Swali la ugomvi: Mnataka vipi mabadiliko wakati tayari mmebadilika?

Sijui kama unajua watanzania wanataka nini, mabadiliko tunayotaka siyo ya vyeo kwamba katoka Slaa kaingia Lowassa hapana.

Watanzania tunataka mabadiliko katika maisha, elimu, afya, chakula bora, Miundombinu, utawala bora, freedom of expression, amani, maendeleo, nk.

In general watanzania wanataka maisha bora haijalishi nani atayaleta.

Tulisubiri mabadiliko hayo kwa zaidi ya miaka 50 tukidhani chama tulichokipa dhamana kitatuongoza kuelekea huko lakini hatuoni mabadiliko yeyote, ndiyo maana tumeamua kuwapumzisha tuweke walio na dhamira ya mabadiliko ya kweli watuongoze tunakotaka.
 
Yawezekana ni kweli usemayo juu ya wagombea hao wawili lakini kwangu mimi naamini kuwa Mungu ana sababu ya kumleta EL Ukawa, hao wabunge wengi unaosema watapatikana kwa sababu yake kwa namna fulani na baadaye vyama vita balance kwa maana ya nguvu za kuwa na uwezo wa kukamata dola wakati wa uchaguzi na wakati huo EL atakuwa amestaafu pengine baada ya miaka 5 ijayo.

Huoni kuwa atakuwa amechangia kuleta mabadiliko? Baada ya hapo kwa mpango wa Mungu atatokea kiongozi mwingine jasiri wa kutupeleka mbele zaidi.
 
Mkuu unataka kufanya siasa iwe kama dini sasa kuamini tuuuuuuu ilimradi ni imani. Lkn hata dini imeshasema imani bila matendo imekufa. Imani yako wewe ya hayo mabadiliko haina utendaji, imejaa nadharia tupu ndio maana unataka watu waendelee kutheorize milele na kuweka wagombea watakaowafanya wawe second-best siku zote.

Ktk Tanzania hii ya leo ni wewe na wenzako wachache ndio hawataki mabadiliko. Hata chama twawala nacho kinataka mabadiliko ndio maana wanasema Magufuli for change. Wamepuuza hata mbwembwe za Humphrey Polepole za kuleta misamiati ya mageuzi badala ya mabadiliko.

Kwa kuwa hakuna mabadiliko zaidi ya kupitishwa kwa katiba mpya ya wananchi, na kama kupigia kura UKAWA tarehe 25 Oktoba 2015 ni kupigia katiba ya wananchi na marupurupu yake, naam na ije siku hiyo haraka ili kupigia mabadiliko
 
Mbowe ni Political Entrepreneur.Kakutana na mazuzu anayaendesha kama gari bovu.
CAG Prof. Assad amlipua Magufuli.

Prof.Assad amehojiwa na idhaa ya Kiswahili ya UN, na kutoa madai kwamba Tanzania kuna tatizo la "POLITICAL ENTREPRENEURSHIP."

Anadai watu wanaendekeza faida binafsi ktk maamuzi yao wakiwa madarakani.

Amekwenda mbali na kusema ule mradi wa MAGUFULI wa kuuza NYUMBA ZA SERIKALI ni mfano wa "POLITICAL ENTREPRENEURSHIP."
 
Huo mfumo utawekwa na UKAWA, Rasimu ya Warioba ndio ina majibu yote na kama vipaumbele vya UKAWA visemavyo 1. Elimu 2.Elimu 3.Elimu 4. Low and order.

Kibaya zaidi sijawahi msikia EL akisungumzia kuhusu Katiba ya wananchi ya Warioba....inshort sijui msimamo wake hadi leo
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Cha kusikitisha ni kuwa wao wenyewe hawajui au hawataki kujua, hawaamini au hawataki kuamini kuwa tayari mabadiliko yameshatokea; mabadiliko ambayo yamewabadilisha wao. Kama watu wenye akili timamu walishapata mgombea wao wa Urais, wakampitisha na kumthibitisha halafu wiki chache baadaye wakaenda kumchukua mgombea toka CCM na hivyo wakamtupa mgombea wao wenyewe, tena si mtu baki tu Katibu wao Mkuu wa chama, watu hawa hawa wanaweza vipi kuja na kusema ati wanataka "mabadiliko"? Yaani, watu waliobadilika wanataka kubadilika tena? Waweje?

Vinyonga wa kisiasa?

Fikiria.

MMM

MMM ni vizuri ukamwacha DR.apunzike kwa amani,kama kweli kaacha Siasa maana hili la kutupwa kalizungumza mwenyewe na majibu yalitolewa na kila upande kwa kadri ya mipasho na mihemko yake.
Lingine ni kupongeze kuwa na roho ngumu kama ya Paka.

Lipi linakushangaza kama kumbadili mgombea na kumtupa Katibu Mkuu limewezekana ni lipi linakutia hofu kitashindikana?
Nimekuwa nikiuliza swali hili mara nyingi lakini hutoi jibu au mtazamo wako kama unavyoleta hoja hizi kwenye uwanja wa majadiliano ,labda kama ulilenga kuwalisha tu wasomaji kama ulivyofurahia miaka nenda rudi na hili limeonekana kuwa Kansa kwako kama hii ya CCM kujiona kuwa ni Watawala toka Mbinguni sijui.

Swali ni hili-Je Lowassa wa CCM hawezi kubadilika kama Binadamu?.
Au ubinadamu wa Lowassa ni tofauti na wengine?

Fisadi-akatubu na kuachana na dhambi ?

Suala lingine MMM wewe kwa wengine tunao soma mistari ya andishi tunajua si muumini wa Serikali Tatu; yaani Serikali ya Muungano,Tanganyika na Zanzibar hivyo kwako UKAWA ni ugonjwa mkumbwa kwa hiyo uwepo wake tayari kwao ni shida.
Lakini unachotakiwa kuelewa kuna nguvu ya UMMA na ambayo kupitia Tume ya KATIBA ilikuwa wazi hitaji la wananchi ilikuwa nini.
Kwa huu mshangao wako '' Yaani, watu waliobadilika wanataka kubadilika tena? Waweje?'' jibu rahisi ni kuwa bado mabadiliko yako mengi na yanakuja na usiwe na haraka muda utapupa jibu.

Kwanza Mfalme CCM aondoke.pili na muhimu sana Katiba Mpya kutoka hapo Nchi hii inazaliwa upya kimawazo na fikra-kutoka Raia hadi viongozi.

Ugonjwa huu wa Ukada wa Chama kila Mahalikwenye uendeshaji wa Serikali ni Ugonjwa mbaya kuliko kitu kingene kwa Maendeleo ya Jamii na utakuwa unanielewa na maanisha nini.

MMM unazidi kujiharibia reputation yako.
Ina maana hujui watanzania wanataka nini? Inamaana hujui ilikuwaje Ukawa ukatengenezwa?
Acha unafki.
 
Tanzania kamwe haiwezi kutawaliwa na chama kingine zaidi ya CCM.

CCM itatawala milele.

Anayebisha na alinakili hili bandiko langu kama rejea ya baadaye.

Narudia tena, CCM itatawala milele.
 
Yawezekana ni kweli usemayo juu ya wagombea hao wawili lakini kwangu mimi naamini kuwa Mungu ana sababu ya kumleta EL Ukawa, hao wabunge wengi unaosema watapatikana kwa sababu yake kwa namna fulani na baadaye vyama vita balance kwa maana ya nguvu za kuwa na uwezo wa kukamata dola wakati wa uchaguzi na wakati huo EL atakuwa amestaafu pengine baada ya miaka 5 ijayo.

Huoni kuwa atakuwa amechangia kuleta mabadiliko? Baada ya hapo kwa mpango wa Mungu atatokea kiongozi mwingine jasiri wa kutupeleka mbele zaidi.

Mkuu unataka kufanya siasa iwe kama dini sasa kuamini tuuuuuuu ilimradi ni imani. Lkn hata dini imeshasema imani bila matendo imekufa. Imani yako wewe ya hayo mabadiliko haina utendaji, imejaa nadharia tupu ndio maana unataka watu waendelee kutheorize milele na kuweka wagombea watakaowafanya wawe second-best siku zote.

Ktk Tanzania hii ya leo ni wewe na wenzako wachache ndio hawataki mabadiliko. Hata chama twawala nacho kinataka mabadiliko ndio maana wanasema Magufuli for change. Wamepuuza hata mbwembwe za Humphrey Polepole za kuleta misamiati ya mageuzi badala ya mabadiliko.

Kwa kuwa hakuna mabadiliko zaidi ya kupitishwa kwa katiba mpya ya wananchi, na kama kupigia kura UKAWA tarehe 25 Oktoba 2015 ni kupigia katiba ya wananchi na marupurupu yake, naam na ije siku hiyo haraka ili kupigia mabadiliko

1. Nini kinakufanya ufikiri Lowasa kapelekwa Ukawa na Mungu?
2. Nini kinakufanya ufikiri Lowasa atastaafu baada ya miaka mitano?
3. Nini kinakufanya uamini kuwa Lowasa atapitisha hiyo katiba unayoisema?
 
Tanzania kamwe haiwezi kutawaliwa na chama kingine zaidi ya CCM.

CCM itatawala milele.

Anayebisha na alinakili hili bandiko langu kama rejea ya baadaye.

Narudia tena, CCM itatawala milele.
Na mimi nimeweka Like kama kumbukumbu.
 
Mzee unazuia mafuriko nyuma ya kibodi,wenzio 32 na vyeo vyao yamewashinda sembuse wewe tena kwa fake ID
 
1. Nini kinakufanya ufikiri Lowasa kapelekwa Ukawa na Mungu?
2. Nini kinakufanya ufikiri Lowasa atastaafu baada ya miaka mitano?
3. Nini kinakufanya uamini kuwa Lowasa atapitisha hiyo katiba unayoisema?
Nini kinakufanya usifikiri kinyume chake?
 
Nilikuwa nikisoma thread za MM hata kama ni ndefu namna gani, na nitaendelea kuzisoma hasa ukizingatia zinazidi kuwa fupi baada ya Dr. Slaa kukatwa; Dr. Slaa (mimi ni mmoja wa watu tuliyemwita 'Rais wa mioyo yetu') ameondoka lakini sisi tunasonga mbele.

Watu tuliowaamini kama wachambuzi wetu wazuri wa mambo ya politics wanawaza tu uchaguzi huu (25th October) na miaka mitano utafikiri ndio mwisho wa dunia; sisi tunawaza miaka 50 ijayo.

Mimi namkubali sana Magufuli kuliko Lowassa - as an individual, lakini naamini sana katika Lowassa+CHADEMA kuliko Magufuli+CCM institutionally
 
Huyu Mwanakijiji anaonekana ni mtu wa kupishana na hali halisi siku zote. Hata mwaka 2005 alikuwa kinara hapa wa kumkubali na kumnadi Kikwete na wanao ona mbali walimuambia anakosea na kuwa hakuna jipya lolote litakalo tokea zaidi ya shida. Leo miaka kumi baadae anarudia kosa lile lile.

Kaka Ukiona Wamachinga. Wasukuma Mkokoteni. Mama Ntilie. bodaboda. Wamepata Akili. Alafu Wanaojidai Wasomi Akili Zao Zimetiwa Giza.

Basi ni Afadhali, Ya Busara Ya Mama Ntile. Boda Boda. Machinga. Na Wasukuma Mkoko Teni. Kwa Wingi Wao Waliotambua Kwamba Sasa ni Wakati Wa Mabadiliko.

Waache Watu Wenye Mawazo Kama Ya Kina Mzee Mwanakijiji. Wenye Imani Na Gari Mbovu.
 
Tanzania kamwe haiwezi kutawaliwa na chama kingine zaidi ya CCM.

CCM itatawala milele.

Anayebisha na alinakili hili bandiko langu kama rejea ya baadaye.

Narudia tena, CCM itatawala milele.

Dah. Kumbe Hata Nyani Naye Ameacha Kurukia Miti. Naekaja Kuisaidia Ccm? Teh. Teh. Teh.
 
Back
Top Bottom