Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA)

Tayari taratibu za zabuni zimeshakamilika na mkandarasi anapaswa kuanza ujenzi. Manispaa ya Kinondoni imeshaweka alama ya "X" katika majengo ambayo yatapaswa kubomolewa kuwezesha upanuzi wa barabara husika unaofanywa na Wakala wa Barabara Mkoa wa Dar es salaam (TANROADS).

Tarehe 15 Septemba 2012 nilifanya mkutano wa hadhara Jimboni Ubungo kwenye kata ya Makuburi ambapo pamoja na maswali mengine niliulizwa ni lini ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kutoka Maziwa mpaka External ukiambatana na ujenzi wa daraja katika barabara husika utaanza.

Pamoja na kueleza hatua iliyofikiwa mpaka sasa nilitoa mwito wananchi wote ambayo makazi yao yamewekewa alama ya "X" ikiwa si wavamizi wa barabara wawasilishe kwa Manispaa ya Kinondoni maelezo na vielelezo vyao kwa kuzingatia Wakala wa Barabara Mkoa wa Dar es es salaam (TANROADS) wao wana bajeti ya ujenzi pekee na madai ya fidia kwa wenye uhalali yako chini ya Manispaa ya Kinondoni; tayari 17 Septemba 2012 baadhi ya wananchi wamewasilisha nyaraka zao.

Ikumbukwe pia kuwa kwa kutambua umuhimu wa suala hili nilichukua hatua mbalimbali za kibunge kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2011 ili barabara husika iweze kupandishwa hadhi na kujengwa kwa kiwango cha lami kwa haraka zaidi kwenye mwaka wa fedha 2011/2012 kuliko ilivyopangwa awali.

Niliziandikia mamlaka husika hususan Wizara ya Ujenzi na TANROADS kuzingatia barabara tajwa katika bajeti kwa lengo la kuchangia katika kupunguza msongamano, Wizara ya Ujenzi awali ilisema serikali kuu haiwezi kushughulikia barabara hiyo kwa kuwa iko chini ya Manispaa ya Kinondoni. Lakini, nikaendelea kuchukua hatua zaidi kwa njia za kibunge na za uwakilishi wa wananchi na hatimaye TANROADS ikaingiza barabara hiyo katika vipaumbele vyake na kutenga fedha za ujenzi wa kiwango cha lami kiasi cha shilingi bilioni 1.2.

Aidha, pamoja na kiwango hicho cha fedha kilichotengwa na TANROADS, tarehe 5 Machi 2012 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alieleza kuwa amewasilisha maombi mengine kupitia Mfuko wa Barabara (Road Fund) kwa ajili ya ujenzi wa daraja kubwa zaidi katika barabara hiyo kwenye eneo la Ubungo Kisiwani/External suala ambalo pia kwa nyakati mbalimbali nilihoji utekelezaji wake.

Izingatiwe kwamba tarehe 21 Machi 2012 niliunganisha wananchi kuchangia hatua za dharura za kufanya matengenezo ili kupunguza kero lakini nikasisitza kuwa suluhisho muhimu zaidi ni kupanua daraja la External katika Eneo la Ubungo Kisiwani ili kupunguza msongamano wa magari na kujenga barabara husika kwa kiwango cha lami hatua ambayo sasa inaelekea kuchukuliwa kwa haraka.

John Mnyika (Mb)
18 Septemba, 2012
 

Mheshimiwa, ipo shida kubwa na ni sugu ya maji katika maeneo yote ya Kimara, wananchi walio maeneo ya Kimara walikuchagua kwa lengo kuu la kutatua kero hiyo ambayo ilionekana kumshinda mh. Keenja, hivyo, fanya yote usipotekeleza hilo hakika utakuwa na kipindi kigumu sana katika eneo la Kimara.

Hivi maji bado hayatoki Ubungo? Nilidhani ahadi hii ya maji ilikuwa ni ahadi kuu iliyotolewa na Mbunge wakati akiomba kura mwaka 2010. Naamini muda wa kuitekeleza upo. Maana inaweza kweli kumpa shida mwaka 2015 atakapoomba kura tena.
 
Mnyika yale yote ulioahidi hujatekeleza hata moja, ila kwa kupiga domo bungeni hilo umefanikiwa, nia yetu ya wakazi wa ubungo ni kutekeleza uliyotuahidi vinginevyo 2015 ukae mguu sawa ukalime.

Hii Kabaka ameisoma au kaamua tu kubaka hoja ya kutokea kwenye vyombo vya habari.

Serayamajimbo
 
Kaka sisi wote ni mashaidi wa kazi kubwa na Mungu akutie nguvu sana kwa hili na pia pongezi zangu kwako
 
Msimtishe Mnyika wenyewe tangu 2010 hamkumpa waliompa wanamwamini; hakuna kama Mnyika mnapoteza muda kama mnatafuta penetration is a loss; mnataka mwanasiasa asiyeongea? mngetafuta BUBU; Ubungo hawakuchagua BUBU; walichagua mtu wa kuwasemea kero zao; ubinfsi na umagamba utawaua mkiona natengeneza miundombinu na kuunganisha wananchi kupigania haki zao mnakasirika kama magubu wachafu wakubwa nyinyi
 
Naomba kuunga mkono hoja hii kwa nguvu sana.
Nashauri ripoti hii uichapishe na kuisambaza ktk jimbo lote. Viongozi wote wa chama ktk ngzi kata na tawi waipate ili wawaeleze wananchi.Ofisi zote za chama iwe na nakala.

Pili, Ni ukweli kwamba wagombea watarajiwa wa vyama vyote wanaeneza taarifa za uwongo huko mtaani kuwa wewe ni mbunge wa magazeti na mjengoni. Ukisambaza taarifa hii utakuwa umekata mzizi wa fitina.

Tatu, si vibaya kama utawaambia wengine kupitia vyombo vya habari. Well, wako watakaosema unatafuta cheap popularity, lakini ndivyo walivyomsema mbowe na helikopta yake 2005 lakini baadaye nao wakamwiga.

kaka hiyo taarifa imeshasambazwa kwa wananchi hususani kwa kata nane ambazo mbunge alifanya ziara ya kufungua misingi ya chama na alikua anakabidhi taarifa hizi kwa viongozi wa misingi. kata ambazo tayari wameshakabidhiwa ni mabibo, mburahati, makuburi, kimara,msigani, kwembe, mbezi na goba.
 
Sio kwamba na roho mbaya na wewe ila 2015 ukishinda na kunya barabarani kwangu sio ogopi kusema ukweli Kwa mbunge mwenye maneno mengi wakati wananchi hatuoni kitu wewe wasikilize wapambe wako wanaokupamba ukajisikia umefanya kazi nzuri.2015 utapata jibu mark my word your one term member of parliament.
hata ulipo mnyima kura yako mwaka 2010 bado akawa mshindi. pili ukinya utazoa tu, sababu barabara kutoka magomeni hadi kiluvya itakua katika kiwango cha kimataifa (morogoro road), huo ni uongozi wa mnyika. tatu: kwa kuwa huna uhalali (ligitimacy) kwa umma basi mnyika bado atakua mbunge wako wa ubungo hata kama unachuki binafsi
 
Mkuu nimesoma na hiyo taarifa ni ya muda nrefu. Shida yangu ni kwamba Mnyika awashirikishe wananchi ili wachonge barabara kwa kutumia grader jipya la manispaa ya kinondoni. Tufanye hayo ili barabara ziwe passable wakati tunasubiri MCHAKATO

Kimbunga,

Asante. Nilikuwa mara mbili kabla ya kwenda bungeni. Wasiliana na Diwani Manota 0784954657 kwa maelezo zaidi na hatua zako za ziada. Mkikwama tuwasiliane tafadhali. Kazi njema.

JJ
 
mh,mbunge,hongera na pole kwa kazi nzuri uifanyayo.sie wananchi toka jimbo lako la ubungo tuko nyuma yako.leo naomba nikutonye tu kuwa sie wajasiriamali vijana wenzako hapa ubungo na dar kwa ujumla tunaathirika sana na umeme huu unaokatikakatika sana.wengi wetu tunamiliki biashara za umeme na tunashindwa kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine.biashara nyingi za kisasa zinahitaji umeme,sasa mtu unafanya ubunifu,halafu mara mgao,mara nguzo imeanguka,mara"tunafanya matengenezo",this is too much!matokeo yake tutalundikana wote eneo moja(lenye uhakika wa umeme) au kufanya biashara zisizohitaji umeme, woote ni mitumba tuu,woote ni Mwenge tuu mpaka basi kitu ambacho si kizuri kwa uchumi wa nchi.Tunaomba mchakamchaka mlioanzisha kumaliza mgao wa umeme uendelee ili na hili tatizo la kukatika sana umeme liishe wananchi tuwe huru kuinvest kwenye biashara yoyote tunayoitaka na popote tunapotaka vinginevyo na mie itabidi nichukue form ya kugombea ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA maana ndio ajira iliyobaki isiyohitaji umeme saaana!nimekuambia wewe kwa vile nakuamini mjeshi wangu,ni mbishi kama mie.GOD bless you,tupo pamoja kamanda.
 
mkuu mnyika nasikia ile barabra ya konoike road, mbezi mwisho ilitangazwa tenda na sasa wanafanya-evaluation kumtafuta mkandarasi, najua ni juhudi zako mkuu, ebu tupe feed back
 
ha ha haaa!bosi wangu De Melo naomba muagize contena ya pempaz nyiiingi sana pamoja na dawa moja hivi inaitwa flagil!
 
Nimesoma kazi ulizofanya, ofcourse nyingi sana nazijua lakini hata kama perfomance ya jimboni isingekuwa kubwa, bado kazi unazofanya bungeni ingenifanya nikuunge mkono tena kwa nguvu zote 2015 kama tulivyokuwa 2010. Bravo.
Hata hivyo, jiandae pia kupokea maoni ya Ritz & co.

Nakuunga mkono
 
Safi mnyika!magamba walie tu,na 2015 tunachukua temeke na kigamboni......nyambafuuu magamba
 
Kamanda hongera......wale waliokuwa wanaleta mabandiko yao kuhusu Jimbo la ubungo its your time kula waya!Pamoja tujaijenga ubungo yetu.
 
Back
Top Bottom