Taasisi za Serikali zashauriwa kushirikisha Serikali za Mtaa ili kuzuia uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049

Kikao kilichoandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kikishirikisha Wadau mbalimbali kujadili kuhusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele kimetoa maombi na maoendekezo tofauti kuhusu mchakato wa kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele.

Kikishirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Brela, WMA, TBS, COSOTA, pamoja na BASATA sehemu ya maoni yaliyolewa ni mamlaka hizo kushirikiana na Serikali za mtaa katika kufanikisha wanadhibiti uchafuzi huo kuanzia ngazi ya chini.

Wakitoa maoni yao katika kikao hicho kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam haya ndio sehemu ya maoni:

Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Elizabeth Mshote amesema “Afya ni suala la msingi pia bila mafao hata Afya inaweza ikaathirika, tunatakiwa kuangalia vitu hivyo kwa kupitia Kanuni tulizonazo.

“Nashauri taasisi na mamlaka ziwatumie watu wa Serikali za Mtaa kwa kuwa ndio ambazo zinakutana na watu wa mtaani kila siku, Taasisi za Serikali zinaweza kukosa watu wa kutosha kufika katika kila mtaa lakini wakitumika viongozi hao wanaweza kuwa na msaada.”

Akichangia mada, SSP Almachius anasema mamlaka zimekuwa zikishughulika mara nyingi na watu ambao wana leseni lakini wapo ambao hawana leseni na hao wamekuwa wakisababisha uchafuzi wa mazingira ya kelele kwa asilia kubwa.

Ameshauri kila mmoja kutimiza wajibu wake kuanzia ngazi ya chini, pia utoaji wa leseni wa kumbi za burudani zinatakiwa kufuatiliwa na mamlaka kwa kuwa kumekuwa na kawaia ya kutoa lakini hakuna ufuatiliaji.

Ameongeza kuwa wanaopewa leseni wanatakiwa kuhakikisha wanatimiza masharti ya kile walichokiomba.

Naye, Dkt. Honest Anicetus ambaye ni Mkuu wa Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira (Wizara ya Afya) amesema “Hakuna sekta yenye mtazamo hasi kwa watu wake lakini pia hakuna uhuru usiokuwa na mipaka ndio maana kunakuwa na sheria ili wote tuwe katika boti moja.”

Upande wa Michael Mwalukaza kutoka PTP (Wizara ya Ardhi) amesema “Suala la kutoa elimu linatakiwa kuendelezwa kwa nguvu zote pamoja na jinsi ya kuzitumia mamlaka husika ili kudhibiti kelele.”
 
Back
Top Bottom