Swali la kizushi: Jimboni au Dodoma?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,996
Ukiwasikiliza wengi wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge wanatoa sababu za mambo gani wanataka kuyafanya kwenye majimbo yao (nimeandika kwa kirefu kwenye Mwanahalisi kesho) "wakishirikiana" na wananchi. Wengi ya wagombea wanatuambia mambo ambayo hatimaye wameyagundua yanahitajika kwenye majimbo yao na kuwa sasa hatimaye matatizo hayo yatapatiwa ufumbuzi.

Wagombea karibu wote hawataki kutuambia nini watafanya wakienda Dodoma kubadilisha mfumo wa utawala wa kifisadi ambao matokeo yake ni hayo matatizo wanayoyaona kwenye majimbo yao. Wagombea hawa wanaamini wanaweza kueffect change bila kubadilisha yanayotokea Dodoma au Ikulu.

Binafsi nakataa.. nataka nijue watafanya nini wakienda Dodoma kubadisliha mfumo wa utawala ili uwe wa kuwajibishana zaidi, wenye kujali zaidi matokeo bora na wenye kuhakikisha haki na usawa vinalindwa? Je yawezekana kweli kuleta mabadiliko kwenye majimbo bila kubadilisha kinachotokea Dodoma?

Si ndio maana wenzetu wanapogombea kama hapa US wanazungumzia what they want to do in "Washington" meaning there is a direct link between what is happening in the national Legislature and the local politics or affairs.

Au tuwahukumu tu kwa yale wanayosema wanataka kufanya majimboni mwao wakati rekodi ya miaka 50 inaonesha kuwa that alone is not enough?
 
Unaongelea wagombea gani? Huwezi kutegemea status quo ibadilishe status quo.
 
Mbunge anaweza akawa na michango ya kuleta changes lakini juu ya uwingi wa wabunge wa chama tawala hata maoni na mawazo yake yasipewe umuhimu....Au bunge linaweza kuamua juu ya swala flani (rejea Sakata la Richmond) lakini serikali isistekeleze....So mabadiliko juu ya wagombea yataletwa na Kura zetu sisi wenyewe, ni kuwaondoa wale wale na chama chao kilekile.....otherwise mi ntawaunge mkono wabunge waongelee kwa watakacofanya majimboni kwao.....
 
Unaongelea wagombea gani? Huwezi kutegemea status quo ibadilishe status quo.

sasa kwanini hawa watu wanakuja na kutuahidi kufanya mambo 1001 wakati status quo iko vile vile? Yaani wananiboa sana mtu anatangaza nia ya kugombea na kuahidi kushirikiana kutatua matatizo ya wananchi na kufanya x,y, z huku mfumo ukiwa umebakia ulivyo. Wataweza vipi? Maana nikikumbuka wabunge wanaoondoka mwaka huu na wenyewe walisema hivyo hivyo 2005, na wengine the same was said in 2000 na before..
 
Hapo ndipo utajua kama mtu anatafuta mabadiliko ya kweli kwa wananchi au anatafuta kura ili kula.

Kwa mtu mwenye akili na anayetafuta mabadiliko ya kweli bungeni kwetu ni pa kupaogopa, kwa sababu mtu unaweza kuji set up to fail kama kweli unatafuta kuweka mabadiliko yanayofuata standards, labda ukubali ku sacrifice principles nyingi tu ili uweze kuwa na gradual change, na ukishaanza kusacrifice principle moja who is to say huta sacrifice nyingi au zote?.Sehemu yenyewe (bunge) bila patronism, innuendos na rushwa you are almost guaranteed kwamba huwezi kuingia, na hata ukiingia by the slimmest chance bila kutumia rushwa utapambanaje na ma party machinery huko juu ambayo yako corrupt by default? And I am not talking only about the ruling party, this applies to the opposition as well.

Ndiyo maana wagombea ndiyo walewale waliokuwa ofisi ya rais wakashindwa kufanya kitu (The January Makambas and Pindas) wanaopitia upinzani ni wachache na wako prone kuwa enticed and silenced (sijaona mbunge wa upinzani machachari ambaye hajafail victim kwa machinations za CCM/ party machineries, from Mrema to Zitto Kabwe and Slaa).Kwa hiyo hata hawa, the more they spend time bungeni, the more they start to lose their edge and start to be career politicians who are going through the motions without convictions.

Ndiyo maana nikauliza, wagombea wenyewe ni wapi? Hawa watumishi wa serikali na mashirika ya umma wanaostaafu na kukosa kazi, pamoja na wanaoacha kazi wengine na incumbents, au kuna watu walio na some fresh ideas?

Maana kama ulivyo imply, hatuwezi kubadilisha kitu kwa kufanya mambo vile vile.
 
Hakika wakifirikia KUBADILI MFUMO KWA DHATI nao wataacha kugombea.....
 
Hakika wakifirikia KUBADILI MFUMO KWA DHATI nao wataacha kugombea.....

ndio maana naona wanaogopa kabisa kusema wanataka kuufumua mfumo mbaya wa kifisadi uliopo. Hakuna hadi hivi mgombea yeyote ambaye amedokeza kuwa kuna tatizo katika mfumo wa utawala wetu na tatizo lenyewe linatokana na ufisadi. Na kuwa tatizo hilo linaweza kushughulikiwa wakipatikana watunga sheria mahiri na wanaojua kutunga sheria. Maana ukiwasikiliza karibu wagombea wote hakuna anayezungumzia suala la kutunga sheria kama sababu ya yeye kutaka kugombea kwa sababu akiulizwa anataka kutunga sheria gani na kwanini hatakuwa na jibu!
 
Ukiwasikiliza wengi wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge wanatoa sababu za mambo gani wanataka kuyafanya kwenye majimbo yao (nimeandika kwa kirefu kwenye Mwanahalisi kesho) "wakishirikiana" na wananchi. Wengi ya wagombea wanatuambia mambo ambayo hatimaye wameyagundua yanahitajika kwenye majimbo yao na kuwa sasa hatimaye matatizo hayo yatapatiwa ufumbuzi.

Wagombea karibu wote hawataki kutuambia nini watafanya wakienda Dodoma kubadilisha mfumo wa utawala wa kifisadi ambao matokeo yake ni hayo matatizo wanayoyaona kwenye majimbo yao. Wagombea hawa wanaamini wanaweza kueffect change bila kubadilisha yanayotokea Dodoma au Ikulu.

Binafsi nakataa.. nataka nijue watafanya nini wakienda Dodoma kubadisliha mfumo wa utawala ili uwe wa kuwajibishana zaidi, wenye kujali zaidi matokeo bora na wenye kuhakikisha haki na usawa vinalindwa? Je yawezekana kweli kuleta mabadiliko kwenye majimbo bila kubadilisha kinachotokea Dodoma?

Si ndio maana wenzetu wanapogombea kama hapa US wanazungumzia what they want to do in "Washington" meaning there is a direct link between what is happening in the national Legislature and the local politics or affairs.

Au tuwahukumu tu kwa yale wanayosema wanataka kufanya majimboni mwao wakati rekodi ya miaka 50 inaonesha kuwa that alone is not enough?

MKJJ,

Watangaza nia wote wanajua ili kupata kura ni lazima wapiga kura ndo uwatangulize mbele. At the same time watangaza nia wameshajua wadanganyika wote tunapenda mepesi mepesi, kwa hiyo vinavyoonekana katika majimbo ndiyo wanaanza nayo in a drama style!!!

Wadanganyika hatuelewi uhusiano wa viongozi na Dodoma na baadaye Dar!! Wadanganyika wengi tunajua atakayekaa magogoni "huwa" tunaletewa na NEC na sisi tunafuata kama kondoo apelekwaye kutolewa sadaka!!

Safari bado ni ndefu sana!!!!
 
sasa kwanini hawa watu wanakuja na kutuahidi kufanya mambo 1001 wakati status quo iko vile vile? Yaani wananiboa sana mtu anatangaza nia ya kugombea na kuahidi kushirikiana kutatua matatizo ya wananchi na kufanya x,y, z huku mfumo ukiwa umebakia ulivyo. Wataweza vipi? Maana nikikumbuka wabunge wanaoondoka mwaka huu na wenyewe walisema hivyo hivyo 2005, na wengine the same was said in 2000 na before..

Labda Wabongo wamezoea kudanganywa na kusikia ahadi kemkem ambazo haziwezi kutimizwa. Hakuna hata utaratibu wa kuwauliza maswali hawa waheshimiwa kuhusu walichofanya huko nyuma ambacho kitaonyesha utendaji wao mzuri. Watasimama mbele ya wapiga KULA na kuanza kubwata bla bla bla bla na kisha kupanga mikakati ya wizi wa kura ili kuingia mjengoni. Kwa maoni yangu more than 85% ya Wabunge wetu hawastahili kuwemo bungeni maana hakuna lolote wanalolifanya miaka nenda miaka rudi.
 
Back
Top Bottom