Tabia ambazo hawazipendi wanaume toka Kwa wake zao

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,528
6,525
Habar Wana Jf.

Dada zangu wanaume hatupendi mtufanye kama mama zetu, hatupendi kuongozwa/ kusimamiwa, haya ndio makosa ambayo wanawake wengi wanayafanya katika ndoa zao.

Mwanamke ukiwa na Tabia ya kutaka kumkontroo mume wako basi ujue unakaribisha sinto fahamu katika ndoa yako,labda niwasaidie kitu kimoja mkifahamu kuhusu wanaume.

Wanaume wameumbwa kudili na mambo yao wenyewe,kama ni changamoto au mapungufu basi ujue atataka kudili nayo yeye mwenyewe na ndio maana ni mara chache Sana ukute mwanaume anaenda Kwa mwanaume mwenzake kumuelezea matatizo yake,huwa mara nyingi tunapambana na Hali zetu wenyewe,na ikitokea mwanaume ameenda kuomba ushauri sehemu juu ya changamoto zake basi ujue ameshibana kweli na huyo mtu.

Sasa basi mwanaume wako anapokuwa na changamoto Fulani,usijitie unamtafutia solution Kwa kumuelezea nini cha kufanya,hapo bwana unafeli,hapo mwanaume anaona kama Una mdharau na kuona anashindwa kujisimamia yeye mwenyewe,anaona kama unamvunjia heshima .

Unachotakiwa kufanya ni kutoa ushauri mdogo tu na isionekane kama unasisitiza Hilo Jambo lako,Kwa kutoa ushauri inaweza kumpa nafasi ya kutafakari na kulifanyia kazi Jambo lako,na usiwe na haraka ya kuona anafanya mabadiliko haraka,kuwa na subira muache afanye pale anapoona inafaa.

Na ukifanikiwa katika hilo ataona unamheshimu na kumuamini na kuna nafasi kubwa ya kufuata ushauri wako,mfano mmeenda out na huko hakuwa na heshima labda Kwa maneno yake au vitendo vyake,ukirudi home usimwambie mume wangu sipendi Tabia uliyoionyesha Leo siku nyingine usirudie tena,no sister!! unafeli hapo ni Sawa na kujifanya wewe ni mama yeke,mwambie hivi mume wangu Leo sijapendezewa na kile kilichotokea pale,yatosha itamfanya ajitafakari na kuna uwezekano mkubwa asirudie tena next time huo ni mfano Tu.

Mtambue kwamba wanaume ndio kichwa cha familia kwahiyo kiasili tu tunaamini Sisi ndio kila kitu,kwahiyo uchague maneno ambayo yatarekebisha Tabia ya mwanaume Bila kujihisi kama Una mkontroo.

Ukilazimisha kumkontroo anaweza kufanya Jambo lako Kwa kipindi Fulani kwakuwa unafosi hivyo lkn baada ya Mda Fulani atarudia mambo Yale Yale.

Ni hayo Tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom