Taarifa kwa Vyombo vya Habari: Hoja ya Kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu

Ila sio siri siku hizi namkubali sana zitto kwani kijana anajipambanua kwa kazi yake.
Bigup kaka zittoi na Mungu wa israel akubariki kama jinsi alivyombariki yakobo.
Long live zitto. Amen!
 
Chanzo: H@ki Ngowi
HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012

• Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini
• Ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’


Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 yawabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka “Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba” na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka “hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge
isipokuwa tu kama;

(a) “taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;”

Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa “hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katib mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri”.

Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge kesho tarehe 23/04/2012 tutawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali Bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda Mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.

Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo Bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na maazimio ya Bunge
yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’ hivyo tunaomba wabunge wazalendo na watanzania wote waiunge mkono ili kuimarisha Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ubadhirifu na kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi.

Kwa niaba ya wabunge wazalendo waliotia saini kuunga mkono taarifa ya
hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni;


…………………………….
Kabwe Zuber Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
22/04/2012.
Da kazi kweli kweli....mbona wapinzani watupu ...? CCM 2 tu ? haina haja kupeleka hoja hii, hapa inaonekana Zito kuna ajenda ya siri labda anataka kupanda chati agombee Urais kumpiku Slaa 2015, pia inawezekana kuna maslahai binafsi ya baadhi ya kamati hizi bunge..nimemsikia Nundu akieleza kwa nini haoni sababu ya kujiuzulu..kumbe kuna watu wana shinikiza KAMPUNUI MOJA TU YA CHINA CIVIL AND CONSTRUCTION LTD bila ya kufata taratibu za Zabuni,
yeye anataka zabuni iitwe na zishindane ili kampuni iliyo bora zaidi ifanye kazi..hizi ndio taratibu, sasa maslahi ya watu binafsi wanaenda wanatoa ripoti za kubuni kwa kina zito na wao bila ya tafiti au kwa maslahi watayopata wanamgeuzia kibao waziri Nundu.
ndio maana CCM 2 tu wamesaini motion hii, Namfahamu NUndu ni mtu msafi sana...kuliko zito..as inaoneka zito kupewa ukuu wa kamati hii ya bunge basi kuna maslahi anayaweka..rejea sakata la CHC NA MKULO ..hali ni hio hio....maslahi tu
wasijifanye wanatetea maslahi ya nchii hii.wote ni maslahi tu.
chunguzeni , someni itafute ripoti ya CAG UJUE UKWELI KUPOTOSHA KWA MASLAHI BINAFSI HAISAIDII KITU
 
You Know Zitto cant be written off, he
goes low and the next thing you know
he is on another level again, Boy you are
good! Just keep the good works, although
you can 10 good deeds but just one wrong
turn most of your supporters go cold on
you, yeah its politics! Just keep going on
good deeds.
 
Sisi tumefurahi sana kuona jambo ambalo halijawahi tokea tangu tupate uhuru!!. Wengi walijua eti Waziri mkuu ni untouchable kumbe anakuwa raia tu anapokuwa implicated. Kumbe tukifuata sheria tutaheshimiana kama ambavyo sasa waziri mkuu anajiona mdoogo mbele ya wabunge ambao hata hawana walinzi na vimulimuli kama yeye.
 
Mhe: Zitto endeleeni kuwapiga presha ndani na huku nje/mitaani sisi tutafanya sehemu yetu.

Ingawa nadhani impact ya hili la kutokuwa na imani ni short-term strategy lakini the long one is to go for jugular and take the head off and his party wholly down.

Ila sijafurhishwa na mchango (kwa asilimia) wa wabunge wa vyama vingine. Lakini maadam idadi inayotakikana imepatikana let's start there. The struggle will get tougher to get the 179 votes to vote the govt out.
 
Lol, wana CCM tunajuana tu...tumejaa shaka shaka tumekaa kama hatuamini amini vile. I hope ni mzima lakini AD


Ndahani... No...lol. I am interested sana kwa sababu nje kabisa ya hio.. Believe me, Sio mwana CCM na I am not one wa kukataa entity yangu yoyote ile. Itanipa majibu mengi nikijua idadi. Hasa ni kwa namna gani siasa imekomaa nchini ama ipo bado kiasi gani kuwiva.
 
You Know Zitto cant be written off, he
goes low and the next thing you know
he is on another level again, Boy you are
good! Just keep the good works, although
you can 10 good deeds but just one wrong
turn most of your supporters go cold on
you, yeah its politics! Just keep going on
good deeds.


Goldman I support you, that is why I always beleive Zitto could fair better if he was striving for presidential candidate in CDM. I see him strategic, an Intelligent Manipulator, a salient rough player and Leadership qualities.
 
Wapi current siginatory list? Wabunge 73, kinanani?

Ni hawa hapa:
Majina ya wabunge waliotia saini hoja ya mh.zitto kabwe




  1. Mhe. Rashid Ali Abdallah – CUF
  2. Mhe . Chiku Aflah Abwao- CHADEMA
  3. Mhe . Saluim Ali Mbarouk – CUF
  4. Mhe . salum Khalfam Barwany – CUF
  5. Mhe . Deo Haule Filikuchombe - CCM
  6. Mhe.Pauline Philipo Gekul - CHADEMA
  7. Mhe. Asaa Othman Hamad - CUF
  8. Mhe. Prof.Kuliyokela Kahigi- CHADEMA
  9. Mhe.Naomi Mwakyoma Kaihula – CHADEMA
  10. Mhe . Sylvester Kasulumbayi - CHADEMA
  11. Mhe. Raya Ibrahim Khamis - CHADEMA
  12. Mhe. Mkiwa Hamad Kiwanga - CUF
  13. Mhe. Susan Limbweni Kiwanga - CHADEMA
  14. Mhe. Grace Sindato Kiwelu – CHADEMA
  15. Mhe. Kombo Khamis Kombo – CUF
  16. Mhe. Joshua Samwel Nassari – CHADEMA
  17. Mhe. Tundu Antiphas Lissu - chadema
  18. Mhe Aphaxar Kangi Lugola - CCM
  19. Mhe susan Anselim Lymo - CHADEMA
  20. Mhe. Moses Machali – NCCR Mageuzi
  21. Mhe. John Shibuda Magalle – CHADEMA
  22. Mhe. Faki Haji Makame - CUF
  23. Mhe . Esther Nicholas Matiko - CHADEMA
  24. Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi - CHADEMA
  25. Mhe. Freman Aikaeli Mbowe - CHADEMA
  26. Mhe. Kurudhum Jumanne Mchuchuli – CHADEMA
  27. Mhe. Halima James Mdee - CHADEMA
  28. John John Mnyika - CHADEMA
  29. Mhe. Augustino Lyatonga Mrema - TLP
  30. Mhe . Maryam Salum Msabaha - CHADEMA
  31. Mhe. Peter Msingwa - CHADEMA
  32. Mhe. Christowaja Gerson Mtinda - CHADEMA
  33. Mhe. Philipa Geofrey Mturano - CHADEMA
  34. Mhe. Christina Lissu Mughwai - CHADEMA
  35. Mhe. Joyce John Mukya – CHADEMA
  36. Mhe. Mchungaji Israel Yohane Natse – CHADEMA
  37. Mhe. Philemon Ndesamburo- CHADEMA
  38. Mhe. Ahmed Juma Ngwali - CUF
  39. Mhe. Vincent Josephat Nyerere - CHADEMA
  40. Mhe. Rashid Ali Omar - CUF
  41. Meshack Jeremiah Opulukwa - CHADEMA
  42. Mhe. Lucy Philemon Owenya - CHADEMA
  43. Mhe. Rachel Mashishanga - CHADEMA
  44. Mhe. Mhonga Said Ruhwanya – CHADEMA
  45. Mhe. Conchesta Rwamlaza – CHADEMA
  46. Mhe. Moza Abedi Saidy - CUF
  47. Mhe. Joseph Roman Selasini – CHADEMA
  48. Mhe. David Ernest Silinde - CHADEMA
  49. Mhe Rose Kamili Sukum - CHADEMA
  50. Mhe. Cecilia Daniel Paresso - CHADEMA
  51. Mhe. Kabwe Zuberi Zitto - CHADEMA
  52. Mhe. Magdalena Sakaya – CUF
  53. Mhe Rebecca Mngodo - CUF
  54. Mhe. Sabreena Sungura - CHADEMA
  55. Mhe. Hamad Rashid Mohammed- CUF
  56. Mhe. Rukia Kassim Ahmed (CUF)
  57. Mhe. Mustapha Boay Akoonay (CHADEMA)
  58. Mhe. Abdalla Haji Ali (CUF)
  59. Mhe. Khatibu Said Ali (CUF)
  60. Mhe. Hamad Ali Hamad (CUF)
  61. Mhe. Riziki Omar Juma (CUF)
  62. Mhe Haji Khatibu Kai (CUF)
  63. Mhe. Anna Marystella John Malack - CHADEMA
  64. Mhe. Hamad Rashid Mohamed (CUF)
  65. Mhe. Rajab Mbarouk Mohamed (CUF)
  66. Mhe. Thuwayba Idrissa Muhamed (CUF)
  67. Mhe. Masoud Abdallah Salum (CUF)
  68. Mhe. Muhamad Ibrahim Sanya (CUF)
  69. Mhe. Ali Khamis Seif (CUF)
  70. Mhe. Haroub Muhammed Shamis (CUF)
  71. Mhe. Amina Amour Nassoro (CUF)
 
Tuseme Bunge litatakiwa kuitisha "Kikao cha Dharura" mara baada ya siku 14 kwisha yaani tr 05/05/2012 au litasubiri Kikao cha Bajeti mwezi Juni?
 
huyu jamaa naye anatakiwa siku ya kiama cha magamba nae awambwe msalabani asulubiwe pamoja na dingi yao jk, I HATE CCM na most of its people except very very few i.e Filikunjombe
 
....Hehehehe hayawi hayawi sasa yamekuwa....Sijui kwa nini Pinda haachii ngazi kabla ya aibu kumkuta.
 
Ingependeza sana kama ingetolewa list ya hao wabunge... So curious wana CCM ni wangapi.

2. Rashid Ali Abdallah – CUF
3. Chiku Aflah Abwao- Chadema
4. Saluim Ali Mbarouk – CUF
5. Salum Khalfam Barwany – CUF
6. Deo Haule Filikuchombe- CCM
7. Pauline Philipo Gekul- Chadema
8. Asaa Othman Hamad- CUF
9. Prof.Kuliyokela Kahigi- Chadema
10. Naomi Mwakyoma Kaihula – Chadema
11. Sylvester Kasulumbayi- Chadema
12. Raya Ibrahim Khamis – Chadema
13. Mkiwa Hamad Kiwanga – CUF
14. Susan Limbweni Kiwanga- Chadema
15. Grace Sindato Kiwelu –Chadema
16. Kombo Khamis Kombo – cuf
17. Joshua Samwel Nassari – Chadema
18. Tundu Antiphas Lissu- Chadema
19. Aphaxar Kangi Lugola- CCM
20. Susan Anselim Lymo- Chadema
21. Moses Machali – NCCR Mageuzi
22. John Shibuda Magalle – Chadema
23. Faki Haji Makame- CUF
24. Esther Nicholas Matiko- Chadema
25. Joseph Osmund Mbilinyi- Chadema
26. Freman Aikaeli Mbowe- Chadema
27. Kurudhum Jumanne Mchuchuli – Chadema
28. Halima James Mdee-Chadema
29. John John Mnyika- Chadema
30. Augustino Lyatonga Mrema- TLP
31. Maryam Salum Msabaha- Chadema
32. Peter Msingwa-chadema
33. Christowaja Gerson Mtinda- Chadema
34. Philipa Geofrey Mturano- Chadema
35. Christina Lissu Mughwai- Chadema
36. Joyce John Mukya – Chadema
37. Mchungaji Israel Yohane Natse – Chadema
38. Philemon Ndesamburo- Chadema
39. Ahmed Juma Ngwali- CUF
40. Vincent Josephat Nyerere- Chadema
41. Rashid Ali Omar- CUF
42. Meshack Jeremiah Opulukwa- Chadema
43. Lucy Philemon Owenya- Chadema
44. Rachel Mashishanga- Chadema
45. Mhonga Said Ruhwanya – Chadema
46. Conchesta Rwamlaza – Chadema
47. Moza Abedi Saidy- CUF
48. Joseph Roman Selasini – Chadema
49. David Ernest Silinde- Chadema
50. Rose Kamili Sukum – Chadema
51. Cecilia Daniel Paresso- chadema
52. Kabwe Zuberi Zitto- Kigoma Kaskazini
53. Magdalena Sakaya – CUF
54. Rebecca Mngodo- CUF
55. Sabreena Sungura -Chadema
56. Hamad Rashid Mohammed- CUF
57. Rukia Kassim Ahmed- CUF
58. Mustapha Boay Akoonay -Chadema
59. Abdalla Haji Ali -CUF
60. Khatibu Said Ali -CUF
61. Hamad Ali Hamad -CUF
62. Riziki Omar Juma -CUF
63. Haji Khatibu Kai -CUF
64. Anna Marystella John Malack -Chadema
65. Hamad Rashid Mohamed -CUF
66. Rajab Mbarouk Mohamed -CUF
67. Thuwayba Idrissa Muhamed -CUF
68. Masoud Abdallah Salum -CUF
69. Muhamad Ibrahim Sanya -CUF
70. Ali Khamis Seif -CUF
71. Haroub Muhammed Shamis -CUF
72. Amina Amour Nassoro -CUF

Majina yamefika 74 na namba 74 ni mhesimiwa nimrod mkono..
Nita edit vyema baadae kidogo AshaDii
OTIS
 
Last edited by a moderator:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012


· Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini

· Ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’

Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 ya wabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka “Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba” na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka “hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge isipokuwa tu kama;

(a) “taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;”

Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa “hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri”.

Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge kesho tarehe 23/04/2012 tutawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali Bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda Mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.

Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo Bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na maazimio ya Bunge yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’ hivyo tunaomba wabunge wazalendo na watanzania wote waiunge mkono ili kuimarisha Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ubadhirifu na kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi.

Kwa niaba ya wabunge wazalendo waliotia saini kuunga mkono taarifa ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni;
…………………………….
Kabwe Zuber Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
22/04/2012.

.....Tatizo ni kua wa-Tanzania wengi sasa tumekua washabiki tu wa haya mambo yanayoendelea Bungeni.tumekua tunaishi katika mazingira ambayo kila mtu anongea lakini hakuna msikilizaji na wote tunalilia ukweli tusio ufahamu,hoja ya kutokua na imani na Waziri mkuu naona haitosaidia chochote katika maendeleo na mustakbali wa nchi yetu,na hata hao mawaziri wakijiuzulu haitosaidia chochote,kwani ni mara ngapi tumeshuhudia awamu zilizopita mawaziri kujiuzulu na wengine hata kufukuzwa,na still hakuna kilichobadilika,tatizo kubwa la msingi ni kua kila kiongozi au hata waziri anapochaguliwa kuongoza Wizara fulani akifika tu anaanza kurithi matatizo ya pale pahala kabla ya hio kazi aliotumwa.Mfano mzuri ni wa huyu Waziri Mkuu wetu Mh Pinda,jamani hebu tukumbukeni nini kilitokea mpaka yeye kuchaguliwa kuwa Waziri Mkuu,amepewa majukumu wakati nchi ipo katika hali mbaya,migogoro mingi,matatizo ya epa,Dowans n.k,jamani huyu mzee sio malaika,anatakiwa kupewa ushirikiano wa hali ya juu,kikubwa ambacho kinaiangamiza nchi yetu ni RUSHWA, Rushwa katika nchi ya Tanzania mizizi yake ipo chini kiasi cha mita mia 500,je ni kiongozi gani anaeweza kuja kuing'oa?mimi kwa maoni yangu naomba kama hio hoja itapita ya Mh Waziri Mkuu kuwajibishwa na kujiuzulu,basi naomba Mh Zitto Kabwe apewe hio nafasi then tuone katika huo uongozi wake Tanzania itakua kama Brunei? once atakapo kua yeye ndio waziri mkuu?kuwa kiongozi katika nchi iliojaa ubadhilifu wa fedha za umma na kutawaliwa na RUSHWA sio mchezo.
 
freedom is coming tommorow... freedom is coming tommorow... keep singing.... freedom is coming tommorow..

big up to our freedom fighters,
1. tindu lissu
2. zitto kabwe
3. john mnyika
4. firikunjombe
5. witness kiwia
6 wilbrod slaa
7. halima mdee
8. joseph mbilinyi
9. mh wenje
10.mh mbowe
11.mh selasini
12 ndesamburo

n.k

people,s power ........................ people,s power

freedom is coming tommorow
 
Ndahani... No...lol. I am interested sana kwa sababu nje kabisa ya hio.. Believe me, Sio mwana CCM na I am not one wa kukataa entity yangu yoyote ile. Itanipa majibu mengi nikijua idadi. Hasa ni kwa namna gani siasa imekomaa nchini ama ipo bado kiasi gani kuwiva.

Siasa inakomaa taratibu taratibu. Woga wa huko nyuma umeanza kupotea na kusema kweli uchaguzi ujao utakuwa na upinzani mkubwa sana.
 
Sasa mbona zitto naye haeleweki chma gani maana yy kwenye nafasi ya chama kaandika kigoma kaskazini, dah huyu zitto mi simuwezi.
 
Siku zote NAKUPENDA, NAKUTHAMINI, NAKUAMINI, NAJIVUNIA NA "NAKUTETEA" pale watu wanapoonyesha kuto kuwa na imani na wewe. Najua upo kwa maslahi ya TAIFA zaidi. Mungu akutie nguvu na nitazidi kukuombea ufanikiwe wewe na chama chako katika harakati za KULIKOMBOA taifa hili kutoka mikononi mwa WADHALIMU wasio na uchungu na nchi hii, viongozi mafisadi, wenye dharau, wenye majivuno, wenye kebehi kwa wananchi, wasio na dira wala mwelekeo na mengi mengine yasiyoriddhisha na kujiona wao ni MIUNGU WATU na wapo kwa maslahi yao si kututetea sisi wanyonge. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
"Kanuni 27(4) Endapo manufaa ya Taifa yatahitaji....Spika anaweza, baada ya kushauriana na Kamati ya Uongozi....kuliita Bunge 'mapema' zaidi"
Hayo ni maneno ya Zitto on his twitter account now
 
Back
Top Bottom