Makuzi ya watoto yanaharibiwa na Teknolojia kama haitasimamiwa na wazazi!

McCollum

JF-Expert Member
Jan 10, 2023
384
679
Habari za Jumapili, ni matumaini yangu muwazima wa afya. Siku ya leo naomba nijadili nanyi au kiwasogezea mada hii "Makuzi ya watoto yanaharibiwa na Teknolojia kama haitasimamiwa na wazazi!"

Awali ya yote nipende kuanza kwa kusema, maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ya sasa yanafanya wananchi wa nchi mbalimbali duniani kujipatia uraia kwenye nchi moja (nchi ya Sayansi na Teknolojia).
download (1).jpeg


Naomba kuanza, kwa miaka ya kuanzia 2015 na kusonga mbele kumekuwa na ongezeko kubwa la watumiaji wa simu janja (Smartphone) nchini Tanzania. Na kwa mujibu wa mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania-TCRA, kwa mwaka 2022 mwezi Septemba watumiaji wa Internet walifikia 31.1 milioni.
images (1).jpeg



Kwasasa limekiwa jambo la kawaida kwa wazazi kuwaachia watoto wao wadogo ambao hawana ufahamu wa kutambua kipi cha kutazama na kusikiliza na wanapokuwa mtandaoni wao ni "kubofya" tu vitu wanavyoviona. Kwasasa imekuwa kama sifa kukutana na mzazi anayeongea maneno haya "Junior anaijua simu huyo, yaani anaweza kuingia YouTube na kutafuta kitu chochote", what a shame! Mzazi anamsifia mtoto wake kuwa na uwezo wa kutafuta chochote bila kujua huwa anaangalia nini.

Nitaliweka hili jambo sawa kwa mifamo dhahiri.

Mfano wa kwanza.
Mwezi wa sita wakati wa likizo ndefu kuna mzazi alinitafuta akiniomba nimsaidie kumfundishia kijana wake ambaye kwa mwaka huu yupo kidato cha pili, kutokana na kujishughulisha na shughuli nyingine wakati wa mchana (kujaribu kuziba pengo la u-jobless) nikakubaliana naye kuwa mtoto wake awe anakuja majira ya saa 12 jioni. Baada ya kumfundisha kijana yule kwa wiki niligundua alikuwa mtu ambaye attention span yake haizidi dakika 5 baada ya hapo anakuacha ukiwa unaongea wewe mwenyewe, hata unapompa kazi ya kufanya nyumbani (Take Home Activity) akirudi siku ijayo anasema sikupata muda wa kufanya na kutoa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu. Nikaona nijaribu kuangalia labda anabanwa na masomo nako nikaona hola!, kwani mtihani wa kuingilia kidato cha pili alipata division 0 ila kwakuwa ni shule ya Serikali hakukuwa na mtu wa kumrudisha form one na ukizingatia nfo kwanza ni shule mpya ambayo wao ndio waanzilishi.
images.jpeg


Ikabidi nijipe muda wa kumfuatilia kwa undani na hapo ndipo nilipokutana na vituko, kijana huyu mdogo about 14 anamiliki simu yake na mama yake ndiye anayempatia pesa ya kuungia vifurushi vya Internet na baada ya hapo anaendelea kufanya surfing and the stuffs na mengine mengi, kumiliki simu si kosa ila shida ni kwamba kumiliki kwake simu kilimeza asilimia 80 ya muda wake wote wa masomo na hivyo alikuwa akisoma kwa dakika kadhaa na kuenda kulala and then siku ingekuwa imeisha. Kama mdau wa Elimu nilijaribu kuongea na mama yake lakini hakukuwa na response yoyote nikaona fresh niendelee na mambo yangu na nisipoteze nguvu yangu, nikamwambia yule dogo kwamba kwasasa nipo bize sana kwahivyo Tuition ikawa imeisha hivyo.
Taarifa hazinabadirika na bado kijana anauburuza mkia wa darasa kwakuwa wamwisho kila siku, bahati mbaya baba yake alifariki mwanzoni mwa mwaka huu na yeye ndiye wakiume pekee na mama yake ndiye aliyebakia ambaye naye anafanya kazi ambayo almost mshahara wake mwingi anautumia kwenye familia na sidhani kama anabakiwa na extra. Baba aliwaacha katika nyumba ya kupanga, dada wa huyo kijana wote wawili wapo nyumbani na walifanya vibaya kwenye mtihani wa kidato cha nne na wameshindwa kumsimamia mdogo wao ila wanamwacha ajikuze.
images (2).jpeg



Wazazi wasiamini kama hizi ios na android OS zitawalelea watoto wao.
download.jpeg
 
Picha zote ni za watoto wa kizungu tu..

Hii ina maana kubwa sana, Afrika bado sana kuathiriwa negatively na teknolojia
 
Umenena vema mkuu but hii ina waathiri zaidi watoto wa English Medium kwa sababu wanaanza kusurf wakiwa darasa la nne ambapo tayari wanakuwa wanaijua " internet language"

Watoto wa kayumba haiwaathiri sana coz wanalelewa kimaadili ya kitanzania plus hawajui kiingereza so mambo ya kucheza na simu kuangalia vitu vibaya kwenye simu kwao inakuwa ngumu kidogo.
 
Picha zote ni za watoto wa kizungu tu..

Hii ina maana kubwa sana, Afrika bado sana kuathiriwa negatively na teknolojia
Na nyie mtafikiwa tu coz mnawalea watoto wenu kizungu mnawasomesha shule za kiingereza tangu wakiwa primary. Nyerere hakuwa mjinga kuweka kiswahili iwe lugha ya kufundishia shule ya Msingi. Hakutaka watoto wakue kabla ya wakati wao
 
Back
Top Bottom