Nichumu Nibebike
JF-Expert Member
- Aug 28, 2016
- 8,660
- 15,745
Jamani, msije kusema napiga porojo, mimi nina digrii kadhaa kwenye mambo ya biashara, nimetumia karibu miaka kumi kusomea mambo ya kibiashara, kwa hiyo ndio maana naona bora niwataadharishe nyie mnaotegemea kununua hisa kwenye makampuni haya ya simu...
Kwa nini mtu huuza hisa?
Kuna sababu kadhaa za kuuza hisa, moja ni kuongeza mtaji ili kukuza biashara,
- Mbili ni pale mtu anapotaka kujitoa kwenye biashara huuza hisa zake kwenye biashara husika,
- Tatu ni kukusanya fedha ili kuweza kulipia madeni iwapo kampuni ipo kwenye hali ngumu kiuchumi.
Kwa nini kampuni nyingi za simu wanauza hisa, na kwa nini wanauza sasa?
- The market is not growing or its not profitable kwa hiyo wanauza hisa ili wawekeze kwenye biashara nyingine ambazo zina faida zaidi,
- Kwa nini wanauza hisa zao sasa? Hapo ndipo pa kujiuliza, kwa nini hawakuuza hisa zao labda miaka miwili, mitatu au mitano iliyopita? Jibu ni kuwa hakuna mtu anayeuza mali yake ikiwa inamzalishia, hakuna mtu anayeuza ng'ombe wa maziwa anayekamuliwa lita nyingi za maziwa. Ngo'ombe anauzwa akiwa amekwisha zeeka, au kama ni jike akiwa hana uwezo wa kutoa maziwa ya kutosha...
Study wanahisa wakubwa, Miaka ya hivi karibuni mwanahisa mkubwa Bwana Rostam aliuza hisa zake zenye thamani ya karibia bilioni mia tatu? Je jiulize, kama kampuni inafanya vizuri, kwa nini wanahisa wakubwa wanauza hisa zao badala ya 'kununua' hisa zaidi? Jibu unalo mwenyewe.
Je unapo nunua hisa unanunua nini?
Kwa kampuni za simu kwa hali ya sasa, unaponunua hisa, UNANUNUA JINA TU.
Haya makampuni makubwa ya simu kama Vodacom, Tigo nk walishauza minara yao yote ya simu kwa kampuni ya Helios Towers Tanzania.
Hawana majengo ofisi zote wamepanga,
Magari yao wamekodisha kwa kampuni mbali mbali za usafirishaji,
kwa hiyo haya makampuni yanamiliki jina tu... Hayana assets za maana. Usidanganyike na majina makubwa ya makampuni haya...
Waulizeni wenzenu walionunua hisa za Precision Air wametengneza faida sh ngapi?
Kiufupi mtaponunua hisa ikala kwenu hakuna atakaye watetea, Sheria ya manunuzi inatoa angalizo kwa mnunuzi wa bidhaa yeyote kwa kusema, 'Buyer beware'!
Kampuni halisi ya simu kwa hivi sasa hapa Tanzania ni Helios Towers ambayo ndiyo inamiliki minara ya mawasiliano (Hawa wengine wamebaki kuwa madalali wa sekta ya mawasiliano)... Siku wakija kutibuka wakakataa kupangisha minara yao, ina maana haya makampuni mengine ya simu yatatoweka... Kinachoyaweka haya makampuni ya simu hapa nchini ni vibali vya mawasiliano walivyouziwa na TCRA. Cku TCRA nao wakigoma ku renew leseni zao za mawasiliano huo ndio utakuwa mwisho wa makampuni husika...
Vodacom sells towers to Helios in $75 million deal: report | TelecomEngine.com
Bharti Airtel to sell 1,350 towers in Tanzania to American Tower Corp
Tigo Tanzania Sells Tower Assets to Helios Towers