Boflo
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 4,384
- 4,409
Hivi kwa nini wabongo wengi wana tabia ya kuchungulia wallet? Ninasema haya kwa sababu yameshanitokea sehemu nyingi, kama ukienda saloon(kiume au kike) ukitoa wallet kama unataka kulipa utaona watu wanachungulia wallet yako, wakiona manoti yamejipanga, utaanza kuambiwa naomba chenji??, au utaona Janadume zima linajipendekeza kwako na kuanza kujichekesha chekesha na kukusifia, hata ukienda bar, shopping centre, ukitoa wallet ilonona, utaona mijitu inakodoa macho utadhani wanalenga manati !! Hii tabia si nzuri tujirekebishe jamani, hii tabia ndiyo inayosababisha Wanawake wengi kumegwa kirahisi na Wanaume kuwa si rizki.