Wakili anayedaiwa kuyatetea Makampuni yanayokopa na kukwepa kulipa Mabilioni ajitetea

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,455
8,290
1000016255.jpg

Wakili Frank Mwalongo amejitokeza kujitetea mbele ya waandishi wa habari kuhusu tuhuma kadhaa ambazo umma ulielezwa kwamba, kampuni ambazo zimekopa mikopo chechefu, zote zinamtumia mahakamani.

Wakili Frank Mwalongo anakiri ni kweli anawakilisha kampuni sita (6) katika kesi zao dhidi ya EQUITY BANK (T) LTD na EQUITY BANK (K) LTD na DELINA GROUP katika kesi yao dhidi ya KCB BANK (T) na KCB BANK (K)

Frank Mwalongo ankairi ni kweli kwamba anawakilisha kampuni ya BIGBON PETROLEUM CO. LTD katika kesi yao dhidi ya NBC - National Bank of Commerce (Tanzania) lakini walifikia suluhu hivyo hakuna kesi.

Frank Mwalongo amekiri ni kweli anawakilisha kampuni za STATE OIL (T) Ltd, KOM (Kahama Oil Mills Limited), TSN OIL, NAS HAULIERS LTD, ZAS Investment Co. LTD, Continental Reliable Clearing (T) Limited (CRC).

Frank Mwalongo anakiri, kwamba anawakilisha kampuni sita (6) mahakamani katika kesi zao dhidi ya EQUITY BANK (T) LTD na EQUITY BANK (K) LTD na kampuni ya DELINA GROUP katika kesi yao dhidi ya KCB BANK.

Ni ukweli kwamba katika kesi hizo mfanano za mikopo chechefu, ambazo Frank Mwalongo alikuwa wakili wao, kampuni tatu (3) zilipewa ushindi mezani katika Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara.

STATE OIL (T) Ltd walishinda kesi dhidi ya EQUITY BANK (T) LTD; TSN OIL walishinda kesi dhidi ya EQUITY BANK (T) na EQUITY BANK (K) LYD; NAS HAULIERS LTD walishinda kesi yao dhidi ya EQUITY BANK (T) LTD.

TSN Group (mali ya Farouq Baghoza) imekopa TZS 80 bilioni EQUITY BANK kwa kudhaminiwa na letter of credit na baadae kukataa kulipa madeni yake na kisha kukimbilia mahakamani, huko walipewa ushindi.

STATE OIL (T) Ltd (Nilesh Suchak); wamekopa TZS 7 bilioni CRDB, wakakopa TZS 4 bilioni ABC BANK, wakakopa $26 milioni EQUITY BANK na kukataa kulipa. Wakakimbilia mahakamani. Kesi wameshinda

NAS HAULIERS LTD; walikopa na kukataa kulipa kiasi cha $16 milioni za EQUITY BANK. Wakakimbilia mahakamani. Nas Hauliers Ltd wakapewa ushindi mahakamani dhidi ya EQUITY BANK (T) Ltd.

Continental Reliable Clearing (T) Limited (CRC) iko hatarini kufungwa kutokana na shauri lililofunguliwa na EQUITY BANK, Equity Bank (T) LTD na Equity Bank (K) LTD, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Benki hizo zinaidai Continental Reliable Clearing (T) Limited (CRC) zaidi ya $10.5 milioni na TZS 780.6 milioni. Shauri hilo lipo chini ya Jaji Butemo Phillip. CRC wanawakilishwa na Wakili Frank Mwalongo.

Kwa mujibu wa Wakili wa EQUITY BANK LTD, Shalom Samuel Masakyi, anasema CRC imekimbilia mahakamani kuzuia uuzwaji wa dhamana ilizoweka kuchelewesha kulipa madeni ili dhamana hizo zisiuzwe.

ZAS Investment Co. LTD inadaiwa na EQUITY BANK Tanzania LTD TZS 22 bilioni, zikiwa ni mkopo ambao ilijipatia kampuni hiyo kwa ajili ya ujenzi wa hoteli kwa nyakati tofauti kuanzia 2017, pamoja na riba.

Mahakama Kuu kanda ya DSM, ilitupilia maombi ya ZAS Investment Co. LTD kutaka kuhamisha kesi kutoka kwa mheahimiwa Jaji Edwin Kakolaki kwenda kwa Jaji Butamo Phillip. Wakili wa ZAS ni Frank Mwalongo.

Wakili wa kampuni ya ZAS Investment Co. LTD ni Frank Mwalongo anakiri kwamba ni kweli kesi hiyo imesikilizwa hadi mwisho katika Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara,na inasubiri hatua ya hukumu.

Continental Reliable Clearing (T) Limited (CRC); (mali ya Abri family Iringa), wamekopa na kukataa kulipa $2 milioni, STANBIC BANK. Pia EXIM BANK $3 milioni na EQUITY BANK $11 milioni (zaidi ya TZS 30 bilioni)

KAHAMA OIL MILLS LIMITED wamechukua kutoka AZANIA BANK kiasi cha TZS 70 billion , huku wakichukua TZS 110 bilioni kutoka EQUITY BANK na kukataa kulipa zote kisha kukimbilia mahakamani.

Kampuni ya Continental Reliable Clearing (T) Limited (CRC) na KAHAMA OIL MILLS LIMITED hizi kesi zipo katika hatua mbalimbali za usikilizaji katika Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara.

Lakini, EQUITY BANK (T) LTD hakurudhika na hukumu iliyotolewa, kampuni ya NAS HAULIERS LTD (walikopa na kukataa kulipa kiasi cha $16 milioni sawa na zaidi ya TZS 67 bilioni) na kupewa ushindi mahakamani.

EQUITY BANK (T) LTD na EQUITY BANK (K) LTD wamekata rufaa mahakama ya rufaa Tanzania dhidi ya hukumu katika kesi yao na STATE OIL (T) Ltd (mali ya Nilesh Suchak) na TSN Group (mali ya Farouq Baghoza).

Wakili Frank Mwalongo anakiri hadharani kwa kusema kwamba mikopo hiyo katika kampuni hizo inahusu fedha kutoka nje ya nchi. Na kwamba mikopo hiyo imekopwa na kampuni kutoka nchi za Mauritius na UAE (Dubai)

EQUITY BANK (T) LTD na EQUITY BANK (K) LTD walikuwa ni benki mwezeshaji (facilitating bank). Mikopo hiyo kampuni hizo zilitumia kulipa madeni yao na fedha nyingine kama mtaji (working capital).

Kampuni hizo zinatajwa kuwa ni Lamar Commodity Trading DMCC (kutoka Dubai) hawa waliwakopesha STATE OIL (T) Ltd na Barak Fund Management (kutoka Mauritius) hawa waliwakopesha TSN GROUP.

EQUITY BANK (K) LTD wakawalipa hizo kampuni za Dubai na Mauritius, fedha baada ya deni kuishi muda mrefu na benki hiyo ya EQUITY BANK (K) LTD ilikuwa mdhamini katika upatikanaji wa mkopo huo.

TSN GROUP walikopa TZS 80 bilioni EQUITY BANK na STATE OIL (T) Ltd walikopa $26 milioni kupitia EQUITY BANK (sawa na TZS 67 bilioni. Kampuni hizo zimepewa ushindi Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara.

STATE OIL (T) Ltd, TSN Group na NAS HAULIERS LTD wamepewa ushindi Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara Vs EQUITY BANK (T) LTD na EQUITY BANK (K) LTD mikopo hiyo haikudhaminiwa na benki hiyo.

Lakini Wakili Frank Mwalongo anasahau kwamba, mikopo kutoka nje ya nchi kwa matumizi ya shughuli ndani ya Tanzania lazima isajiliwe kwa mujibu wa THE FOREIGN EXCHANGE REGULATIONS, 2022

Wakili Frank Mwalongo anetushangaza wengi kwamba hajui ni kosa kubwa kushindwa kusajili mikopo ya nje? Failure to register foreign loan. THE FOREIGN EXCHANGE ACT (CAP. 271) (Made under section 6 (1))

BoT imepewa jukumu la kufuatilia pamoja na mambo mengine madeni ya nje ya sekta binafsi. Madeni ya nje yanafuatiliwa kwa uangalifu ili kuhakikisha kuwa uchumi una uwezo wa kutimiza majukumu yake ya deni

Kanuni za Fedha za Kigeni 2022 zinatoa sharti la mkopo wowote wa kigeni kwa mkazi wa Tanzania wenye muda unaozidi siku 365 usajiliwe na BoT na kupewa Nambari ya Usajili wa Deni (Debt Registration Number - DRN).

Debt Registration Number (DRN ni msimbo wa kipekee (unique identification code) wa utambulisho uliopewa kutambua mikopo ya nje (external loans) iliyosajiliwa katika kanzidata ya mikopo ya nje katika BOT.

Zaidi ya hayo DRN itakuwa rejeleo la malipo, huduma ya deni na muamala mwingine wowote unaohusiana na mkopo huo (reference for disbursement, debt service and any other transaction related to that loan).

Kama mkopo kwa kampuni ni wa muda wa miaka 3, uko chini ya mikopo ambayo ni lazima isajiliwe na BoT kwa mujibu wa Kanuni. (THE FOREIGN EXCHANGE ACT (CAP. 271) (Made under section 6 (1))

Baada ya kutia saini makubaliano ya mkopo, kampuni inapaswa kuwasilisha nakala iliyoidhinishwa ya makubaliano ya mkopo na hati nyingine husika kwa benki yako ndani ya siku 14 kwa madhumuni ya usajili.

Benki inatakiwa kuwasilisha hati hizo kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ndani ya siku 7 baada ya kuzipokea kutoka kwa kampuni yako kwa ajili ya kutoa Nambari ya Usajili wa Deni (Debt Registration Number - DRN).

Kwa kuwa hujaeleza hatua hizo katika ufafanuzi wako, kwa kuzingatia hayo, kama wateja wako na huenda benki yako tayari mlikiuka Sheria ya Fedha za Kigeni na Kanuni na chini ya kutozwa kwa adhabu na BOT.

Sio wateja (hizo kampuni) tu kama mkopaji, bali sheria inatoa adhabu kwa benki yako kwa kupokea mapato ya mkopo na kushindwa kuwasilisha nyaraka zinazohitajika BoT kwa usajili kwa mujibu wa matakwa ya sheria.

Kanuni zimerekebishwa (THE FOREIGN EXCHANGE (AMENDMENT) REGULATIONS, 2023). Awali, adhabu ya TZS 1M ingetozwa kwa wateja wako (kampuni hizo) kwa kila siku ambayo mkopo unabaki bila kusajiliwa.

Hata hivyo, katika marekebisho ya kanuni ya sasa, (THE FOREIGN EXCHANGE (AMENDMENT) REGULATIONS, 2023) adhabu ni TZS milioni nne (4) au kifungo kisichozidi miaka 14 au vyote kwenda kwa pamoja.

The Foreign Exchange ACT (CAP. 271), The Foreign Exchange Regulations, 2022; Borrowing from abroad, kifungu cha 25 cha kanuni hizo kimetoa ufafanuzi mzuri zaidi kuhusu jambo hilo. Tunaweza kufanya rejea.

Sharti kwamba mkataba wa mkopo usijumuishe masharti ambayo yanamtaka mkopaji kufungua akaunti ya fedha za kigeni nje ya Tanzaniq. Endapo mkataba wa mkopo una masharti hayo, BoT haitasajili mkopo huo.

Kwa mujibu wa mwongozo wa BoT mkataba wa mkopo unapaswa kuwa na: Jina la mkopeshaji na mkopaji; Mawasiliano, anwani ya posta, nambari ya faksi, nambari ya simu na anwani ya mkopeshaji na mkopaji;

Kiasi cha mkopo na sarafu ya manunuzi; Madhumuni ya mkopo (Purpose of the loan); Kiwango cha riba kinachotumika; Kipindi cha ukomavu wa mkopo; Ratiba ya marejesho ya mkopo yenye tarehe zilizoonyeshwa.

Kifungu kinachoonyesha sheria inayotumika Malipo yanayoonyesha kiasi, tarehe ya malipo na sarafu; Malipo ya huduma ya deni yanayoonyesha mtaji na riba iliyolipwa na tarehe za thamani;

Malipo mengine yanayolipwa, ada ya ahadi, ada za usimamizi n.k; Maelezo juu ya uboreshaji wa mkopo au kughairiwa; na Maelezo juu ya urekebishaji au ufadhili wa mkopo (Details on loan restructuring or refinancing)

Wakili Frank Mwalongo anakiri kwamba, EQUITY BANK (K) LTD wanatoa mikopo Tanzania ambayo haijasajiliwa. Na wanaipitisha kiufundi-ufundi na inafanyiwa repayment bila BoT kufahamu. Ni mikopo mingi.

Na wakili Frank Mwalongo anasema mifano ya mikopo hiyo zimepewa kampuni ambazo anazisimamia mahakamani. Mikopo imetolewa bila kufuata utaratibu. Hili ni kosa kwa mujibu wa kanuni za fedha za kigeni.

Hivyo, Wakili Frank Mwalongo, bado hoja zetu nyingi za msingi hujajibu kuhusu hii mikopo chechefu. Unaweza tena kuwaita waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi mzuri kwa kuzingatia hayo ambayo kanuni zimeelekeza.

Katika kupunguza riba ya mikopo inayotolewa na benki za biashara Tanzania, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika uchunguzi wake ilibaini kwamba wafanyakazi wa taasisi hizo wanatoa mikopo kwa kupindisha taratibu.

Taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuhusu mikopo chechefu ambayo ilielezwa na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Florence Luoga, Novemba 2021 ilielez kwamba wakopaji wanafanya udanganyifu.

Kutokana na udanyifu huo, benki hizo za biashara zinalazimika kuweka kuweka tahadhari kwa kutoza riba kubwa. BoT wanafahamu hayo lakini hawachukui hatua. Hili ni TATIZO na lazima lishughulikiwe kwa uzito.

Benki Kuu ya Tanzania ishughulike na wadau wake, hizo benki na kuwajibisha wafanyakazi wa benki hizo na wateja wake wanaokiuka utaratibu uliowekwa na serikali. Kutoa mikopo kwa njia za uhalifu ni kosa.

Benki husika ziwachukulie hatua za kisheria wahusika wote, Benki Kuu ya Tanzania inamfungia kuajiriwa na benki au taasisi yoyote. Hayo yalikuwa maelekezo ya Gavana wa BoT, Florens Luoga, Novemba 2021.

Taasisi za kuchakata taarifa za mikopo (credit reference bureau) zihusike kuchunguza hii mikopo chechefu hususani katika hizo benki za biashara. Mikopo chechefu ni gonjwa linaloisumbua sekta ya fedha.

Taifa lenye uwiano mdogo wa mikopo chechefu, huonekana kuwa sekta imara ya fedha kutokana na usimamizi makini kwa kulinda uchumi wa nchi na fedha za wateja wanaoweka amana zao benki.

Udanganyifu unaofanywa na hawa wakopaji, michezo hiyo inafanywa kwa ushirikiano mkubwa kati ya wafanyabiashara na wafanyakazi wa benki hizo za biashara. Hii ndiyo mikopo hiyo chechefu.

Benki zinakosa mitaji. Kiasi ambacho wangekopeshwa wajasiriamali baada ya mikopo kurejeshwa maelfu ya vijana wangepata mikopo. Benki zinapata faida kwa sababu ya wanahisa lakini hakuna nafuu kwa wakopaji.

Martin Maranja Masese, MMM.

Kufahamu undani wa Sakata hili, soma;
 
View attachment 2973730

Hana kosa, ndio mfumo wa dunia. Na ustaarabu unavyotaka, hata shetani akija Leo duniani, hawezi kufungwa moja kwa moja, lazima apewe wakili wa kumtetea
 
Back
Top Bottom