Tabia ya kutumia watoto wadogo kuomba misaada mtaani haivumiliki

Meneja CoLtd

Member
Mar 6, 2021
60
59
Sasa hivi kumekua na ongezeko kubwa la baadhi wa watu kuwatumia watoto wadogo kujipatia kipato kwa kuomba omba.

Wengi kati ya hao wanao ombaomba wanaonekana wanauhitaji wa chakula na fedha.

Lakini hili la kuwatumia watoto wadogo kuomba omba binafsi linaniuzi kwani naona kama ni udhalilishaji.

NB: SIKATAI WATU KUOMBA LAKINI HILI LA KUWATUMIA WATOTO WADOGO SIDHANI KAMA TUNAJENGA TAIFA.

Kama kunauwezekano mamlaka husika ingelitafutia ufumbuzi hili jambo.
 
Iwe ni watoto wadogo au watu wazima hawatakiwi kuwa OMBAOMBA Mitaani na mabarabarani

Kama serikali imeweza kujenga rehabilitation centers, Magereza ya watu wazima na watoto...wake kwa waume, hospitali ya Vichaa Mirembe na ina bajeti kwanini isijenge maeneo rasmi ya kuwahudumia hawa watu na wawekewe bajeti?

Ombaomba wengine ni wazima kabisa na wana nguvu ya kutafuta riziki ila wavivu

Tukiwapa vihela mitaani na barabarani watazidi kuongezeka wengi na kwa kasi
 
bbc swahili africa eye washalionesha ila serikali zetu zipo kimya
 
Iwe ni watoto wadogo au watu wazima hawatakiwi kuwa OMBAOMBA Mitaani na mabarabarani

Kama serikali imeweza kujenga rehabilitation centers, Magereza ya watu wazima na watoto...wake kwa waume, hospitali ya Vichaa Mirembe na ina bajeti kwanini isijenge maeneo rasmi ya kuwahudumia hawa watu na wawekewe bajeti?

Ombaomba wengine ni wazima kabisa na wana nguvu ya kutafuta riziki ila wavivu

Tukiwapa vihela mitaani na barabarani watazidi kuongezeka wengi na kwa kasi
serikali imekosa mipango mikakati , ilikuwa inawezekana wakafungua production units na kuwaajili hawa watu pia kuwawekea makazi yao binafsi maeneo hayo hayo ya production units ila ndo hivyo tuna serikali kipofu isiyoweza hata kuendesha bandari wala kusimamia misitu
 
Back
Top Bottom