Ndege zisizo na rubani na programu za makombora za Iran zinatishia Israel na majirani zetu wa Kiarabu na ndege zisizo na rubani za Iran zimeleta na kuleta kifo na uharibifu kwa watu wasio na hatia nchini Ukraine.


Hata hivyo uchokozi wa utawala huo wa Iran kwa kiasi kikubwa unakabiliwa na hali ya kutojali katika jumuiya ya kimataifa. Miaka minane iliyopita, madola ya Magharibi yaliahidi kwamba iwapo Iran itakiuka makubaliano ya nyuklia, vikwazo hivyo virejeshwa. Kweli, Iran inakiuka makubaliano. Lakini vikwazo havijarejeshwa.


Kuzuia mipango kificho ya hatari ya nyuklia ya Iran. Sera hii ya kujifanya hamnazo ya mataifa na umoja wa mataifa lazima ibadilike . Vikwazo lazima virudishwe. Na zaidi ya yote, Iran lazima ikabiliane na tishio la kushughulikiwa .* Maadamu mimi ni Waziri Mkuu wa Israeli, nitafanya kila niwezalo kuzuia Iran kupata silaha za nyuklia.


Vile vile, tunapaswa kuunga mkono wanawake na wanaume jasiri wa Iran wanajitokeza kupinga utawala Tehran, ambao wanatamani uhuru. Ambao wameamka kwa ujasiri kwenye vijia vya Tehran na miji mingine ya Irani na wanakabiliwa na kifo. Ni watu wa Iran tuwaunge mkono, sio wakandamizaji wao, maana wamejitolea kupiga ukandamizaji hivyo ni washirika wetu wa kweli kwa mustakabali bora.

Mabibi na mabwana, kama wakati wetu ujao utakuwa wa baraka au laana itategemea pia jinsi tunavyoshughulikia labda maendeleo muhimu zaidi ya wakati wetu. Kuongezeka kwa akili ya bandia AI - Artificial intelligence.

Mapinduzi ya AI yanaendelea kwa kasi kubwa ya kama spidi ya mwanga wa radi. Ilichukua karne nyingi kwa ubinadamu kufikia mapinduzi ya kilimo. Ilichukua miongo kadhaa kufikia mapinduzi ya viwanda. Tunaweza kuwa na miaka michache tu ya kukabiliana na mapinduzi ya AI.


Hatari ni kubwa, na ziko mbele yetu. Kuvurugwa kwa demokrasia, ubongo wetu kuchukuliwa na akili bandia , nafasi za kazi kupunguzwa, kuongezeka kwa uhalifu, na udukuzi wa mifumo yote inayowezesha maisha ya kisasa. Bado kinachosumbua zaidi, ni mlipuko unaowezekana wa vita vinavyoendeshwa na Akili Bandia -AI ambavyo vinaweza kufikia kiwango kisichoweza kufikiria.


Na nyuma ya hii labda kuna tishio kubwa zaidi, kilichokuwa simulizi za kusadikika ya mambo ya hadithi za kisayansi, kwamba mashine za kujifundisha zinaweza kudhibiti wanadamu, badala ya sisi watu kudhibiti mashine. Mataifa yanayoongoza duniani, hata yawe na ushindani, lazima yashughulikie hatari hizi. Ni lazima tufanye hivyo haraka. Na lazima tufanye hivyo pamoja. Lazima tuhakikishe kwamba zama za Akili Bandia ya AI utopia haigeuki kuwa tishio la AI.


Tuna mengi ya chanya ya kupata kupitia Akili Bandia . Hebu wazia baraka za hatimaye kubaini muundo wa kanuni za vinasaba chembe za urithi (gene), kurefusha maisha ya mwanadamu kwa miongo kadhaa, na kupunguza sana magonjwa ya uzee. Hebu fikiria huduma ya afya inayolengwa kulingana na muundo wa maumbile ya vinasaba vya kila mtu, na dawa ya kutabiri ambayo huzuia magonjwa muda mrefu kabla ya kutokea. Wazia roboti zinazosaidia kuwatunza wazee. Hebu fikiria mwisho wa msongamano wa magari, huku magari yanayojiendesha yakiwa ardhini, chini ya ardhi na angani. Hebu wazia elimu ya ziada kujifunza kibinafsi ambayo inakuza uwezo kamili wa kila mtu katika maisha yake yote.


Hebu fikiria ulimwengu wenye nishati safi isiyo na kikomo, na maliasili kwa mataifa yote. Hebu fikiria kilimo cha kisasa zaidi na viwanda vya kiotomatiki vinavyotoa chakula na bidhaa kwa wingi vinavyomaliza kabisa tatizo la njaa na upatikanaji chakula.


Najua huu maneno haya unayosikia ni kama mistari ya wimbo wa mwanamuziki nguli mtunzi John Lennon. Lakini yote yanaweza kutokea.


Hebu kwa punde waza , fikiria kwamba tunaweza kufikia mwisho wa uhaba wa kila kitu!. Kitu ambacho kimeshindikana katika hali ya ubinadamu ndani ya historia yote. Haya Yote ni ndani ya uwezo wetu. Na hapa kuna kitu kingine ambacho tunaweza kufikia. Kwa matumizi sahihi ya Akili Bandia- AI, tunaweza kuchunguza mbingu za mbali kuliko hapo awali na kupanua tunachofahamu zaidi ya sayari yetu ya bluu.


Kwa uzuri au ubaya, maendeleo ya Akili Bandia - AI yataongozwa na mataifa machache, na nchi yangu Israeli tayari iko kati yao. Kama vile mapinduzi ya kiteknolojia ya Israeli yalivyoupa ulimwengu ubunifu wa kustaajabisha, nina imani kwamba Akili Bandia AI iliyotengenezwa na Israeli itasaidia tena wanadamu wote.


Natoa wito kwa viongozi wa dunia kuja pamoja ili kuchagiza mabadiliko makubwa yaliyo mbele yetu. Lakini kufanya hivyo kwa njia ya kuwajibika na ya kimaadili. Lengo letu lazima liwe zaidi kulinda kuwa Akili Bandia- AI inaleta uhuru na sio kiduchu, inazuia vita badala ya kuvianzisha na kuhakikisha kuwa watu wanaishi maisha marefu, yenye afya, yenye tija na amani. Ni ndani ya uwezo wetu.


Na tunapotumia nguvu za Akili Bandia -AI, ngoja kwanza tukumbuke kila wakati thamani isiyoweza kubadilishwa ya ubinadamu na hekima ya mwanadamu. Hebu tuthamini na undani wa uwezo wa huruma, ambao hauwezi kuchukuliwa na nafsi ya Akili Bandia AI


Maelfu ya miaka, Musa aliwapa wana wa Israel chaguo lisilo na wakati na la ulimwengu wote. Angalieni, nimesema mbele yenu hivi leo, baraka na laana. Na tuchague kwa busara kati ya laana na baraka zinazosimama mbele yetu leo. Wacha tutumie azimio letu na ujasiri wetu kukomesha laana ya Iran ya nyuklia na kurudisha nyuma ushabiki na uchokozi wake.

Hebu tulete baraka za Mashariki ya Kati mpya ambayo itabadilisha ardhi ambayo iliwahi kuandikwa kwa migogoro na machafuko, kuwa uwanda wa ustawi na amani. Na tuepuke hatari za Akili Bandia - AI kwa kuchanganya utu, nguvu za akili ya binadamu na mashine, ili kuleta mustakabali mzuri wa ulimwengu wetu katika wakati wetu, na kwa siku zote za mbele. Asante.


*Source : FULL TEXT: Benjamin Netanyahu's 2023 UN General Assembly Speech
 
Mtoa mada acha uongo, uongo ni ushetani, pigania ya kwetu hapa na hasa kijijini kwako, IDF lilikua linakaribia Damascus, IDF lilishavuka suez canal!,ila hii inatusaidia nini sisi watanzania?,its craze tupo to much occupied na mambo ya nje wakati hatuwezi kujadili ya kwetu, tuna matatizo mengi mno nchi hii, tujitahidi kuelekeza nguvu na maarifa zaidi huku kuliko ya middle east
 
Mtoa mada acha uongo, uongo ni ushetani, pigania ya kwetu hapa na hasa kijijini kwako, IDF lilikua linakaribia Damascus, IDF lilishavuka suez canal!,ila hii inatusaidia nini sisi watanzania?,its craze tupo to much occupied na mambo ya nje wakati hatuwezi kujadili ya kwetu, tuna matatizo mengi mno nchi hii, tujitahidi kuelekeza nguvu na maarifa zaidi huku kuliko ya middle east
Kasome vita ya Yom Kippur ilianzaje.
 
Kasome vita ya Yom Kippur ilianzaje.
No Sina muda huo, hapa nchini kuna pressings issue zinazonigusa,why nipote muda wangu kujua ya middle east?,najiuliza why umeme ukatike hapa nchini, why hizi social services ni duni?
 
No Sina muda huo, hapa nchini kuna pressings issue zinazonigusa,why nipote muda wangu kujua ya middle east?,najiuliza why umeme ukatike hapa nchini, why hizi social services ni duni?
Ukifahamu yanayoendelea sehemu nyingine duniani ndiyo utatambua vyema kwa nini unapatwa na matatizo unayopata. Inasikitisha unadharau hilo.
 
Ukifahamu yanayoendelea sehemu nyingine duniani ndiyo utatambua vyema kwa nini unapatwa na matatizo unayopata. Inasikitisha unadharau hilo.
We have the right to disagree, nipo too much occupied na haya yanayonizunguka na yananielemea mno,ningependa nimuulize waziri wangu wa Afya why huduma zetu ni mbovu mpaka inapelekea ninyi muende India kutibiwa au Netcare milpark na sio Ikonda hospital au mwananyamala hospital?
 
Hiwezi kujiandaa na kila kitu kwa muda wote especially dhidi ya binadam mwenzako kwasababu hujui dk kadhaa zijazo ataamua nini. Hua inatokea ndo maana leo tuna Sept 11 na matukio mengine kama hayo.

Hakuna shirika la ujasusi linalo detect kila tukio na kudeal nalo kwa 100%. Ila pia Mossad nao ni shirika la kawaida sidhani kwenye list ya mashirika bora kama linaifikia hata ISI ya Pakistan sema ni vile tu wana deal na challenges zinazokuwa organized na vikundi vya kawaida ila pia hua wanasaidiwa intel na mashirika ya magharibi ila kinyume na hapo wanaweza kuwa sawa na wengine tu
 
We have the right to disagree, nipo too much occupied na haya yanayonizunguka na yananielemea mno,ningependa nimuulize waziri wangu wa Afya why huduma zetu ni mbovu mpaka inapelekea ninyi muende India kutibiwa au Netcare milpark na sio Ikonda hospital au mwananyamala hospital?
Unatakiwa pia ujue huko India kuna nini hadi wanaenda huko. Kinyume na hapo huwezi kuongopea watu kuwa umetingwa kufuatilia mambo ya maana.
 
Hiwezi kujiandaa na kila kitu kwa muda wote especially dhidi ya binadam mwenzako kwasababu hujui dk kadhaa zijazo ataamua nini. Hua inatokea ndo maana leo tuna Sept 11 na matukio mengine kama hayo.

Hakuna shirika la ujasusi linalo detect kila tukio na kudeal nalo kwa 100%. Ila pia Mossad nao ni shirika la kawaida sidhani kwenye list ya mashirika bora kama linaifikia hata ISI ya Pakistan sema ni vile tu wana deal na challenges zinazokuwa organized na vikundi vya kawaida ila pia hua wanasaidiwa intel na mashirika ya magharibi ila kinyume na hapo wanaweza kuwa sawa na wengine tu
Mossad wapo vizuri sana. Kuweza kuua wanasayansi wa Neuclear wa Iran ndani ya ardhi yao si kitu kidogo. Hili ni moja ya shirika la kijasusi bora zaidi duniani.
 
1 Thesalonike 5:3
"Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa."
Walijisahau hili neno hawakulizingatia.
 
Mwaka 1973 Israeli ilishambuliwa na Misri na Syria kwa kushtukizwa wakati wa majira ya sikukuu ya Yom Kippur. Misri walivuka mfereji wa Suez na kuingia Israel(Sinai). Wasyria nao wakaingia huko Golan.

Hali ilikuwa tete sana kwa Israel hadi jeshi likaamua kuwa liwaache Wasyria wafanye wanavyotaka wao wadeal na mwenye nguvu, Misri.

Ukiisoma ile vita, habari za kijasusi kuhusu vita kutoka Mossad na MI ziliwafikia wakubwa mapema. Lakini siasa zilifanya wawe wazito kuchukua maamuzi.

Kwenye Movie Golda(2023), Waziri mkuu wa wakati huo, Golda Meir anasikika akisema kuwa kumobilize jeshi wakati wa sikukuu za Yom Kippur ni kutaka kujiua kisiasa na kuwapa wapinzani cha kusema.

Kwenye demokrasia, maamuzi makubwa, hata yanayohusu usalama wa nchi hutanguliza kwanza maslahi ya kisiasa kisha ya nchi ndiyo yanafuata.

Idara za ujasusi za Israeli zilishutumiwa vikali sana baada ya vita ya Yom Kippur, lakini ni ngumu sana idara hizi kufanya kazi zake vizuri kwenye mazingira ya kidemokrasia.

Jana tena, kwenye msimu wa Yom Kippur, asubuhi ya sabato Israel imeshambuliwa na Hamas kwa style ile ile ya 1973. Miaka 50 ya kumbukumbu ya vitw ya Yom Kippur!!. Tena imeshambuliwa baada ya kutokea machafuko makubwa ya kugombania "siasa" ndani ya Israeli.

Si rahisi kwa chombo kama Mossad kutofahamu kuhusu shambulio lililotokea jana. Lakini ni wanasiasa ndiyo wanaofanyia kazi taarifa za kijasusi. Na wanasiasa wanafanya maamuzi kwa kutanguliza maslahi ya kisiasa mbele.

Maoni yangu: Siasa za kidemokrasia ni hatari kwa usalama wa nchi. Zinaweza kukwamisha hata kazi za taasisi bora kama Mossad.
Baada ya mwezi mmoja nitaaza kuamini,
1. Mossad hawakuwa na intelijensia juu ya maandalizi ya shambulio la Hamas 06/10/2023.
2. Au taarifa walikuwa nazo ila walijifanya hawajui ili litokee ili watimize adhima na agenda zao.
 
Back
Top Bottom