Mo Energy na uchafuzi wa mazingira

heartbeats

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
5,762
8,715
Wakuu,

Hakuna kitu nakerereka kama kutembea kila mita kumi nakutana na chupa ya Mo energy imezagaa hakuna dalili kwamba itaenda popote.

Kwanini nisione chupa ingine kama ya maji ya azam au hill au kilimanjaro, hata ikionekana kwa bahati mbaya basi ukirudi hutoikuta hii ndo inatakiwa.

Sasa Mo na Mo energy zake sijui anatuonaje sisi wananchi na mamlaka zinazosimamia mazingira.

Hili likinywaji linatumika sana kila uchwao kama madawa ya kulevya, kwaiyo uchafuzi wa mazingira kupitia haya machupa yake utazidi kwa kiwango cha kutisha.

Kwanini asitengeneze chupa zinazofaa kuwa Recyclable? Kwanini ziwepo ktk chupa nyeusi kama amefungasha madawa.

Haya machupa ukiacha athari ya kuchafua mazingira pia zinatumika katika kubebea mihadarati kama kete za bangi, pombe kwa kwa muda usioruhusiwa unakuta dereva au mwanafunzi anachupa ya Mo kumbe ndani ameload kisungura au kvant au bia.

EMBU MO FANYA UTARATIBU WA KUBADILI CHUPA ZAKO ZIWEZE KUOKOTWA NA HAWA WAOKOTA MACHUPA ILI KUSAVE MAZINGIRA, KAMA UWEZI BASI AJIRI VIJANA WAWE WANAZIOKOTA HUKU MITAANI.

Hii ni aibu kwa wasomi na watu wanaosimamia mazingira wanawezaje kuruhusu huu upuuzi aibu tunaona sisi tunaoona ichi kitu hakipo sawa.

Nimemaliza
 
Amelipa kodi.
Siku zote tumia changamoto kama fursa, Kazi kwako kuzitumia chupa za Mo Energy kama fursa.
Lkn kumbuka Energy zipo za Azam, Jambo, Mo nk nk
 
Mkuu.

Mo dewji alisharijibu hili swali. Mo ana kampuni ya re-cycle ambayo ipo Mbagala, hiyo kampuni ndio ipo na kazi ya kukusanya hizo chupa.

Mimi nishafanya kazi back in days as sales man.kuna kitu kinaitwa mabando.

Wanachukuliwa vijana zile chupa ambazo zipo reject zinatolewa katika mikanda Halafu zinafunguliwa zinabaki tupu.

Zikibaki tupu zinapelekwa nyuma ya kiwanda zinakandamizwa na mashine Halafu vijana wanazipakia kwenye magari.

Unakuta bando moja linaweza kuwa na almost 80+ kg vijana wanapakia magari yale makubwa hata mawili au matatu, Hakika ni kazi ngumu.

Yakitoka hapo yanapelekwa kuwa re-cycled.

Kinachofanya wasionekane wanafanya kazi ni usimamizi tu, maana kwa mo pia kuna kitu kinaitwa UPAMI wao wanahusika na kutafuta vibarua, so let’s kama vibarua wanapaswa kulipwa 10k kwa siku wanapokea May be 7k na nyingine inaingia UPAMI.
Hata hivyo mda mwingine panakuwa na uhujumu ndio unachokiona hata mtaani.
 
Back
Top Bottom