TABlA YA WANA JAMII FORUMS

Kumbe nawe mmoja wao. Ukweli umefika japo unauma.

Btw, acheni basi na kamtindo ka kudandia mada na kupotezea mtiririko kwa kuingiza habari zenu za baa na mahaba.

Tumeshaacha dada. Tusamehe bure.

Karibu Viola PUb jioni leo nikununulie taska baridi na kokoto. Huwezi jua mambo ya mila.................
 
Sikujua kama wewe ni mpenzi wa jukwaa la mahusiano na pia sifa za watu wa jukwaa hilo ni pamoja na kukaribishana chai na vikaoni baa. Asante kwa upendo wako kunifumbua macho kuhusu jukwaa ulilolitaja.

Naam! Ukarimu sio sifa ni Tabia ndugu yangu; I hope umeelimika vinginevyo nikupe POLE nyingine tena!
 
Kila jamii ina tabia zake.
Ukienda kwa maaskari wanakuwa na tabia yao ya ujumla ambayo huitwa haiba.
Ukienda kwa waalimu hali kadhalika wana haiba au tabia yao.
Ukienda kwa wanafunzi ni hivyo hivyo.
Hapa kwetu. J. F. Kuna watu kutoka makundi mbalimbali,
je tukikaa kwa pamoja tutaibua tabia gani?

Griti sinka!!!
 
Jukwaa la SIASA-Opportunist (some)
Jukwaa la Mapenzi-wanafamilia
Jukwaa la DINI-WATATA WALE(Iko siku watatoana macho)
Jukwaa la science na technolojia-wazee wa 10%
Jukwaa la itelijensia-no comment kwa hawa watu

etc
Wana JF,
Aliyeanzisha mada anataka kujua makundi haya yote kwa ujumla wake, combined together, yatatoa tabia ganiza ujumla? hajasema kila jukwaa tulinyambulishe tabia zake,... sababu ni obvious kuwa jukwaa la ampenzi lazima lina watu wanaopendana, dini wanaohiltilafiana kiimani, siasa n.k.! JF kama kundi moja tu la watu, say uwakusanye wote wakae wote kwa pamoja kwa mwezi mzima, wote au wengi wao, wamanifest tabia zipi?
 
Composition ya wana JF I gesi iko hivi -watumishi wa serikali na mashirika ya umma (si dhani kama kuna wanajeshi na walimu wa shule za msingi hapa kama wapo wachache)---ni watu wa daraja la kati na la juu wachache....kuna wana siasa , wabunge, ma dc. madiwani nk, mainjinia wachache pia...manesi nadhani hakuna kabisa, wauza mitumba pia na mashaka hawapo.....pia umri wao ni kati miaka 24yrs-75yrs
kuna wastaafu wachache.....kuna mawakala wa mafisadi.....waandishi wa habari wengi zaidi bila kusahau wanafunzi walio nje ya nchi. KWA UPANDE WA JINSIA NADHANI WANAUME NI WENGI ZAIDI
-
....kitabia
1) Wengi ni vipanga sana (very intelijenti pipo)
1) ni watu wamanung'uniko kila jambo linalofanywa na wasiowakubali hata kama ni la heri basi ni threat kwao
2) Ni watu wenye huruma na huguswa na matukio yanayoamsha hisia sana ila kama linahusu dini huruma zao huenda kando
3) Ni wa dini kwa haiba
4) Si waoga kutetea wanachoamini
5) Ni wasomi na mahiri
6) Ni wacheshi, wapenda amani
7) Ni wachunguzi wa mambo ngumu kuwadanganya
8) Wengi ni wazalendo wenye mwamko unaoleta matumaini ya kesho
9) Sina hakika kama wanapenda au wanachukia 'MUUNGANO"
10) Wakiondoa imani kwa mtu ngumu kuirudisha
 
Kwanini isianzishwe siku moja ambayo watu wa jf watakutana na kwa kifupi kila mmoja apewe kadi yake yenye namba pekee kwani najua wengine wakiambiwa wapewe kadi zenye majina basi hawatashiriki kabisa tamasha hilo. nadhani hii itakuwa ni mwanzo wa kufanya jf ni sehemu ya kujenga na kuunganisha watu
 
Godwine hata mimi niliwaza hivyo lakini je wewe godwine kama wewe ni 6 au EL utakuja? nahisi wengi hawatakuja wakihofia title zao na maoni yao hapa.
mix with yours
 
Ha ha ha, kapwani; mix with yours, ndio changanya na zako hiyo? Teh a.k.a Mbayuwayu
 
Godwine hata mimi niliwaza hivyo lakini je wewe godwine kama wewe ni 6 au EL utakuja? nahisi wengi hawatakuja wakihofia title zao na maoni yao hapa.
mix with yours

mimi wakifanya tamasha nitakuja kwani maranyingi napenda kushiriki matamasha mbalimbali ya jamii na pamoja
 
Utafiti wa kina inabidi ufanyike ili hili liweze kuwa solved
Kila jamii ina tabia zake.
Ukienda kwa maaskari wanakuwa na tabia yao ya ujumla ambayo huitwa haiba.
Ukienda kwa waalimu hali kadhalika wana haiba au tabia yao.
Ukienda kwa wanafunzi ni hivyo hivyo.
Hapa kwetu. J. F. Kuna watu kutoka makundi mbalimbali,
je tukikaa kwa pamoja tutaibua tabia gani?
 
Kila jamii ina tabia zake.
Ukienda kwa maaskari wanakuwa na tabia yao ya ujumla ambayo huitwa haiba.
Ukienda kwa waalimu hali kadhalika wana haiba au tabia yao.
Ukienda kwa wanafunzi ni hivyo hivyo.
Hapa kwetu. J. F. Kuna watu kutoka makundi mbalimbali,
je tukikaa kwa pamoja tutaibua tabia gani?

.
Engels and demons discussing defferent issues without fighting each other.(friction force)
 
Hivi Acid wewe ni nani ghafla bin vuu naona Tindikali mbona umebadili jina . mheshimiwa...ama hizi ndio mojawapo ya Tabia za JF?

'Afu mwanzo alikuwa na Corrosive Nature.... 'sa ivi kawa Acid tu....:disapointed:
 
Jukwaa la mahusiano, mapenzi na urafiki - hawa wana tabia ya kujaliana, kupendana na ni wanafamilia kwa ujumla, hawaogopani na wengi wao wanafahamiana kwa sura na hata familia zao zinafahamiana. Ni wacheshi hawana jazba japo kuna baadhi ya watu huwa wanajaribu kuwachafulia hali ya hewa kwenye jukwaa lao lakini wao huwa wapole na waelewa.
Kwakuwa mimi ni mgeni humu hata week sijamaliza kama Tabia ni hizo hapo PRETA basi hakuna shaka ni watu wa kuigwa katika jamii ya sasa.
 
Back
Top Bottom