Taarifa ya rasmi ya Shirika la Nyumba (NHC) kuhusu utekelezaji wa Sera ya Ubia wa Uwekezaji

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetoa ufafanuzi kuhusu taarifa za wapangaji wa majengo ya nyumba za shirika hilo waliopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam kutoa malalamiko kuwa wanahamishwa pasipokuwa na mazungomzo yoyote baina ya oande zote mbili.

Hii hapa taarifa kamili kutoka NHC…

=============

Dar es Salaam Tarehe: 14 Juni, 12023

Shirika la Nyumba la Taifa lilianza utekelezaji wa sera ya ubia ya kuendeleza majengo yake machakavu yaliyopo katikati ya miji nchini tangu mwaka 1993. Uendelezaji huo una lengo la kuboresha madhari ya miji, kuongeza mapato ya Shirika na kuongeza maeneo kwa ajili ya makazi na shughuli za biashara.

Sera hiyo iliboreshwa katika nyakati tofauti na mwaka 2022 maboresho makubwa yalifanyika katika sera hiyo na kuzinduliwa Novemba 16 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa.

Baada ya uzinduzi wa Sera hiyo iliyoboreshwa mwaka 2022, Shirika lilitangaza orodha ya viwanja 87 vilivyopo katika mikoa 18 kwa ajili ya uwekezaji ambapo viwanja 17 sawa na asilimia 20 Vipo katika eneo la Kariakoo.

Baada ya kutangaza maeneo hayo, Shirika lilipokea jumla ya maombi 59 kwa ajili ya kuendefeza viwanja 28 vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini. Ili kuwa na uhakika wa uwezo na uadilifu wa waombaji hao, Shirika lilifanya uchambuzi wa maombi yaliyowasilishwa na maombi 24 yaliyokidhi vigezo yaliidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi kwa hatua zaidi.

Bodi ilielekeza ufanyike upekuzi wa kina (due deligence) ili kujiridhisha juu ya uwezo wa wawekezaji, sifa za kampuni husika na taarifa zingine za ziada ili kuepuka makosa yaliyojitokeza katika miradi ya awali ya ubia. Upekuzi huo umekamilika na kwa sasa wawekezaji wanakamilisha kuandaa michoro pamoja na kupitia rasimu ya mikataba ya ubia ili baadaye Shirika liiwasilishe mikataba hiyo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uhakiki na kuidhinishwa.

Pamoja na hatua zote za uwazi zilizochukuliwa na Shirika kumekuwa na taarifa za upotoshaji kwamba miradi hiyo ya ubia imepewa mtu mmoja kuiendeleza, jambo ambalo siyo kweli kwa kuwa walioomba ni makampuni ya Tanzania yaliyokidhi vigezo vya Sera ya Ubia na siyo mtu binafsi.

Ili kupisha uendetezaji unaokusudiwa, Shirika Ijmezungumza na kuwapa elimu wapangaji wake ambao pia wamepewa notisi ya siku 90 kwa mujibu wa mikataba ya upangaji. Ni vizuri ifahamike kwamba kwa mujibu wa Sheria ilitakiwa wapewe notisi ya siku 30 tu ili kupisha uendelezaji.

Pamoja na kutoa muda wa ziada wa siku 60 yapo maombi ya baadhi ya wapangaji ya kuongezewa muda ambayo yanatizamwa na Shirika na yatatolewa uamuzi.

Aidha, tunatoa tahadhari kwa wapangaji hao wasikubali kuchangishwa fedha na wanaojiita wabia katika majengo yatakayondelezwa kwa ahadi ya kupewa upangaji baada ya ujenzi kukamilika. Hadi sasa hakuna mbia atiyesaini mkataba na Shirika na kwamba Shirika litachukua hatua kwa mtu au kampuni itakayobainika kufanya vitendo hivyo.

Utekelezaji wa Sera ya ubia na sekta binafsi ambayo ni injini ya maendeleo ni mweEekeo thabiti wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na unapaswa kuungwa mkono ili kuharakisha maendeleo, kukuza uchumi na kuongeza mapato ya nchi yetu.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA



UTEKELEZAJI SERA YA UBIA_page-0001.jpg

Pia soma: Wapangaji nyumba za NHC Kariakoo walalamika notisi za kuhama bila mazungumzo, wadai NHC wamempa dili mwekezaji mpya kimyakimya
 
Ingawa hakukuwa na haja ya kutoa ufafanuzi kwa sababu hii sera ilizinduliwa na kutangazwa mbele ya vyombo vya habari mchana kweupe kabisa still wamefanya vizuri kutoa ufafanuzi

Hawa wapotoshaji dawa yao ni kuwagonga facts tu maana wanasumbuliwa sana na chuki na misongo ya mawazo
 
Back
Top Bottom