Tabia za watu zinazonikera

Aisee mimi kama bin Adam hzi tabia kwa kweli zinanikera sana...

1. Kuchungulia mtu anaoga bafuni

2. Kusoma SMS inayoandikwa na mtu asiyekuhusu wala hamjuani

3. Kujitapa kwa vitu usivyokuwa navyo kama vile kujidai umesoma au unamiliki gari wakati siyo

4. Mtu kukataa asili yake au kukana ndugu zake

5. Wapenzi wanaosimulia kwa wengine jinsi walivyofanya ngono na wenzi wao usiku uliopita

6. Mgeni kuwasha TV au kufungua friji bila ya kuruhusiwa na mwenyeji wake

7. Watu wanaoongea mambo yao binafsi ya mahusiano kwenye usafiri wa Umma

8. Watu wanopenda kuvaliana nguo za ndani au kuazimana nguo na viatu

9. Wenzi wanaopiga mayowe wakati wa ku..do ilhali wanajua wanaishi kwenye nyumba isiyo na dari
10, Watu wanaoporomosha matusi hadharani bila ya kujali hadhira iliyopo mchanganyiko wake ukoje.

Kama na wewe una tabia kama hizi tafadhali sana USINIKWAZE!!

5. Inakuwaje mtu mnajifungia chimbani mmeduu for your own interest, pleasure and sectrecy afu mkimaliza ukamtangaze mwenzio?

Hii kweli lazima ikere..ni tabia mbaya saaaaana
 
mkuu naona ya sita kama uchoyo vile...kwani tv nini bana YANI ukiwa haupo watu kwa vile wageni tusiangalie tv,ungeifungia chumbani au utie kufuli ka labaaa
 
Wananikera wale wenye kupenda kuchukua cm za wanzao na kuanza kusoma vilivyomo siwapendi mnanikeraaaaaaaaaa
 
Nakerekaga
1. Tabia ya mtu kupanda kwenye daladala huku kavaa vest na hajanyoa jikwapa lake halafu umkute kasimama kashikia bomba
2. Kutoa hewa chafu kwenye mjumuiiko wa watu wengi
3. Kupenga makam**i kwa mkono halafu mtu anajifutia nguoni au anafikicha mikono... Majitu kama haya huwa ya kwanza kutoa mkono yakikutana na watu

Hiyo ya kwapa hahahahaha ni mbaya unaeza hata upate kichefchef
 
1.Kukojoa halafu ukimaliza unamsalimia mtu kwa mkono.

2. Kuingiza kidole puani halafu unampa mtu mkono.

3. Kutoa makohozi wakati wa kula.

4. Kusimulia movie wakati wenzako wanaitazama mara ya kwanza.

5. kubeep beep kila mara.

6. Kudanganya kwenye simu, niko hapo nakuja kumbe ndio unatoka home.

7. Kukaa siti ya nyuma na kuanza kuweka mikono mbele kwa mtu aliyekaa siti ya mbele.

8. Kuuliza uliza nyakati kila mara, " sasa hivi ni saa ngapi??, sasa hivi ni saa ngapi?? bado dakika ngapi?? "

9. Kutembelea wenzako nyakati za msosi. Ikifika saa sita tu tayari ushafika, halafu stori nyingi, huondoki tu tule.

10. Kukojoa bara barani.

asilimia kubwa ya wabongo tuna hizi tabia zinakera
 
Hahahahahahahahahahaha

JF is never boring

Ha ha haa, mkuu nyingine kuna jamaa wanakera sana kujifanya wao usalama, au polisi au wanajeshi utasikia akimpiga mwenzake mkwara, unanijua mimi wewe?? nitakufunga!!! aaa mambo gani hayo bana, tuache hizo..
 
1. Mademu wanaopenda kupiga mikuki (Kuomba omba hovyo) ref. Mamndenyi.

2. Kukuna map.mbu yako kisha kunipa mkono wako. ref. Bishanga

3. Kujifanya kila kitu unajua. Kila stori unachangia ref. Lady doctor

4. Kukopa halafu kulipa unazingua. ref. chama.

5. Invisible kunipa BAN kisa nilikataa kumkopesha.

6.

7.

8.

n.k
haha mkuu hiyo namba 5, inaonekana umemiss sana ban, ngoja mkuu akuje pande hizi arekebishe
 
namba 4. hapo pana utata wewe mwenyewe magumashi matupu unaishi kimjinimjini huna lolote sioni ulichonacho cha kukopwa Chama anakopa Barclays bank na anautaratibu mzuri tu wa kulipa madeni yake na hadaiwi na mtu yoyote!
 
namba 4. hapo pana utata wewe mwenyewe magumashi matupu unaishi kimjinimjini huna lolote sioni ulichonacho cha kukopwa Chama anakopa Barclays bank na anautaratibu mzuri tu wa kulipa madeni yake na hadaiwi na mtu yoyote!


chama.
Au unataka niweke clips za mazingumzo yetu!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom