Nadhani viongozi wengi wa chadema hamkujua kuwa watu tumechoka kiasi gani na tabia za viongozi wabovu na wasio na msimamo na hapa sasa mnatakiwa mjue nguvu ya umma ina uwezo gani na inataka nini kwa viongozi wa chadema kwa kifupi ni hivi hao wasaliti hata wangekwenda kwa Mbowe akasema amewasamehe na kuwarudisha tungenyamaza lakini tungesha wajua kuwa kuwa viongozi wa chadema hawana tofauti na magamba wa Vasco Da Gama hivyo tungejiondokea kimya na kutafuta chama chenye mwelekeo na kuhamia huko na kwa jambo hili mmeonyesha ukomavu kwa kusoma alama za nyakati na kujua wananchi wanataka nini na sio ubabaishaji na vyeo na ndiyo maana tulikuwa tayari kukosa madiwani na hata tubakiwe na madiwani wawili au mmoja wenye msimamo na siyo mamluki ya madiwani wasioelewa wananchi wanataka nini.