Taarifa ya Msimamo wa CDM Juu ya Uteuzi wa Tume ya Mchakato wa Katiba Mpya

tuweni fair Zanzibar wametoka wakristo wangapi? Si kulalamika tu kuonewa
Hicho ndio anachotaka mwenzenu kama hamjamjua huyo gamba mwelevu, keshajua religious arguments are bound to create a reaction and sway you towards nonsense arguments.

Hila ukweli wenyewe hii timu itatimiza matakwa ya katiba mpya maana the real problem ni mtu aliewachagua na namna ya walivyopendekezwa. Binafsi nimeanza kuchoka na hili suala la katiba.

Binafsi nina ndoto za kukamata millioni one day niwe na kiburi, lakini kabla ya kufika huko realistically nafikiria njia ya kunifikisha hapo. Hawa Chadema siwaelewi kabisa badala ya kupigana vita vyao kwanza jinsi katiba inavyowaumiza wao kwa sasa kwenye chaguzi, mahakama na democracy rights in general. Yaani wao wamekazana kuvamia nchi na silaha za kushinda vita ya mkoa it makes me wonder if their constitution problems are related to their struggles at the moment or they just want to politicize the issue.

Lets face it watanzania wanaotandikwa na kufukuzwa kila siku bila ya kujua haki zao zilizo wazi hawana huwezo wa kutunga katiba inayofaa kuongoza kwa sasa. sijui kwanini walio waelevu wasielekeze nguvu za haraka hakara kuakikisha kwanza wanapata katiba yenye usawa hili vita vyao viwe na nguvu kwa sasa na mengine baadae.
 
Kwanini aisee? kweli nimesikitika sana JK kuchagua viongozi wakuu wa tume wakristo (chair na makamu) wake..hii katiba lazima itakuwa na elements za kikanisa ...bado sijarizika au unaona sawa

Kwanini katika watu 15 wa Tanganyika 4 tu ndio wawe waislam (very unfair representation of muslims in tanganyika)

Funguka arif ukisema M/kiti na makamu wake ni Wakristo nitakukumbusha Rais wetu mwislam na makamu wake Mwislam pia.
 
Mimi ninacho kiona hapa jamaa anataka kurudia kale kamchezo kalichoshindwa kufikia malengo (White Paper) ya Jaji Sinde Warioba nakamteua tena ili kuhalalisha hilo ila ambacho nasikitika kachagua Wazee wenye umri mkubwa ilihali nchi yetu barabara za vijijini haziendeki kirahisi watakuwa wanachoka sana kusafiri badala ya kufanya kazi,. Pia kumkosa Isa Shivji ni pengo na kosa lisilo fichika. Tunachotafuta ni maoni ya katiba mpya na sio ushauri wa katiba mpya.
 
Kwanini aisee? kweli nimesikitika sana JK kuchagua viongozi wakuu wa tume wakristo (chair na makamu) wake..hii katiba lazima itakuwa na elements za kikanisa ...bado sijarizika au unaona sawa

Kwanini katika watu 15 wa Tanganyika 4 tu ndio wawe waislam (very unfair representation of muslims in tanganyika)

Funguka arif ukisema M/kiti na makamu wake ni Wakristo nitakukumbusha Rais wetu mwislam na makamu wake Mwislam pia.
 
Hivi mnataka kuniambia hao waliochagua wa dini kweli? wenye dini zao huku duniani wamebaki wachache sana. Sivyo ufisadi na wizi usingekuwapo.Mimi Mkristu lakini naamini mafisadi wa ccm hawana dini kuanzia na mwenyekiti wao.Wanaonekana tu makanisani na misikitini tu lakini imani ya Mwenyezi Mungu Subhanna hawana.
 
Kamati nzuri, lakini chadema tunawaomba mwambieni kikwete kuwa ISSA SHIVJI PROF ni muhimu sana kuwepo katika kamati hii. Watanzania tunamhitaji mno.
 
Mimi sijarizika na wajumbe wa upande wa Tanganyika kati ya wajumbe 15; wanne tu ndio waislam kwanini? ina maana Tanganyika inawakilishwa na wakristo tu?
Nadhani watanzania ni lazima tuwe watu wenye fikra pevu,swala la dini tukilishabikia sana ni ujinga mtupu,kwanza dini mnazoshishabikia zote ni ngeni mlipata kama mapokeo mliaacha dini zenu za asili mkakimbilia ustarabu wa ulaya na uarabuni.sasa kwa kufanya hivyo mnataka kupoteza umoja wenu kama ndgu kwa misingi ya dini.nawashauri tulizeni akili zenu tuchambue vitu vya msingi ,tuone kikwete atwambie ametumia vigezo gani kuwateua walioteuliwa.kama amewataea hao kwa misingi ya dini hapo tujenge hoja ya kuikataa tume hiyo.kikubwa tuwapime hao jamaa na histori za uongozi wao huko nyuma kama kweli ni wazalendo je wanauwezo kuwafanyia kazi watanzania kama yalivyomatarajio yao juu ya kupata katiba bora .Labda swali langu kuna uwiano gani watu 15 kutoka visiwani wanawakilisha kiasi gani. na kutoka bara 15 wanawakilisha watu zaidi ya million 40 .je tume hii itakusanya maoni ya kuunda katiba ya muungano ,na tume ya kukusanya maoni ya Tanganyika ni ipi .hizi ndiyo hoja tujiulize tanganyika imemezwa kwenye muungano haipo haitambuliki ,tume hiyo nasema ni ya muungano.tunataka tume ya kukusanya maoni ya watanaganyika.
 
Yaani waislamu ni wa 4 tu kwa bara si haki sijaipenda hii tume
 
Mimi sijarizika na wajumbe wa upande wa Tanganyika kati ya wajumbe 15; wanne tu ndio waislam kwanini? ina maana Tanganyika inawakilishwa na wakristo tu?

Na mimi ni kutoka BAHAI witnes sisi tumeonewa kwote kwotekwote hamna hata mjumbe toka din yetu! Pia mjomba wangi ni Mhindu naye analalamika hivyo hivyo kuwa hakuna mhindu hata mmoja si bara wala unguja! Huu ni uonevu! Na mpwa wangu yeye anaabudu jiwe naye lalamiko ni hilo hilo. Jiran yangu yeye anaabudu ngombe naye tatizo ni hilo hilo! Hata shemeji yangu upande wa baba mdogo aloyeoa mdogo wake na kaka yake shangazi ambaye dini yake ni islam lakin Suni anasema hajaona suni hata Mmoja kaona shia tu kwa hiyo anasema hajaridhika. Usijali sana TOPICAL tupo wengi!
 
Topical lazima una kasoro za kimaoni.
Bahati nzuri aliyeunda tume ni muislam
Hii habari ya kuhesabu wakristo na waislam kwenye kila kitu ni dhambi ya kipuuzi lakini ambayo itatugharimu sana
Mnahesabu idadi ya mawaziri kwa misingi ya udini, wakuu wa mikoa na sasa wajumbe wa tume
Huu ni udini wa hatari sana, unapandikiza mbegu za hovyo sana
Leo raisi na makamu waislamu, umeongezwa nini ambacho hukuwa nacho kabla au wakristo wamepungukiwa nini walichokuwa nacho kabla?
Acheni upuuzi huu wa udini

Jamani kwa nini tunachoka kufikiri? kwa nini udini uchukue nafasi namna hiyo? inanipa mashaka na maendeleo ya nchi yetu kama vijana tunang'ang'ania udini kama hivi! Badala ya kujadili hoja za msingi na zenye kuleta tija badala yake tunajadili eti composition ya time imejaa wakristo...hebu tuepuke akili mtindi ambayo haiwezi kuwaza vitu vya msingi na vyenye kuleta tijan kwa Taifa letu! Nashauri udini tuweke pembeni tuangalie maendeleo ya nchi yetu! Hasa tukizingatia uwezo na maadili ya kazi.
 
TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaendelea kuchambua wasifu wa wajumbe walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba.

CHADEMA kitatoa tamko juu ya uteuzi wa tume husika baada ya uchambuzi kukamilika wa kutafakari iwapo uteuzi husika umezingatia matakwa ya umma na dhamira ya kujenga muafaka wa kitaifa wa kuwa na katiba mpya na bora.

Pamoja na kutaja majina ya wajumbe wa tume, CHADEMA kilitarajia kwamba Rais Jakaya Kikwete angeeleza pia ratiba ya kufanyika kwa marekebisho mengine muhimu ya awamu nyingine kuhusu bunge maalum la katiba na hatua ya kutunga katiba mpya na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki kabla ya mchakato kufikia katika hatua husika.

Katika muktadha huo, Kamati Maalum ya Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoundwa tarehe 20 Novemba 2011 kwa ajili ya kukutana na Rais Jakaya Kikwete kuhusu sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011; itafanya kikao chake karibuni kupitia taarifa ya uchambuzi unaoendelea kufanywa juu ya uteuzi uliofanyika wa wajumbe wa tume na tamko litatolewa kwa umma kuhusu mchakato huu muhimu kwa maslahi ya taifa.

Itakumbukwa kwamba tarehe 27 na 28 Novemba 2011 Rais Kikwete alifanya mkutano wa siku mbili na viongozi wa CHADEMA kuhusu muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba na pande mbili kukubaliana kuhusu haja ya sheria husika kufanyiwa marekebisho kwa mashauriano na wadau mbalimbali kwa lengo la kudumisha muafaka wa kitaifa kwenye mchakato wa katiba mpya.

Kamati Maalum ya CHADEMA ilikutana tena na Rais tarehe 21 Januari 2012 Ikulu Dar es salaam ambapo kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe ilitaarifiwa hatua ambayo ilifikiwa na serikali katika kuanza kuiboresha sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 ili ikidhi mahitaji ya kujenga kuaminiana na muafaka wa kitaifa kwa mawasiliano na mashauriano na wadau mbalimbali.

Tarehe 22 Januari 2012 Kamati Kuu ilipokea na kujadili taarifa ya Kamati Maalum kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 na kujulishwa hatua ambazo serikali ilifikia katika maandalizi ya kuifanyia marekebisho tajwa katika Mkutano wa Sita wa Bunge unaotarajia kuanza tarehe 31 Januari 2012.

Kamati Kuu iliamua kwamba Kamati Maalum iendelee kufanya mawasiliano na mashauriano na Rais Kikwete na Serikali kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 inafanyiwa marekebisho ya msingi kabla ya mchakato wa kukusanya maoni kwa mujibu wa sheria husika haujaanza.

Kamati Maalum ilitakiwa kuendelea kufuatilia utekelezaji wa maazimio matatu ya Kamati Kuu yaliyofikiwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kuhusu mchakato wa katiba mpya; maudhui ya maazimio hayo ni kama ifuatavyo:

Mosi; "kutoa elimu kwa wananchi na wadau wote juu ya ubovu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na juu ya haja ya kuwa na sheria itakayoweka utaratibu bora zaidi wa kuunda Tume Shirikishi ya Katiba kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi, kuandaa ripoti na Rasimu ya Katiba Mpya, Bunge Maalum la Katiba na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki".

Pili; "Ushiriki wa CHADEMA katika mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba utategemea utayari wa Serikali ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko ya kimsingi katika sheria hiyo kwa lengo la kujenga muafaka wa kitaifa juu ya mchakato huo".

Tatu; "viongozi wote wa chama na wa kuchaguliwa katika ngazi zote kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara yenye lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na madhara yake kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya na bora kwa nchi yetu kwa lengo la kuunganisha umma wa watanzania kuweza kufanya mabadiliko ya msingi"

Imetolewa tarehe 07 Aprili 2012 na: John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
Mngesema tu mnasubiri maoni ya wananchi kuhusu uteuzi huu wa tume.

Nadhani mmeshindwa kupinga moja kwa moja uteuzi huu kwasababu labda kuna baadhi ya mambo mlikubaliana kwenye kikao cha ikulu (nadhani taarifa yake bado ni siri), na maybe JK kayafuata baadhi ya mapendekezo yenu,ie what people should be in etc, maybe si mapendekezo yote aliyoyachukua, lakini statement hii haionyeshi msimamo wa chama dhidi ya uteuzi wa JK.

Kuna namna mnasuasua, pengine kulinda credibility ya maamuzi ya kwenda kwenye juis, hopefuly mtasimamia yaliyowapeleka ikulu badala ya kuja na taarifa kama hii isioonyesha lolote wala kuwa na mantiki yoyote!
 
Prof Shivji hatuoni sababu kubwa ya Raisi kumuacha hapo hajaitendea haki nchi hawa ndio hazina ya nchi lazima watumike kwa masilahi ya nchi happa Jk hatutokaa tumuelewe labda afanye vinginevyo.
 
Acheni kufikiria mambo ya kijinga kwani jk ameteua tume ya kushughulikia katiba ya kidini au nchi? Mbona unasema waislamu tu? Tuambie wapagani wamewakilishwa na nani?. Alafu unasema tume ya bara ina waislamu 4 tu kwani tume ziko ngapi?. Mbona hujaeleza katika orodha yote waislamu wangapi? Wakristu wangapi na wasio na dini wangapi?. Acha ujinga tume hii haikusanyi maoni ya kanisa wala msikiti. Kwani kama huna kitu cha maana cha kuandika lazima kuandika?.

Kwani hatakama wajumbe wote wangekuwa waislamu wangewasaidia nini?, rais na makamo wote waislamu imewasaidia nini waislamu? Spika na naibu wakristu je wamewasaidia nini wakristu?. Muhimu ni kuangalia uwezo wa mtu katika kazi sio dini tutajiangamiza kwa ujinga wetu wenyewe.

Kwa taharifa yako mtu anaweza kuwa na jina la kislamu au kikistu lakini asiwe muumini wa dini hiyo.
 
Mimi sijarizika na wajumbe wa upande wa Tanganyika kati ya wajumbe 15; wanne tu ndio waislam kwanini? ina maana Tanganyika inawakilishwa na wakristo tu?

Mbona wajumbe kutoka Zanzibar wote ni Waislam? Inamaana Zanzibar hakuna Wakristo? Au ndo kampeni zenu za udini mnaziendeleza? Binafsi sina imani na kamati yote kwani inamwelekeo wa kidini (Uislam). Kwa tume hii hatuwezi kupata katiba tunayoitarajia.
 
TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaendelea kuchambua wasifu wa wajumbe walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba.

CHADEMA kitatoa tamko juu ya uteuzi wa tume husika baada ya uchambuzi kukamilika wa kutafakari iwapo uteuzi husika umezingatia matakwa ya umma na dhamira ya kujenga muafaka wa kitaifa wa kuwa na katiba mpya na bora.

Pamoja na kutaja majina ya wajumbe wa tume, CHADEMA kilitarajia kwamba Rais Jakaya Kikwete angeeleza pia ratiba ya kufanyika kwa marekebisho mengine muhimu ya awamu nyingine kuhusu bunge maalum la katiba na hatua ya kutunga katiba mpya na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki kabla ya mchakato kufikia katika hatua husika.

Katika muktadha huo, Kamati Maalum ya Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoundwa tarehe 20 Novemba 2011 kwa ajili ya kukutana na Rais Jakaya Kikwete kuhusu sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011; itafanya kikao chake karibuni kupitia taarifa ya uchambuzi unaoendelea kufanywa juu ya uteuzi uliofanyika wa wajumbe wa tume na tamko litatolewa kwa umma kuhusu mchakato huu muhimu kwa maslahi ya taifa.

Itakumbukwa kwamba tarehe 27 na 28 Novemba 2011 Rais Kikwete alifanya mkutano wa siku mbili na viongozi wa CHADEMA kuhusu muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba na pande mbili kukubaliana kuhusu haja ya sheria husika kufanyiwa marekebisho kwa mashauriano na wadau mbalimbali kwa lengo la kudumisha muafaka wa kitaifa kwenye mchakato wa katiba mpya.

Kamati Maalum ya CHADEMA ilikutana tena na Rais tarehe 21 Januari 2012 Ikulu Dar es salaam ambapo kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe ilitaarifiwa hatua ambayo ilifikiwa na serikali katika kuanza kuiboresha sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 ili ikidhi mahitaji ya kujenga kuaminiana na muafaka wa kitaifa kwa mawasiliano na mashauriano na wadau mbalimbali.

Tarehe 22 Januari 2012 Kamati Kuu ilipokea na kujadili taarifa ya Kamati Maalum kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 na kujulishwa hatua ambazo serikali ilifikia katika maandalizi ya kuifanyia marekebisho tajwa katika Mkutano wa Sita wa Bunge unaotarajia kuanza tarehe 31 Januari 2012.

Kamati Kuu iliamua kwamba Kamati Maalum iendelee kufanya mawasiliano na mashauriano na Rais Kikwete na Serikali kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 inafanyiwa marekebisho ya msingi kabla ya mchakato wa kukusanya maoni kwa mujibu wa sheria husika haujaanza.

Kamati Maalum ilitakiwa kuendelea kufuatilia utekelezaji wa maazimio matatu ya Kamati Kuu yaliyofikiwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kuhusu mchakato wa katiba mpya; maudhui ya maazimio hayo ni kama ifuatavyo:

Mosi; “kutoa elimu kwa wananchi na wadau wote juu ya ubovu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na juu ya haja ya kuwa na sheria itakayoweka utaratibu bora zaidi wa kuunda Tume Shirikishi ya Katiba kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi, kuandaa ripoti na Rasimu ya Katiba Mpya, Bunge Maalum la Katiba na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki”.

Pili; “Ushiriki wa CHADEMA katika mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba utategemea utayari wa Serikali ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko ya kimsingi katika sheria hiyo kwa lengo la kujenga muafaka wa kitaifa juu ya mchakato huo”.

Tatu; “viongozi wote wa chama na wa kuchaguliwa katika ngazi zote kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara yenye lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na madhara yake kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya na bora kwa nchi yetu kwa lengo la kuunganisha umma wa watanzania kuweza kufanya mabadiliko ya msingi”

Imetolewa tarehe 07 Aprili 2012 na: John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
Ipingen hii TUME mpate kwenda kukalia tena sofa za ikulu na kunywa chai na mafisad huku mkipongezana!!!
 
Ivi jk alikosa vijana wa kuwaingiza kwenye iyo kamati?
Na wasiwasi na hao wazee kama watayatilia maanani mapendekezo ya vijana.
Tume wazee watupu,alafu wote wana mambo ya kikoloni.
 
Dawa ya hawa watu ni sisi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kupiga kura na siku ya kura kujitokeza kwa wingi ili kuwang'oa madarakani wasiendelee kutufanyinga mafyongo.
 
Yaani waislamu ni wa 4 tu kwa bara si haki sijaipenda hii tume
Wewe nawe ukilaza unakusumbua plus Udini,je kwann haujajiuliza ni kwann huku bara wakristo wamekua 11 na Zanzibar wamekua 15? then ujiulize inakuwaje Zanzibar iwe na Wajumbe 15 while wao ni wachache sana kulinganisha huku Bara tuliopo kama 40 plus? think again na hii tume kwangu naona imekaa vibaya,yuko wapi Mtaalamu wa Katiba Prof Shivj? haya ndio ya kutizamwa zaidi
 
Mngesema tu mnasubiri maoni ya wananchi kuhusu uteuzi huu wa tume.

Nadhani mmeshindwa kupinga moja kwa moja uteuzi huu kwasababu labda kuna baadhi ya mambo mlikubaliana kwenye kikao cha ikulu (nadhani taarifa yake bado ni siri), na maybe JK kayafuata baadhi ya mapendekezo yenu,ie what people should be in etc, maybe si mapendekezo yote aliyoyachukua, lakini statement hii haionyeshi msimamo wa chama dhidi ya uteuzi wa JK.

Kuna namna mnasuasua, pengine kulinda credibility ya maamuzi ya kwenda kwenye juis, hopefuly mtasimamia yaliyowapeleka ikulu badala ya kuja na taarifa kama hii isioonyesha lolote wala kuwa na mantiki yoyote!

Mkuu Jmushi, isome vyema. Isome kwa makini. Utaweza kuelewa. Asante.
 
Back
Top Bottom