Tafsiri ya Kujivua Magamba CCM inapotoshwa

Wazembe wa kufikiria kama wewe hukimbilia miamvuli ya kujificha (defensive mechanism) bila kuchosha akili zao. Kwa nini usijadili hoja iliyopo mezani?

we ndo mzembe, ina maana una akili sana kuliko wana JF wote waliotafsiri. Displacement type of defense mechanism
 
we ndo mzembe, ina maana una akili sana kuliko wana JF wote waliotafsiri. Displacement type of defense mechanism
Nyakageni ulichokuwa unakifanya tangia thread hii ingie hapa ulikuwa sahihi kulingana na upeo wako i.e. Kusoma maoni ya watu wengine tu. Lakini kucomment hauwezi kabisa na nafikiri ni kwa sababu ya uwezo wako mdongo wa kuzaliwa. Nipo nakuombea ili angalau upate nafuu ya ujinga.
 
Kwa muda mrefu wanaharakati wa vyama pinzani wakuwa wakiwalaumu walioshika dola na chama chao kwamba kinawafumbia macho mafisadi. Katika wakati mwingine kiongozi wa dola na chama tawala wamekuwa akilaumiwa kwa kusihindwa kufanya yale yanayoitwa maamuzi magumu. Katika moja ya tafsiri ya maamuzi magumu imekuwa ikisemekana kwamba bwana mkubwa anashindwa kuwaondoa baadhi ya viongozi katika chama na serikali kwa kuwa ni marafiki zake wa karibu. Baadhi ya matukio ambayo yanahusishwa na ufisadi ndani ya serikali na chama ni mkataba wa Dowans na fedha za Epa. Yapo majina ya watu kadhaa ambayo mara nyingi yamekuwa yakihusishwa na wanaharakati na wapinzani kuwa wanajihusisha na ufisadi.

Kwa mtizamo na uchambuzi wangu wanaotoa tuhuma hizi wamegawanyika katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni la wanaharakati wa haki za binaadamu na viongozi wa dini ambao wengi wao dhamira yao ni kutetea haki za wanyone. Kundi la pili ni la wanasiasa ambao wengi wao dhamira yao kuu (kwa maoni yangu) ni mafanikio ya kisiasa.

Kwa kundi la kwanza bila shaka hawawezi kukurupuka na kubeza harakati za CCM za kujivua magamba bila kuwa na ushahidi wa moja kwa moja kama ni za kujisafisha kisiasa tu bila kuwa na utashi kamili wa kutekeleza dhamira hiyo. Nionavyo mimi kipindi cha mwezi mmoja toka uamuzi huo ulipochukuliwa na baadhi ya hatua kuchukuliwa nI kidogo sana kuweza kutathimi dhamira yao. Kwa kundi la pili, kwa maoni yangu, kujivua gamba kwa CCM kama ni kwa dhamira njema ni kikwazo kwao. Maana mafanikio ya upinzani yamefanikishwa kwa kiasi kikubwa kutokana na udhaifu wa CCM zikiwemo tuhuma za ufisadi. Ndio maana asilimia sabini ya mazungumzo katika mikutano ya vyama vingi vya upinzani yametawaliwa na ufisadi wa chama tawala. Kwa hali ya kawaida ni kwamba wapinzani watakuwa wanakiombea chama tawala kisiwe na dhamira nzuri ya kuondoa ufisadi.
Ccm haihitaji kuombewa isiwe na dhamira nzuri, kwa sababu kihalisi haina dhamira nzuri. Mwenyekiti wake ni fisadi. Hiyo iko wazi hata kwa wanafunzi wa primary. Wabunge wao ambao 'walishinda' kwa ufisadi wakichukuliwa hatua ccm itakosa hata uhalali wa kutawala.
 
ukiongeza JK

Ni vigumu sana kwangu kuwabishia kuhusu hilo kwani mimi si mwanachama wa CCM na ninyi sijua mnauhusiano gani na CCM au viongozi wake kuweza kupata taarifa za ndani na nyeti kama hizo. Mimi kama msikilizaji na mchambuzi ninauwezo wa kuongea
kutokana na takwimu ninazoweza kuzipata katika vyanzo vinavyoaminika. Ndio maana bado nasisitiza kwamba ni mapema kuwahukumu CCM kwa hilo. Acha historia iwahukumu juu ya dhamira yao ya kujivua magamba. Kwa namna nilivyomsikiliza MKAMA, NAPE, MH MWAKYEMBE na MH RAISI sina sababu ya kutowaamini kwa sasa. Ninachoweza kufanya ni kukaa na kuwapa muda ili baadae niwahukumu kwa matendo yao sio kwa hisia zangu binafsi.
 
unajua bwanamkubwa tangu CCM itangaze hii move ya kujivua gamba jambo hilo limekuwa kama ndo falsafa ya ccm kwa sasa. Kwa mantiki hiyo, the fundamental question here is "kujivuagamba ni nini? na maswalimengine yatakafuatia. kwa hivo ni sahihi watu wanavoendelea kutafakari. Hii ni muhimu katika kondoa utata katika statement yaani maneno yaliyotumiwa na yanaashiria nini kulingana na hali halisi iliyopo. Let us be more critical about this.
 
unajua bwanamkubwa tangu CCM itangaze hii move ya kujivua gamba jambo hilo limekuwa kama ndo falsafa ya ccm kwa sasa. Kwa mantiki hiyo, the fundamental question here is "kujivuagamba ni nini? na maswalimengine yatakafuatia. kwa hivo ni sahihi watu wanavoendelea kutafakari. Hii ni muhimu katika kondoa utata katika statement yaani maneno yaliyotumiwa na yanaashiria nini kulingana na hali halisi iliyopo. Let us be more critical about this.

I agree with you kwamba critical analysis ya dhana yenyewe ni mhimu.

Kwa kadili nilivyowasikia wenyewe CCM katika ufafanuzi wao wa dhana ya kujivua magamba, wamekuwa wakianza kujenga hoja katika premises kwamba kwa kipindi cha miaka michache iliyopitita heshima na kukubalika kwa CCM kwa watanzania kumeshuka kwa kiwango cha kutisha. Na hilo, wanasema, limejidhihirisha wazi katika uchaguzi mkuu uliopita. Kisa cha yote hayo, wana CCM wanaendelea kujenga hoja, kinatokana na tuhuma za kuwemo ufisadi mkubwa ndani ya CCM, zinazowahusisha baadhi ya vigogo na wafadhili wakubwa wa CCM. Kama hali kama hii ikiendelea,wana CCM wanadhani, hatima ya chama katika siku za usoni itakuwa mbaya zaidi. Ili kuondoa yote haya, wanasema, kunaulazima wa kujiangalia upya na kuyaondoa yale yote yanayokifanya chama kionekane mbele ya wananchi hakina maana. Tatizo la kwanza na kubwa a kukabiliana nalo, kwa mujibu wa makada wa CCM ni ufisaji na/au tuhuma za ufisadi. Dhana ya kujivua gama inajengwa katika kuwaondoa katika uongozi wa chama wanachama mafisadi au wale wanaotuhumiwa kuwa mafisadi. Katika hili, kwa maoni yangu, kinachoangaliwa sana ni kuwepo kwa tuhuma kubwa za ufisadi, ambazo zimewafanya watu kuamini kwamba watu fulani katika CCM ni mafisadi. Bila kujali uwepo wa ushahidi wa moja kwa moja, wana CCM wameamua kuwaengua katika uongozi wa chama wale ambao kwenye macho ya wengi wanaonekana kuwa mafisadi. Kwa uelewa wangu na kusaidiwa na takwimu toka katika vyanzo mbalimbali dhana ya ufisadi ndivyo inavyoelezewa na waasisi wake.

Labda tuanzie hapo kuchambua
 
Sidhani kama kuna haja ya kuumiza kichwa kwa kutafuta falsafa pana katika hili. Labda kama CCM wanataka sasa kuingiza "ambiguity" kwenye dhana yao hii ya "kujivua gamba" ili kuzidi kubabaisha wachambuzi. Nilivyomsikia Mwenyekiti wa Chama (Mh. JK) mara ya kwanza alisema maneno yenye mwelekeo huu: "kuna wenzetu wamekuwa mzigo kwa Chama; hatuwezi kuendelea nao; itabidi wakae pembeni, watupishe tuimarishe Chama. Ni kama nyoka anayojivua gamba wakati inapobidi ili kukabliana na mazingira mapya". Ukijumlisha na yaliyotokea NEC, utaona ni dhahiri kuwa kwa kiasi kikubwa dhana hiyo imejikita kwenye kuwaengua wale wote wanaoonekana mzigo; wanaokipunguzia Chama umaarufu. Hapo ndipo dhana hiyo ilipoegemea zaidi. Walioipa uzito hawakukosea kwani kama ni mabadiliko endelevu ya kukiongezea Chama mvuto hayo yasingekuja na kauli "dramatic" kama zilizojitokeza safari hii baada ya uchaguzi wa 2010. Kwa kifupi ni kwamba CCM imepata pigo (hata la kihisia tu) kiasi kwamba inatafuta mkakati wa kimapinduzi (sio mabadiliko ya kawaida) ili kurejesha imani ya wananchi wengi (baada ya kugundua kwamba kweli wanazidi kuipoteza kwa kasi ambayo hawakutarajia).
 
:israel:Bye Bye CCM. Wahenga wamesema "siku ya kufa nyani miti yote inateleza" maana yake hapa tuseme "Mwaka wa kufa CCM mbinu zote zinakwama" sasa wewe umesema unajivua gamba, halafu ukavunja secretariat yako ukaunda nyingine haraka haraka, na yenyewe ikapita mikoani kwa kasi mpya na nguvu mpya kuelezea juu ya kujivua hilo gamba ambalo wala halieleweki kwa wadanganyika kwamba ni gamba la nyoka au la kobe. Mara mafisadi wakawanyooshea vidole mkaufyata na kuanza kuparurana wenyewe, Mara tumetaja majina ya mafisadi, mara hatukutaja huyu mwongo. Mara tumewapa mafisadi siku tisini wajitafakari, ooh mara hatujatoa siku tisini. Mbona hamueleweki????? kubalini yaishe ujanja wenu wadanganyika wameung'amua:israel:
 
Back
Top Bottom