Taarifa za mikopo midogo midogo ya kibiashara!

Mie nimeshajenga frames huku bara, hapa nimekwama pesa ya kianzio tu yaani 2m ambayo nitaitumia kwa aina ya biashara. Ninazo dhamana zisizohamishika japo HATI ndio bado sijaipata, sijaanza biashara ila ndio natarajia kuanza.

Wapi nitapata mkopo? Maana nimewaona Access Bank wao wanasema wanatoa mikopo kwa walio na biashara tayari, nimeshindwa nifanyeje nipate kujikwamua kiuchumi.

mkuu huna mtaji unataka ukopeshwe?
unafanya hatari na utafilisika miezi michache tu.
inatakiwa uwe na zako ndio uongezee na za bank na uwe na uzoefu na biashara yako.
ukiwa na mtaji wa m10 unaweza kukopa m3 na ukarejesha bila tatizo!
 
Napingana na wewe kuhusu Accessbank.
1; Kwa mteja mpya anaqualify kupata mkopo wa 100k-25Mil...and maximum maturity is 12months.

2;Kwa mteja anayerudia (repeat client)....upande wa micro loans bado anaqualify up to 25Mil....ila maturity ni up to 24months.

3;Pale kariakoo branch...wanakitengo cha SME...hawa wanatoa mikopo from 30Mil and above!

4;Interest ya Accessbank ni 21%,Loan processing duration ni 3days.

NB; Wako active sana kwa mtu asielipa kwa wakati otherwise masharti yao ni nafuu sana.

dhamana inakuwa je hapa?
 
watu wengi wanalalamika riba kubwa,lakini imekuwa kama sheria ya uchumi kuwa interest>inflation, kushusha interest,gvt lazima inflation kwanza
 
Taarifa nyingine ni kwamba TIB wanatoa mikopo mikubwa ya uwekezaji kuanzia USD 150,000. Nitafuatilia kujua masharti yao!
Asante kwa taarifa mkuu, mimi nina biashara yangu ndogo inaendelea ninahitaji mkopo ili kuikuza lakini nina shamba tu halina hati lakin ninaweza kupata mkopo kwa dhamana hii? kama ninaweza ni bank gan watakao weza kunisaidia? Naombeni msaada wenu juu ya hili.
 
Sina hakika kama shamba ambalo halijapimwa na kwa hiyo halina hati linaweza kutumiwa kupata mkopo kutoka benki. Hebu jaribu kutembelea benki yoyote uwaeleze. Naamini watakupa ushauri na kukuelekeza cha kufanya!
 
Mimi nimezunguuka kama benk nne ila kutokana na muundo wa biashara yangu benk zote nimeka mkopo sijaelewa kwa nini awajaweka mikopo ya aina hii.hata kama una unadhamini wauwakika(NYUMBA) labda bwana MZUZU utujuze kwa TIB. Ninaotoa bidhaa na kushusha kwenye godauni au kufikisha kwa madalali.
 
Benaire kuwa mkweli, interest za access Bank, minimum ni 3.75% per month sasa unaposema 21% per annual unadanganya.
 
2. FINCA .....Nimepata taarifa kuwa mtu akikopa 15mil anatakiwa kurudisha 1.7mil kwa mwezi ambayo inatupa interest ya 33.3%

Mwenye taarifa zaidi atuwekee hapa ili tuweza ku-update hii page ili iwasadie wale wanaohitaji mikopo ili wajikwamue!

Babu DC!![/COLOR]

khs FINCA ninavyofaham;
Unaweza kopa kuanzia 500,000 mpaka 15m kwa mkopo wa mtu binafsi(masharti uwe na biashara yenye mzunguko ndani ya mwezi mmoja ili uweze kufanya rejesho la principal na interest) hawahitaji uwe na account na kama documentation itaenda vizuri unaweza pata mkopo ndani ya siku 7. Interest yao ni 3 percent ya loan kwa mwezi. Na term zao zinaanzia mpaka miezi 3 hadi 18, that means depending with the loan term its where the final interest is determine. Kama miezi 6 basi interest ni 18percent. Hawana overdarft coz ndio kwanza wanajipanga waanze huduma ya savings this year. Nawakilisha.

KUHUSU FINCA
kuna mikopo ya aina tatu ya binafsi. small loans inarange from 500k-5m with 5% interest rates, na kuna medium loans (5.1m-10m) with 4% interest rate, kuna large loan, (10.1m-100m) with 3% interest rate.
  • Interest rate inakwenda kwa mfumo wa decreasing rate, yaani inakatwa kwenye principal iliyobaki so inakwenda kwa kushuka interms of amount. So kwa FINCA riba inakuwa affected na mda unaokaa na hiyo hela na kiasi cha hela ulichochukua.
  • mfano mtu anaechukua hela kubwa kwa mda mfupi riba yake mwisho term ya mkopo ni ndogo ukilinganisha na mtu anaechukua hela hiyo hiyo kwa mda mrefu zaidi.
So ukitaka kujua riba mwisho wa term chukua rejesho unalolipa kila mwezi zidisha kwa mda unaokaa na hiyo hela kwa miez. jumla yake toa na kiasi cha mkopo ulichopewa.ile increment ndo riba yenyewe.
 
Mkuu last man ahsante kwa info kuhusu Finca. Vp kuhusu terms zao zingine mfano collateral ni lazima iwe immovable kwa maana ya real estate kama yanavyotaka mabenk mengi au? Na legal status ya mkopeshwaji ina conditions zozote?
 
Vigezo vya kupata mkopo nirahisi tu, uwe mtanzania, uwe na miaka kuanzia kumi na nane, uwe unamiliki biashara ( legal business, na yenye tin na leseni husika ya biashara) na iwe na uzoefu usiopungua miezi sita,
KUHUSU DHAMANA
finca wanakubali kuweka fixed assets(assets za biashara) home chattels, kama mkopo ni mkubwa au hizo fixed assets na home chattels hazitoshi unaweka kuweka, morgage surveyed or unsurveyed, or vehicle, or fixed deposit account.
NOTE
kinachodetermine kiasi cha mkopo unaopewa finca ni ukubwa wa biashara yako, yaan mtaji unaozunguka, uwezo wa biashara yako kulipa rejesho husika la mwezi, na loan security, yaan dhamana zako.
 
Mkuu Last man ahsante kwa maelezo mazuri nadhani nimekuelewa nikiwa na la ziada nitakucheck mkuu!
 
Usijaribu kukopa huko labda uwe na tatizo kubwa na bank uwe haukopesheki.(fanya uchunguzi wa kina kwanza kabla ya kuingia huko FINCA)

Mkuu Sanja tunashukuru sana kwa ushauri wako. Pengine kwa faida pana ya wadau jamvini, unaweza kueleza japo kifupi sababu zilizopelekea hitimisho lako? Tunatanguliza shukrani za dhati!
 
Mkuu Sanja tunashukuru sana kwa ushauri wako. Pengine kwa faida pana ya wadau jamvini, unaweza kueleza japo kifupi sababu zilizopelekea hitimisho lako? Tunatanguliza shukrani za dhati!
Kidogo ninachoweza kueleza nikuwa hiyo riba ya 5% ni kwa mwezi, sasa fikilia unachukua mkopo wa miaka mitatu (miezi36), hii inamana utatoa kiasi cha riba ya (36*5=180%) Mf umekopa 1,000,000/=, utaripa riba ya tsh50,000/= mara miezi36 jumla ya riba tu ni tsh 1800,000/= .Kama nimekosea watalam watanirekebisha. Swali linabaki nibiashara gani yenye kiasi kikubwa hivo. (Kwenye mabenk navoelewa ni riba ya muda wote wa mkopo mfano 22%)
 
Kidogo ninachoweza kueleza nikuwa hiyo riba ya 5% ni kwa mwezi, sasa fikilia unachukua mkopo wa miaka mitatu (miezi36), hii inamana utatoa kiasi cha riba ya (36*5=180%) Mf umekopa 1,000,000/=, utaripa riba ya tsh50,000/= mara miezi36 jumla ya riba tu ni tsh 180,000/= .Kama nimekosea watalam watanirekebisha. Swali linabaki nibiashara gani yenye kiasi kikubwa hivo. (Kwenye mabenk navoelewa ni riba ya muda wote wa mkopo mfano 22%)

Sanja umesema sana c kdg kwani umemaliza kila kitu. Catch hapa iilikuwa kwenye interest rate, jamaa aliposema 5% hakusema ni monthly rate kitu ambacho c fair. Banks zetu zinalaumiwa sana kwa riba kubwa but kwa hili la Finca then banks bado ziko better tena by far. Once again thanks Mkuu Sanja!
 
Mimi nimekuwa na wazo ambalo linaweza kuwasaidia vijana kama wengi tukifanya hivyo. Mfano kama vijana kadhaa wanataka kuanzisha kamradi kao ka ufundi chuma, nanunua mtambo wa weding na vifaa vyake na nawakopesha kisha kila mwezi warudishe kidogo kidogo kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi mitatu na interest ya 8- 12%. Nitakuwa nimewasaidia sana kuliko masharti magumu ya bank. Wengi tukifanya hivyotutakuwa tumewasaidia sana vijana na papo pesa zetu kuweka kwenye mzunguko wa faida.

Nashukuru ndg..sasa kwa sisi tulio mbali (Mtwara mjini)tunaweza kumeet condition zako. Kama inawezekana basi ni PM tufanye kazi.
 
Back
Top Bottom