Tafadhali baada ya Simba Day naomba 'Utamaduni' huu mzuri wa Marehemu Mzee Wetu 'Bamchawi' urejewe

Status
Not open for further replies.

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,892
109,614
GENTAMYCINE naomba baada tu ya Tamasha Kubwa la Simba Day tarehe 6 August, 2023 mambo haya Mawili muhimu sana yafanyike kabla Timu haijaenda Tanga kwa Mechi za Ngao ya Jamii na kuanza kwa Ligi Kuu ya NBC na Michuano Miwili ya Kimataifa.....

1. Waitwe Wazee Wetu wa Kikwajuni Zanzibar na Wazee Maalum wa Tanzania Bara wasome Kitabu ( Dua Kali ) kisha ipikwe Yamini na Walambishwe Wachezaji wote, Benchi la Ufundi na Viongozi wote wa Simba SC kisha Waambiwe ambaye atahujumu / ataihujumu Timu Akifa au akirukwa na Akili asimlaumu Mtu.

2. Wachezaji wa Simba SC waambiwe mubashara ( tena bila ya kuwaonea Aibu ) kuwa Wakiroga basi Waroge ili tu Wasiumie ( wasipate Majeraha ) ila kamwe wasije wakawa Wanarogana ( Wanachawiana ) Wao kwa Wao.

Watoto wa juzi ( miaka ya karibuni ) najua hapa mtanishangaa sana GENTAMYCINE kwa hiki nilichokiandika hapa ila kwa wale Wakongwe Wenzagu najua Watanielewa vyema nilichokimaanisha

Sikumbuki ni lini Simba SC iliyokuwa chini ya Muasisi wa Utamaduni huu Marehemu Mzee Bamchawi iliukosa Ubingwa wa Ligi Kuu, haikufika mbali katika Michuano ya Kimataifa na ilifungwa na Mtani wake Yanga SC.

Naomba hili lifanyike na lizingatiwe.
 
Yani Kuna watu wengine ni wapuuzi sana.


1. Kakolanya kaondoka, MANURA kaumia tangu MSIMU uliopita hakuna MBADALA wao Hadi Leo.

2. Simba ilishindwa kwa YAHAYA Mbegu kumsaidia shabalala..

3. Simba Haina Beki wa maana wa Kumchallange Inonga na Malone.

4. Simba Haina kiungo Mkabaji Tangu KUUMIA Kwa Lwanga. ( 6)

5. Simba Haina mshambuliaji WA MAANA zaidi ya Baleke.

BADALA YAKE SIMBA IMESAJILI MAWINGA 11.

KAANGALIE YANGA NA AZAMU WALIVYO TIMIA.

SIMBA HATA IROGE VIPI HAIWEZI KUMFUNGA MANCHESTER CITY.

Kama UCHAWI ungekuwa unachezaa mpira Nigeria wangekuwa na Kila kombe Dunia.
 
Kakolanya kaondoka. Simba ilishindwa kwa YAHAYA Mbegu kumsaidia shabalala.. Simba Haina Beki wa maana wa Kumchallange Inonga na Malone. Simba Haina kiungo Mkabaji Tangu KUUMIA Kwa Lwanga. Simba Haina mshambuliaji WA MAANA zaidi ya Baleke. BADALA YAKE SIMBA IMESAJILI MAWINGA 11.
Inaonekana ungekuwa kiongozi wa Simba, ungesajili wachezaji 50
 
Huyu ndiye think tank wa thimba.....!!!, Inasikitisha kuona huyu ndiye alipata tuzo hapa Jf

Huyu ndugu yangu utamuweza! Hata ligi haijaanza ashaanza kushauri waroge kisa tu manara, barbara na kiongozi wao mkuu walikua wanatoa siri za kambi kwa yanga
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom