Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,681
- 1,698
Jumamosi tarehe 26/01/2013 nikiwa ofisini mida ya saa mbili usiku mie na jamaa zangu tukisubiri kusikiliza taarifa ya habari (StarTv) jamaa yetu mmoja akingia na watu watatu (mwanamke mmoja) wakiwa na laptops na video camera na kuanza kutafuta switchsockets ili kucharge.
Mwanamke akaenda moja kwa moja kwenye tv na kuizima na kuchomeka charger ya kilaptop chake na kutuacha wenyeji tukiduwaa na hatua hiyo.
Kwa kweli ilituuma mno na sikuvumilia, nikamuomba atafute pengine kwani switchsockets zipo nyingi cha ajabu mdada akasema sisi ndo tutafute pahala pengine pa kuangalia/kusikiliza taarifa hiyo ya habari. Sikuvumilia na niliamka kwenda toa charger yake na kuwasha tv. Baadae mmoja wao akaniambia yule mdada ni Ufoo Saro wa ITV, tulishangaa sana kwa tabia hiyo na kujiuliza mbona busara hana au kwa kuwa ni mwandishi wa habari (tena ITV) au katoka Mzizima (Dar) na kutudharau wa mikoani?
Sasa kama mtu ambae hana simile si angemzaba kibao?