Ramli yako kibokoSalam za jumapili wanabodi!!
Napenda kuweka hii rejea mahsusi kwa siku za mbele!!
Katika awamu ya tano kuna vitendo vya hovyo sana hasa ktk suala zima la matumizi ya pesa za umma. Na u hivyo huu unafunikwa na Kauli ya 'nia njema'
Nchi yetu imejiondoa kabisa ktk program ya uwazi na mambo mengi sasa imekuwa ni siri kuu....
Tukianza na sakata la E-passport tukumbuke na ya Richmond!! Kwenye Richmond 'nia njema' na uharaka vilileta balaa!! Sura ile ile ya sakata la Richmond ndio imejitokeza kwenye E-passport!! Richmond ilipewa Kazi kinyume na zabuni na hii kampuni ya e E-passport pia imepewa Kazi kinyume na zabuni na haina sifa stahiki.
Awamu ya tano imetupa pembeni utaratibu wa zabuni na sasa inaamua na kufanya manunuzi au kuingia mikataba wenyewe kwa amri toka juu...
Rejea hii itatukumbusha siku za usoni na hasa kwa Miradi hii....
1. Uwanja wa ndege chato
2.vitambulisho vya utaifa
3.fly overs
4. Bombadier
5.Tenda za ujenzi za TBA n.k
Kwa kumalizia tuu.... nimeandika hayo nikiwa full detailed..... kuna vitu duniani havichiki navyo ni Jua...mwezi na ukweli.
MUDA NI HAKIMU WA YOTE!!