SoC03 Uwajibikaji kwa kila mtu

Stories of Change - 2023 Competition

James White7

New Member
Jun 4, 2023
1
0
Mnamo mwaka 2018 ni kiwa kwenye daladala nikiwa narudi nyumbani,ndani ya gari kulikuwa na watu wakilalamika juu ya kiongozi katika taasisi fulani,Watu hao walikuwa wanalalamika sana wakisema"Yule jamaa angekuwa anawajibika ipasavyo tungefanikiwa sana,anatukwamisha sana".Mara ghafla moja Kati ya hai Watu walikuwa wanalalamika akasema huku Kama akitafakali kwa makini alisema hivi "Je sisi tumefanya jitiada gani katika Mambo ambayo tunayaweza ambayo ayahitaji Msaada wa yule jamaa?" Ndipo wale wenzie Wanasema hivi "Kweli sisi wa Bongo tunapenda lawama sana,ulivyosema mwanetu Ni kweli".tangu siku hiyo nikajua ya kwamba kila mtu katika familia,taifa au Dini anaowajibu fulani wakufanya,ingawa wajibu unatofautiana kiukubwa kwa kila mtu.

Neno uwajibikaji nimelitafsiri Kama hivi Ni kitendo Cha mtu kujua nafasi yake na majukumu yake ya kufanya Mahali fulani na wakati fulani uliosahihi. Nitaongerea wajibu wa viongozi wa taifa,viongozi wa Dini na viongozi wa famili (Baba na Mama n.k).Kwa asilimia kubwa andiko langu litagusa kila mtu kwa maana kila mtu hapa Duniani anawajibu wa kufanya katika jamii fulani.

Wajibu wa viongozi wa taifa;
Viongozi wa taifa wamepewa dhamana za kusimamia wale wanaowaongoza.
Viongozi wa taifa wanapaswa kujua wanapofanya wajibu wao Basi maendeleo katika taifa yatapatikana huenda kwa kuchelewa lakini yatakapotokea yatakuwa na faida na kumbukumbu kubwa kwa kizazi hiki na kijacho.

Viongozi wanapaswa kujinyima na kutokubali ufisadi ,rushwa na kutowapa nafasi Maadui,hivi ni vitu hatari kwa taifa kwa sababu vitu hivi vina Raha kuvipata lakini vina hasara ya muda mrefu.

Piga picha Kama wazee wetu wazamani wasingetunza misitu fulani muhimu ingekuwaje,kwa sababu wazee wetu wajua umuhimu na wajibu wao Basi walitunga Sheria na kuweka nguvu fulani kusudi ili kulinda maliasili hizo muhimu. Kwa wale wapare nafikili wanielewa,kule upale Kuna msitu unaitwa Shengena ilikuwa uwezi kufanya uharibifu enzi hizo kwa sababu ulikuwa unamizimu ya mababu inayolinda Mali hizo hivyo ilikuwa ngumu kuchukua mali zilizopo humo au kufanya uharibifu.

Faida itakayopatikuwepo endapo viongozi watajua wajibu wao Basi itawafanya wananchi au watawaliwa kuwa na Moyo wa kujituma lakini itakuwa faida kwa kizazi kijacho. Viongozi watakao fanya wajibu wao watakuwa na Amani Moyoni baada ya kumaliza majukumu yao kwa sababu awanahatia yoyote inayowasumbua juu ya Uongozi wao.Mungu pia atawalipa wale Viongozi wote watakaofanya vyema maana sisi wote tu Mali ya Mungu.

Wajibu wa viongozi wa Dini;
Miaka ya hivi karibuni Nimeona viongozi wa Dini wakiwa wamejihusisha na siasa,wakufanya biashara kuliko kufundisha yaliyo kweli na kuendekeza anasa kuliko kumpendeza Mungu wao.

Wapendwa Viongozi wa Dini hampasi kujihusisha na siasa jukumu lenu Ni kuongoza Watu kumfahamu yule anaepaswa kuabudiwa.dini na siasa au serikali vukiungana Ni Jambo hatari ndio maana taifa la Marekani lilipoanza kwa Mara ya kwanza halikuunganisha siasa na Dini,Dini zikiungana na siasa Ni rahisi kutokea machafuko na maasi. Nyerere alichokifanya Ni kitu kizuri sana kwa kuifanya taifa hili lisiwe na dini alisema Watu taifa lake halina Dini lakini Watu wake Wana dini,alichokiamua Mw Nyerere nilikuwa na maana ya kipekee sana.

Viongozi wa Dini mnapaswa kuwaonhoza Watu mnaowaongoza kukifahamu kweli juu ya Mungu na kuwafundisha Watu kuenenda katika tabia Safi na mwenendo mwema. Maadili kumomonyoka katika jamii ,familia na taifa yanaweza kupungua endapo kila kiongozi wa Dini atachukua nafasi take Kama kiongozi wa Dini.

Mungu atawadai viongozi wa Dini amtawajibika ipasavyo,Ni heri mkatae majukumu yenu kuliko kukubali alafu kutowajibika. Mungu atawabariki viongozi wote wafanyao vyema na watazalisha jamii Safi.

Viongozi wa Dini mnapaswa kujua mna wito nilipitiwa ni kuwaonhoza Watu kumfahamu Mungu. Taifa lenye viongozi wazuri wa Dini Basi taifa Hilo litabarikiwa na litakiwa na maadili mema. Viongozi wa Dini siasa aiwahusu kazi yenu Ni kuwaombea wanasisa sio kujiingiza katika siasa.

Viongozi katika familia;
Wazazi/walezi wengi wamejikita zaidi kutafuta fedha zaidi kuliko kusimamia familia zao juu ya maadili ndio maana kumeibuka na fukuto la Watoto na vijana ambao Ni mzigo katika taifa letu.

Pia wapo wazazi ambao wamejikita katika uvivu wakiendekeza starehe na kusahau familia zao na kusababisha familia kupata magonjwa hata kifo na umasikini.

Wazazi/walezi Yani Baba na Mama wanatakiwa kujua wamepewa jukumu la juwalea Watoto wao kwa maana wao ndio walio waleta Duniani,endapo awatawatunza vyema Basi wanalo Deni Mbele za Mungu muumbaji wa Mbinguni na nchi pia watazalisha kiazi hatari ambacho kitakuwa hatari kisichofaa.

Baba inampasa kuwapenda Watu wa familia take,Mama kumtii mumewe na kulea familia.Baba na mama inawqpasa kusaidia kulea familia kwa kila nyanja za maisha.

Vijana Yani kaka na Dada au wote waliowakubwa inawqpasa kuwaongoza wadogo zao kufanya vile ulivyo sahihi,Baba na Mama wakati Mwingine ulemewa na majukumu hivyo vijana wakubwa wanalojukumu la kuwasaidia wadogo zao ili wawe vijana Bora badae.

Hebu wazazi/walezi msisahau kukaa karibu na Watoto wenu na kuwalea Simaanishi msitafute pesa,tafuteni pesa kwa bidii ili kumbukeni malezi ya Watoto wenu .Pesa nyingi itasaidia Nini ikiwa Watoto watakuwa Watu wasiofaa.

Nimeona Watoto wakitoa machozi kwa sababu wazazi wao awakuchukua wajibu wao oooh Nimeona baadhi ya Raia wakiumia na kulia kwa uchungu kwa sababu viongozi wao awakuwajibika ipasavyo oooh Nimeona Vijana wakiharibika Ila kwa sababu viongozi wa Dini waliwakwaza na kuwaumiza oooh nimeona.inasikitisha sana.

Mungu anisaidie Mungu akusaidie tufanye na tujue wajibu wetu. Amen
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom