Warioba na Salim walitulia baada ya kuona kuwa wale wenye makundi na wanaosemekana kupendelewa wametoswa.
Unajua Salim na Warioba washashughulikiwa sana na makundi ndani ya CCM.
Wanaamini kuwa Magufuli atanyoosha mambo hadi kieleweke.
Kuna ambao wangepitishwa wallahi wangelianzisha...hata mkapa na mwinyi washagoma kupiga kampeni..
Tafuta nyuzi za vikao vya wazee kabla ya utezi na updates zake alizokuwa anatoa Msekwa kwny media.
Unaposema Magufuli atanyoosha mambo hadi kieleweke unazungumzia kwa masuala ya ndani ya CCM au ndiyo ahadi anazotoa za kupambana na ufisadi, uzembe na uonevu serikalini?
Kwangu mimi, kama kweli atafanya hayo anayoahidi kwa Taifa (ambayo ndiyo yamekuwa yakipiganiwa na upinzani) basi ana kura yangu. Tatizo kubwa naloliona ahadi hizo ni kama kuipindua CCM yenyewe. Sijui wakubwa wa chama hicho watakuwa tayari kuruhusu mageuzi radical kiasi hicho? Ndio maana wengi wana mashaka kuwa hayo ni maneno ya kutafutia kura tu.
Huyu Lowassa hana haja ya Kuongea sana ye aingoje ikulu yake tu baaaaaas.
Ikulu ya monduri.. au ya hewan??
Ataishia kuisikia ukulu kwenye vyombo vya habari
Kwa kichwa kigumu kilichoshindwa kuzisoma nyakati hili suala la Lowassa kuingia ikulu ni ndoto lakini ni jepesi kinyume cha ugumu wa kichwa chako.
Ameshasema wamepwaya, mwenye macho haabiwi tazama. Wamepoteza wiki nzima ya kampeni huku uswazi wakatiwenzao wanakata mbuga.
Mzee Mwanakijiji,
Nilishawahi kulinena hili miaka mitatu nyuma nikisema Lowassa akiamua kugombea urais basi atashinda Monduli tu. Kwengineko in Tanzania Lowassa ni sumu na atachangia kwa kiwango kikubwa chama chake kushindwa katika uchaguzi. Nilishauri aachane na ulingo wa siasa ajikalie kama mbunge mpaka atakapotosheka nao anaweza kustaafu na kuwa mshauri. Narudia bado msimamo wangu ule ule kuwa active politics particularly urais is a bad move for Lowassa. Richmond haijasahaulika, Madudu ya wizara ya ardhi bado hayajasahaulika, na kwengineko. Kuna msemo mtu ukifanya mazuri ni rahisi watu kusahau but baya halisahauliki ndani ya mioyo ya watu. Nguvu ya pesa katika urais ni kugumu maana sio rahisi kuhonga watu milioni 20 wakupigie kura wewe labda uwe na utajiri kama wa Bill Gates.
Hata hivyo mie ningelifurahi akagombea ili CCM kiwe chama cha upinzani kwani wamejisahau sana na kufanya madudu mengi. Ni wakati muafaka tupate chama cha upinzani tubadilishe kidogo taswira ya nyumba yetu ya Tanzania.
Ufunguzi umeisha sema.
Pasco
hapo mwanzo nlikuwa nkiona watu wanajiita great thinkers but what they post and discuss vilikuwa agaist what they claim to be,,but now nmegundua kuwa kuna great thinkers kweli,na kuna kenge ambao wengi wamejoin recently,,but cio wote waliojoin recent ni kenge na wafata mkumbo,,ila wengi waoo!!!!uzi haukuwa na biaz m2 ameeleza fact then great thinkers wanachambua bila hamasa!!!god bless tanzania na kila aitakiaye heri nchi yetu.
Kwenye hii mada namrudushia Mungu utukufu! Na ninaamini bado unabii utatimia tu. Hata uchelewe vipi! There is a prophecy on our country, a prophecy that WILL be fulfilled. And in that prophecy Lowassa is not in it. It doesn't matter millions bow before him.