Tahadhari kwa mliojipanga kununua hisa za makampuni ya simu...

Wewe niite muongo ila nenda UKANUNUE JINA. Fedha ni zako na sina mamlaka nazo... Mimi kama expert kazi yangu ni kutoa angalizo, na nimetimiza majukumu yangu kwa umma wa watanzania... Hasa ndugu zangu wasio na upeo mkubwa juu ya mambo ya biashara, wasije wakaliwa kama walivyoliwa kwenye DECI...
Bado sijaona huo U_expert wako. Unajitamba na degree ya biashara. Kila mtu akianza kusema elimu yake hapa na uzoefu alionao tutafika kweli. Kwa uzoefu wangu wa miaka 5 wa kununua hisa na kuuza hata kufatilia kila leo soko la hisa, hapo umeipotosha jamii. Kuwa makini na fatilia kwa makini soko la hisa usitoe taarifa kama haujafatilia vya kutosha (No research no right to speak). Sitoweza kutaja elimu yangu kama unavyojibandikia wewe elimu ili kupotosha wachache waliomo humu juu ya soko la hisa. Me naona thread yako ni kama vile imekaa kivita fulani ndani yake.

Tuwe makini
 
Una point nzuri....why now and not five years ago while it was booming..

Haya makampuni ya simu yalikuwa na influence sana wakati wa Kikwete; viongozi wa ccm wa wakati huo walikuwa shareholders kwenye makampuni kama Vodacom hivyo waliweza kuishawishi serikali isitekeleze sheria ya kuyataka makampuni ya simu yajiorodheshe kwenye soko la hisa kama yalivyotakiwa yafanye!!!

Kutokujiorodhesha kwenye soko la hisa kuliyawezesha haya makampuni kukwepa kulipa kodi stahiki kwasababu walikuwa hawana ulazima wa kuweka mahesabu yao wazi kwa umma ambapo kama wakijiorodhesha ni lazima vitabu vyao vya mahesabu viwekwe wazi vionekane na umma na hivyo kuwa vigumu kutolipa kodi stahiki!!

Haya makampuni yanajiorodhesha sasa kukidhi utekelezaji wa sheria ambapo enzi ya Kikwete ilipuuziwa!!!!
 
Mtoa mada ebu tueleze Ni biashara gani yenye mwelekeo wa kukua kuliko mawasiliano? Kuhusu wafanyabiashara wakubwa kujitoa hats buffet aliuza hisa za McDonalds hadi Leo anakiri lilikua Ni kosa so uje na evidence zakutosha sio unasoma kwenye notes. And kuhusu kuuza minara kwakua umesoma biashara ungelielewa hilo unapoitaji nyama unanunua Ndama na kumfuga au unaenda buchani?!
 
Leo pia nimesikia Kuna mtu kapiga simu REDIO tumaini kipindi cha dukuduku akiomba Swiss port wawalipe gawio lao la hisa toka mwaka 2015 au 2005 sijasikia vizuri hawajawahi kutoa gawio Kwa wana hisa

Sent from Microsoft Lumia 950xl Lte
 
Mwenye ujuzi zaidi kuhusiana na mambo ya hisa atujulishe sisi tusiojua lolote kuhusiana na mambo ya hisa mana kama mimi naona kununua hisa za simu ni faida tosha
 
Nami navyojua ndio hvyo ...huyu mleta Uzi ana degree ya kukariri kwenye vimbweta bila kufuatilia yanayoendelea kwenye nchi.
Mkuu tusaidie wengine inakuwaje sasa hata wakiorodhesha DSE huku assets hawana Mimi nayenunua hisa nanunua kipi kama siyo jina kwa kauli ya mtoa madam!?
 
Wewe niite muongo ila nenda UKANUNUE JINA. Fedha ni zako na sina mamlaka nazo... Mimi kama expert kazi yangu ni kutoa angalizo, na nimetimiza majukumu yangu kwa umma wa watanzania... Hasa ndugu zangu wasio na upeo mkubwa juu ya mambo ya biashara, wasije wakaliwa kama walivyoliwa kwenye DECI...
Wewe unajua zaidi kuliko CMSA na DSE who are evaluating those Telecom Companies? Usipotoshe.
 
Tokea NMB hisa zake zishuke toka 4100 hadi 2750 sina hamu nazo
Tokea Hisa za CRDB zisipande hata kufikia 1000 sina hamu nao
Tokea hisa za TCC kushuka toka 16000 hadi 11500 sina hamu nao
Tokea swala arudi 500 sawa na bei aliyoingia nayo sokoni sina hamu nao
 
@ Root kua na imani nayo ndugu mana NMB walianza na hisa 1 kwa Tsh 600 na sasa hivi ni mara 4 ya bei walioanzia.TBL walianza na less than 2000 (nlinunua hisa 1 kwa 1800) ila sasa hivi ni more than 10,000 so hisa iko vizuri ila hii ya mitandao ya simu naamini zitakua good sana ila nafurahi nnavosoma hapa mana naelimika na kujifunza mengi
 
Leo pia nimesikia Kuna mtu kapiga simu REDIO tumaini kipindi cha dukuduku akiomba Swiss port wawalipe gawio lao la hisa toka mwaka 2015 au 2005 sijasikia vizuri hawajawahi kutoa gawio Kwa wana hisa

Sent from Microsoft Lumia 950xl Lte
Ordinary shareholders wanakuaga wa mwisho kupata gawiwo kama faida itakuwepo baada ya kutoa gharama zote na sio lazima wao wapate dividend/gawiwo kama litapatikana.
 
Kama hii ndio msingi (premise) wa unachosema (argument yako), umepotoka na unapotosha wengine.

Hapa unaweza kuwa na point, lakini kwa msingi huo huo milicom imenunua hisa za zantel kutoka etisalat si muda mrefu umepita, nao wawe studied. Na hii isieleweke kwamba nasema zantel wanafanya vizuri au la.

Unanunua thamani ya baadaye (future value) ya kampuni.

Sio ajabu unaloita "jina tu" lina thamani zaidi ya minara, majengo na magari. Umesema umesoma biashara miaka 10 au zaidi so you should know this. Minara, majengo na magari sio core asset kwa mitandao ya simu, zingekuwa core asset wasingemuachia mwingine.

Hii ni sahihi. Ungeishia hapa ingetosha.

Utter nonsense. And spoken with so much authority and in such a self assured manner too, the story of these forums.
You are a FUNDI indeed! Thank you!
 
Jamani, msije kusema napiga porojo, mimi nina digrii kadhaa kwenye mambo ya biashara, nimetumia karibu miaka kumi kusomea mambo ya kibiashara
Miaka 10 yote ya nini? Au ulikuwa una "disco" au una "resit"! Hongera, but your major syllogism fell apart, anyway!
 
Jamani, msije kusema napiga porojo, mimi nina digrii kadhaa kwenye mambo ya biashara, nimetumia karibu miaka kumi kusomea mambo ya kibiashara, kwa hiyo ndio maana naona bora niwataadharishe nyie mnaotegemea kununua hisa kwenye makampuni haya ya simu...

Kwa nini mtu huuza hisa?
Kuna sababu kadhaa za kuuza hisa, moja ni kuongeza mtaji ili kukuza biashara,
- Mbili ni pale mtu anapotaka kujitoa kwenye biashara huuza hisa zake kwenye biashara husika,
- Tatu ni kukusanya fedha ili kuweza kulipia madeni iwapo kampuni ipo kwenye hali ngumu kiuchumi.

Kwa nini kampuni nyingi za simu wanauza hisa, na kwa nini wanauza sasa?
- The market is not growing or its not profitable kwa hiyo wanauza hisa ili wawekeze kwenye biashara nyingine ambazo zina faida zaidi,
- Kwa nini wanauza hisa zao sasa? Hapo ndipo pa kujiuliza, kwa nini hawakuuza hisa zao labda miaka miwili, mitatu au mitano iliyopita? Jibu ni kuwa hakuna mtu anayeuza mali yake ikiwa inamzalishia, hakuna mtu anayeuza ng'ombe wa maziwa anayekamuliwa lita nyingi za maziwa. Ngo'ombe anauzwa akiwa amekwisha zeeka, au kama ni jike akiwa hana uwezo wa kutoa maziwa ya kutosha...
Study wanahisa wakubwa, Miaka ya hivi karibuni mwanahisa mkubwa Bwana Rostam aliuza hisa zake zenye thamani ya karibia bilioni mia tatu? Je jiulize, kama kampuni inafanya vizuri, kwa nini wanahisa wakubwa wanauza hisa zao badala ya 'kununua' hisa zaidi? Jibu unalo mwenyewe.

Je unapo nunua hisa unanunua nini?

Kwa kampuni za simu kwa hali ya sasa, unaponunua hisa, UNANUNUA JINA TU.
Haya makampuni makubwa ya simu kama Vodacom, Tigo nk walishauza minara yao yote ya simu kwa kampuni ya Helios Towers Tanzania.
Hawana majengo ofisi zote wamepanga,
Magari yao wamekodisha kwa kampuni mbali mbali za usafirishaji,
kwa hiyo haya makampuni yanamiliki jina tu... Hayana assets za maana. Usidanganyike na majina makubwa ya makampuni haya...
Waulizeni wenzenu walionunua hisa za Precision Air wametengneza faida sh ngapi?

Kiufupi mtaponunua hisa ikala kwenu hakuna atakaye watetea, Sheria ya manunuzi inatoa angalizo kwa mnunuzi wa bidhaa yeyote kwa kusema, 'Buyer beware'!

Kampuni halisi ya simu kwa hivi sasa hapa Tanzania ni Helios Towers ambayo ndiyo inamiliki minara ya mawasiliano (Hawa wengine wamebaki kuwa madalali wa sekta ya mawasiliano)... Siku wakija kutibuka wakakataa kupangisha minara yao, ina maana haya makampuni mengine ya simu yatatoweka... Kinachoyaweka haya makampuni ya simu hapa nchini ni vibali vya mawasiliano walivyouziwa na TCRA. Cku TCRA nao wakigoma ku renew leseni zao za mawasiliano huo ndio utakuwa mwisho wa makampuni husika...

Vodacom sells towers to Helios in $75 million deal: report | TelecomEngine.com

Bharti Airtel to sell 1,350 towers in Tanzania to American Tower Corp

Tigo Tanzania Sells Tower Assets to Helios Towers
Huyu jamaa ni muongo kuliko hats mwenye jina lake mohongo wa pale mjengoni

Had I kufikia kampuni za simu wanabinafsisha minara yao ni kwa sababu ya usumbufu wa service tu ndiomana wakaona wauze minara yao kwa kampuni ya kimarekani iliokua na uzoefu na kampuni hio imeanzia kununua minara barani Africa nchini south Africa wakaenda Nigeria Congo sasa wapo Tanzania sio kwa kufilisika

Makampuni ya hisa yana faida kubwa sna ndiomana serkali ikalazimisha wauze hisa zao kwa wazawa ili nao wafaidike na gaio la mwezi
Kutoka kwenye faida na nijambo jema kabisa
Swala ka kuuza hisa kwa kampuni kubwa duniani sio kigeni labda hapa kwetu bongo ndio utaona tajiri anangangania makampuni take pekeake bila kuuza hata robo ya hisa na huo ni ujinga kabisa
 
Kama mnabisha kuwa hii si kazi ya lobby group, kwa nini sekta nyingine 'hazijalazimishwa' kuingia DSE? Kulikuwa na ulazima gani wa kampuni za simu kufanya ivyo? Mbona Helios wanaomiliki minara hawajalazimishwa kuingia DSE? Mbona Tanesco, IPTL and the like hawajaingizwa DSE?
Kampuni zote kubwa zimelazimishwa isipokua za wazawa tu ndio watakua na hiari ya kuuza au kutokuuza hisa zao kwenye solo la DSE
 
Naona disinformation zimeanza. Umetengeneza mazingira ya kuaminika huku ukidanganya pia. Nenda website ya TCRA kuna information za kutosha kuhusu telecom industry hapa Tanzania. The industry is growing. Hilo la Helios it was a good move by the government and telcom companies kupunguza gharama, mind you Helios wanamiliki minara na wanawapangisha telcom kuweka vifaa vyao. Statement zako zina uongo.
 
Mkuu tusaidie wengine inakuwaje sasa hata wakiorodhesha DSE huku assets hawana Mimi nayenunua hisa nanunua kipi kama siyo jina kwa kauli ya mtoa madam!?
Makampuni ya madini na simu yalitakiwa yawe yamejiorodhesha kwenye soko la hisa ila kutokana na serikali iliyopita kutofuatilia ndio maana hawakufanya hivyo .Serikali ya sasa ndio inataka kutekeleza hilo agizo.Ndivyo hivyo mkuu ukitaka mengi ya hisa tafuta madalali wata"speculatia" vzuri.
 
Jamani, msije kusema napiga porojo, mimi nina digrii kadhaa kwenye mambo ya biashara, nimetumia karibu miaka kumi kusomea mambo ya kibiashara, kwa hiyo ndio maana naona bora niwataadharishe nyie mnaotegemea kununua hisa kwenye makampuni haya ya simu...

Kwa nini mtu huuza hisa?
Kuna sababu kadhaa za kuuza hisa, moja ni kuongeza mtaji ili kukuza biashara,
- Mbili ni pale mtu anapotaka kujitoa kwenye biashara huuza hisa zake kwenye biashara husika,
- Tatu ni kukusanya fedha ili kuweza kulipia madeni iwapo kampuni ipo kwenye hali ngumu kiuchumi.

Kwa nini kampuni nyingi za simu wanauza hisa, na kwa nini wanauza sasa?
- The market is not growing or its not profitable kwa hiyo wanauza hisa ili wawekeze kwenye biashara nyingine ambazo zina faida zaidi,
- Kwa nini wanauza hisa zao sasa? Hapo ndipo pa kujiuliza, kwa nini hawakuuza hisa zao labda miaka miwili, mitatu au mitano iliyopita? Jibu ni kuwa hakuna mtu anayeuza mali yake ikiwa inamzalishia, hakuna mtu anayeuza ng'ombe wa maziwa anayekamuliwa lita nyingi za maziwa. Ngo'ombe anauzwa akiwa amekwisha zeeka, au kama ni jike akiwa hana uwezo wa kutoa maziwa ya kutosha...
Study wanahisa wakubwa, Miaka ya hivi karibuni mwanahisa mkubwa Bwana Rostam aliuza hisa zake zenye thamani ya karibia bilioni mia tatu? Je jiulize, kama kampuni inafanya vizuri, kwa nini wanahisa wakubwa wanauza hisa zao badala ya 'kununua' hisa zaidi? Jibu unalo mwenyewe.

Je unapo nunua hisa unanunua nini?

Kwa kampuni za simu kwa hali ya sasa, unaponunua hisa, UNANUNUA JINA TU.
Haya makampuni makubwa ya simu kama Vodacom, Tigo nk walishauza minara yao yote ya simu kwa kampuni ya Helios Towers Tanzania.
Hawana majengo ofisi zote wamepanga,
Magari yao wamekodisha kwa kampuni mbali mbali za usafirishaji,
kwa hiyo haya makampuni yanamiliki jina tu... Hayana assets za maana. Usidanganyike na majina makubwa ya makampuni haya...
Waulizeni wenzenu walionunua hisa za Precision Air wametengneza faida sh ngapi?

Kiufupi mtaponunua hisa ikala kwenu hakuna atakaye watetea, Sheria ya manunuzi inatoa angalizo kwa mnunuzi wa bidhaa yeyote kwa kusema, 'Buyer beware'!

Kampuni halisi ya simu kwa hivi sasa hapa Tanzania ni Helios Towers ambayo ndiyo inamiliki minara ya mawasiliano (Hawa wengine wamebaki kuwa madalali wa sekta ya mawasiliano)... Siku wakija kutibuka wakakataa kupangisha minara yao, ina maana haya makampuni mengine ya simu yatatoweka... Kinachoyaweka haya makampuni ya simu hapa nchini ni vibali vya mawasiliano walivyouziwa na TCRA. Cku TCRA nao wakigoma ku renew leseni zao za mawasiliano huo ndio utakuwa mwisho wa makampuni husika...

Vodacom sells towers to Helios in $75 million deal: report | TelecomEngine.com

Bharti Airtel to sell 1,350 towers in Tanzania to American Tower Corp

Tigo Tanzania Sells Tower Assets to Helios Towers
ACHA KUDANGANYA UMMA ...NIMESOMA HATA SIJAMALIZA HII HABARI YAKO NI YA MTU ASIEJUA LOLOTE KUHUSU HISA NA UENDESHAJI WA KAMPUNI ZA SIMU, SABABU YA KAMPUNI ZA SIMU KUUZA HISA IPO KISHERIA NA HAIKUWA INATEKELEZWA, SERIKALI IMEWABANA SASA WANAGAWA SHARES NA NI ONLY 25% NA KAMA SIO SERIKALI HAWAKUWA NA SHIDA NA KUUZA HISA. NWAYS NITARUDI
 
Mkuu mimi nashukuru sana unatupunguzia competition wakati wa IPO maana nafaham zikiwa under subscribed hizo share hatutauziwa kwa pro rata base so nitapata zote nitakazohitaji. Halafu ikifika wa kati wa profit kubwa na dividend ya kutosha mtajikuta mliemfuata huyu "Bwana yule" mnakuja kununua kwa price ambayo kwangu itakua ni faida ya maisha na nitaziuza tu kwenu coz mtabid kwa price kubwa. Natanguliza shukrani kwa "Bwana yule"
 
Mleta mada umeongea vizuri tuu,ila watu hawajakuelewa baadhi.Unaponunua hisa lazima uangalie hali ya kifedha ya kampuni japo miaka mitatu nyuma na mbeleni kuna uelekeo wa faida. Sio kukurupuka,na pia mnunuaji ajue kampuni yaweza kupata hasara na gawio lisiwepo. Wajifunze Tanzania Oxygen watu walinunua hisa,baadae ukaguzi wa mahesabu ikabainika nadhani sina uhakika kampuni ilikuwa haizalishi faida.Hivyo hisa zake kwa muda mrefu zikadoda sokoni.
Ni kuchukua tahadhari hasa unapotaka kuwekeza kwenye hisa.
 
Back
Top Bottom